Sunday, March 25, 2012

SIMBA UWANJANI TENA LEO KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Timu ya Simba ya Tanzania itachuana na wawakilishi kutoka Algeria timu ya ES Satif katika mashindano ya kombe la wawakilishi hatua ya kwanza. mchezo huo utachezwa katika uwanja wa taifa kuanzia saa 9 alasiri. makocha wa timu zote mbili wamejigamba kuibuka na ushindi. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki wawakilishi pekee wa Tanzania Simba spoti klabu.

Friday, March 23, 2012

IFAHAMU SIMBA SPORT CLUB

SIMBA SC: Imetoka wapi? NCHINI Tanzania, Simba ni jina kubwa kuliko kinywaji cha Cocacola. Ni miongoni mwa timu mbili zenye washabiki wengi zaidi si tu nchini humu, lakini katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki. Ina majina mbalimbali ya utani kama vile Wekundu wa Msimbazi na Lunyasi na ina makao yake makuu katika mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam. Timu hii ilianzishwa mwaka 1936 jijini Dar es Salaam ikitumia jina la Queens lakini baadaye lilibadilisha jina na kuitwa Eagle kabla ya kubadilishwa tena na kuitwa Sunderland –jina lililotumika hadi mwaka 1971 ambapo ndipo jina la Simba Sports Club lilianza kutumika. Ingawa tayari jina la Sunderland lilikuwa maarufu na kubwa tayari, lilibadilishwa na kuwa Simba; jina la mfalme wa msituni, ikiwa ni kutokana na pendekezo la aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, ambaye alishauri jina libadilishwe wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la makao makuu ya klabu mtaa wa Msimbazi. Katika majina yaliyopendekezwa, jina la Simba lilikubaliwa zaidi na wengi na likaamuliwa kutumika kuanzia mwaka huo wa 1971. Simba ilianza kutanuka zaidi wakati ikitumia jina la Sunderland. Ilikuwa na matawi yake katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ambapo ziliundwa timu zilizokuwa na kazi ya kupika wachezaji waliokuja kuchezea Simba baadaye. Miongoni mwa timu hizo ni Morning Stars, Canada Dry, Liverpool na Ilala Stuff, ambako huko mchezaji aliyeonekana kukomaa alipelekwa kukipiga Sunderland. Majina Maarufu Zaidi ya jina la Simba, kama zilivyo timu nyingine maarufu duniani, timu hii pia hutambulika kwa majina mengine tofauti. Hufahamika pia kwa jina la Wekundu wa Msimbazi, Taifa Kubwa na Lunyasi. Jezi Klabu ya Simba huvaa jezi nyekundu katika uwanja wake wa nyumbani na nyeupe inapokuwa ugenini. Wakati mwingine huvaa jezi zenye mchanganyiko wa rangi hizo mbili. Uongozi CHOMBO cha juu kabisa cha maamuzi katika klabu ya Simba ni Mkutano Mkuu wa Wanachama ambao ndiyo huchagua viongozi wa klabu. Shughuli za kila siku husimamiwa na Kamati ya Utendaji ingawa sekretarieti ndiyo huzifanya kwa maelekezo ya kamati. Kiongozi wa Kamati ya Utendaji ni Mwenyekiti wa klabu na yeye pamoja na kamati yake yote inawajibika kwa wanachama moja kwa moja. Safu ya Uongozi kwa Sasa Mwenyekiti Ismail Aden Rage Makamu Mwenyekiti Geofrey Nyange Katibu Mkuu Evodius Mtawala Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Joseph Itang’are Said Pamba Daniel Manembe Francis Waya Sued Mkwabi Ibrahim Masoud Zakaria Hans Pope NB: Kwa nyadhifa zao, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa nyadhifa zao MATAJI KATIKA historia yake, Simba imetwaa jumla ya mataji 36, yakiwamo 17 ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, katika michuano mbalimbali ambayo imeshiriki tangu ianzishwe. Mataji hayo yanajumuisha ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi ya Muungano, Kombe la Nyerere, Kagame na Kombe la Mapinduzi. Haya Ndiyo Mataji Yaliyochulikuwa na Simba UBINGWA WA LIGI KUU: 1965, 1966, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004 na 2007 (Ligi Ndogo) na 2010. LILILOKUWA KOMBE LA NYERERE: 1984, 1995 na 2000 LILILOKUWA KOMBE LA MUUNGANO: 1993, 1994, 1995, 2001, na 2002 KOMBE LA TUSKER: 2001, 2002, 2003 na 2005 KOMBE LA CAF: Ilifika fainali mwaka 1993 KOMBE LA KAGAME: 1974, 1991, 1992, 1995, 1996 na 2002 LIGI YA MABINGWA AFRIKA: Kucheza hatua ya makundi 2003 KLABU BINGWA AFRIKA: Kucheza Nusu Fainali 1974 KWA TAARIFA ZAIDI TEMBELEA TOVUTI HII http://simba.co.tz/club-info

WANYARWANDA KUCHEZESHA MECHI YA SIMBA NA ES SATIF

HUDU Munyemana ametangazwa kuwa mwamuzi wa pambano la Kombe la CAF baina ya Simba na ES Setif kutoka Algeria lililopangwa kufanyika Machi 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), mwamuzi wa kati katika pambano hilo atakuwa Hudu Munyemana kutoka Rwanda ambaye atasaidiwa na Felicien Kabanda na Theogene Ndagijimana huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Edouard Bahizi. Kwa mujibu wa CAF, Kamisaa wa pambano hilo atakuwa ni Felix Tangawarima kutoka Zimbabwe na waamuzi hao watakiwa kuwasili nchini siku mbili au tatu kabla ya mechi kulingana na usafiri ulivyo. Mwamuzi Munyemana amewahi kuchezesha mechi mbalimbali za Simba katika Kombe la Kagame na pia mwaka juzi alikuwa mwamuzi katika mchuano wa Kombe la CAF baina ya Doula ya Cameroon na ES Entente ya Algeria inayocheza na Simba. http://simba.co.tz/sites/default/files/imagecache/news_full/news/huuudu.JPG http://simba.co.tz/news/club-news/2012/03/17/warwanda-kuchezesha-mechi-ya-simba-na-es-setif.html

PRIMIER LEAGUE THIS WEEKEND

LIGI YA UINGLEZA ITAENDELEA TENA KESHO KWA MECHI NNE AMBAPO CHELSEA WATAIKARIBISHA SPURS SAA 9.45 ALASIRI BAADAYE SAA 12.OO JIONI ARSENAL WATAIKARIBISHA ASTON VILLA, LIVER POOL WATAKUWA WENYEJI WA WIGANI NA BOLTON WATAIKARIBISHA TIMU ILIYOZINDUKA YA BLACKBURN ZAIDI TEMBELEA TOVUTI IFUATAYO http://www.bbc.co.uk/sport/football/premier-league/fixtures

Friday, March 16, 2012

RATIBA LIGI YA MABINGWA ULAYA UEFA HATUA YA NANE BORA HADHARANI

Timu ya Chelsea ya England itakutana na Benifica ya Ureno katika hatua ya nane bora, ratiba kamili ya mechi hizo iliyotolewa leo inaonesha kama ifuatavyo:- CHAMPIONS LEAGUE FIXTURES Tuesday 27 March: Benfica v Chelsea, Apoel v Real Madrid Wednesday 28 March: Marseille v Bayern Munich, AC Milan v Barcelona Tuesday 3 April: Bayern Munich v Marseille, Barcelona v AC Milan Wednesday 4 April: Chelsea v Benfica, Real Madrid v Apoel Tuesday 17 April: Marseille or Bayern Munich v Apoel or Real Madrid Wednesday 18 April: Benfica or Chelsea v AC Milan or Barcelona Tuesday 24 April: AC Milan or Barcelona v Benfica or Chelsea Wednesday 25 April: Apoel or Real Madrid v Marseille or Bayern Munich Saturday 19 May: Final

Wednesday, March 14, 2012

Anzhi Makhachkala chasing Messi, Ronaldo and Bendtner,

TRANSFER GOSSIP Germany international striker Lukas Podolski, 26, has had a medical paving the way for his £10m move from Cologne to Arsenal. Sun Full story: Daily Star Lille midfielder Eden Hazard says he was "excited" to hear of Sir Alex Ferguson's scouting trip to see him, and would be interested in joining Manchester United. Full story: The Telegraph Blackburn Rovers manager Steve Kean says he has not given up hope of keeping 21-year-old winger Junior Hoilett, who is out of contract in the summer. Full story: Lancashire Telegraph Russian side Anzhi Makhachkala are ready to offer striker Nicklas Bendtner a route out of Arsenal in the summer, with Sunderland unlikely to make his loan permanent. Full story: Metro Liverpool and Arsenal have both joined the race to sign Spanish winger Jose Manuel Jurado, who currently plays for Schalke. Full story: Footy Latest Roberto Carlos hopes to sign both Cristiano Ronaldo and Lionel Messi for Russian side Anzhi Makhachkala. Full story: Marca (in Spanish) Steve Bruce set to open talks with Wolves Bruce was sacked as Sunderland manager in November Napoli have told Chelsea and Manchester City that they will have to pay 'crazy' money to sign Uruguayan striker Edinson Cavani. Full story: the Sun OTHER GOSSIP Former Sunderland boss Steve Bruce is ready to resume talks with Wolves about becoming their next manager. Full story: Daily Mail Jack Wilshere has told his Arsenal team-mates that he could return to action from an ankle injury at the end of this month. Full story: Daily Express Carlos Tevez could remain at Manchester City beyond the end of the season after impressing with his attitude and desire to regain match fitness since returning to the club in February. Full story: the Guardian Former Arsenal star Ian Wright believes son Shaun Wright-Phillips and his Queens Park Rangers team-mates will be relegated and will be lucky to get a point from their remaining 10 league matches. Daily Mirror Full story: London Evening Standard Relegation would hit QPR hard financially because most of this season's big-name arrivals signed lucrative deals which do not include relegation clauses. Full story: the Mirror Chelsea interim coach Roberto di Matteo believes Fernando Torres has failed to score goals because he has a "psychological problem". Full story: Metro Real Madrid star Cristiano Ronaldo has ruled out a return to England instead insisting he will stay with the Spanish club. Full story: talkSPORT England fans travelling to Ukraine for Euro 2012 are being urged to make sure they are vaccinated against measles after an outbreak of the disease. Full story: Daily Mail AND FINALLY Tottenham playmaker Rafael van der Vaart has posted footage on Twitter of his five-year-old son Damian showing some impressive football skills.

Tuesday, March 13, 2012

ROSISKY SIGN NEW DEAL FOR ARSENAL

Rosisky amesaini mkataba mpya zaidi ingia hapa http://www.bbc.co.uk/sport/0/football/17340418 WAKATI HUO HUO ARSENAL JANA IMEPATA USHINDI WA 2 KWA 1 DHIDI YA NEWCASTLE zaidi ingia hapa http://www.bbc.co.uk/sport/0/football/17254808

YANGA YAKUMBANA NA RUNGU LA TFF

Timu ya yanga imeadhibiwa na shirikisho la soka la Tanzania kufuatia tafrani ya jumamosi ambapo wachezaji wake walimpiga refa wa pambano hilo. picha ifutayo inaonesha sakata hilo wachezaji wa yanga wakimpiga refa Nkongo Jumamosi iliyopita.zaidi bonyeza hapa http://www.mwanaspoti.co.tz/wcreadnews.php?id=10962

Saturday, March 10, 2012

NENO LA UZIMA



http://www.mwakasege.org/images/banner.jpg





SOMO
: IKIMBIENI ZINAA
Wiki ya Kwanza
          Je! Unaamini ya kuwa Mungu anaweza kusema na watu kwa njia ya ndoto? Najua ni rahisi kuamini kuwa Mungu alisema na watu zamani kwa njia ya ndoto kama tunavyosoma katika Biblia; lakini je! Unaamini ya kuwa Mungu anasema na watu kwa njia ya ndoto siku hizi?
          Najua kuna watu wanaoamini na wengine hawaamini. Sijui wewe uko upande gani.
          Lakini nataka nikueleze hivi; Kufuatana na Biblia kuna ndoto za aina tatu;
(a)              Kuna ndoto kutoka kwa Mungu. Soma kitabu cha Hesabu 12:6, na Yoeli 2:28.
(b)              Kuna ndoto zinakuja kwa sababu ya shughuli nyingi. Soma kitabu cha Mhubiri 5:3.
(c)              Kuna ndoto za uongo zinazotoka kwa shetani aliye baba wa uongo. Soma kitabu cha Yeremia 23:52 na Yohana 8:44.
Unaweza kutofautisha kwa namna gani tofauti iliyopo kati ya hizi ndoto? Na utajuaje kuwa ndoto uliyoiota imetoka kwa Mungu? Kila ndoto lazima ipimwe na Neno la Mungu. Ikiwa imetoka kwa Mungu, ni lazima utakuta neno la Mungu ambalo linaeleza maana yake. Mara nyingine ndoto toka kwa Mungu huja kama fumbo; lakini Roho Mtakatifu ajuaye kuyafumbua mafumbo ya Mungu (1 Wakorintho 2:10,11), atalifunua fumbo hilo kwa kukuonyesha neno la Mungu linalofanana na ndoto hiyo.
Si busara kuzikubali ndoto zote unazoota bila ya kuzipima katika Neno la Mungu. Na pia si busara kuzikataa ndoto zote bila kuzipima katika Neno la Mungu.
Nimeona nianze kwa kukueleza haya kwa kuwa chanzo cha kuandika kitabu hiki, ni ujumbe wa Mungu ulionijia kwa njia ya ndoto.
Ndoto yenyewe ilikuwa hivi: Niliona katika ndoto mtu mmoja mkristo, tena aliyeokoka akifanya mambo ya zinaa bila hata kuogopa. Na wakati nilipokuwa nikimtazama na kusikitika, nikasikia sauti toka juu yangu ikisema;
“ NITACHUKULIANA MPAKA LINI NA MWANADAMU AFANYAYE MAMBO YA JINSI HIYO?” Baada ya kusikia maneno hayo nikaamka.
Wakati huo ulikuwa ni alfajiri, na ndoto hiyo ilinipa maswali na masononeko mengi moyoni mwangu. Na niliamua kumshirikisha mke wangu Diana juu ya ndoto hiyo.
Mke wangu akaniuliza; “ Maana yake nini ndoto hiyo?”
Nilipotaka kufungua kinywa ili nimjibu uchungu mzito ulijaa moyoni mwangu, nikasikia kuugua rohoni, na mara nikaanza kulia!
Unaweza ukaniuliza; “Mwakasege kwa nini ndoto ikulize machozi?”
Hili ni swali zuri. Hata mimi nilijiuliza kwa nini nitoe machozi kwa ajili ya ndoto. Lakini baada ya kulifuatilia jambo hili katika maombi na katika neno la Mungu nilielewa sababu yake.
Je! Unafahamu matokeo ya Mungu kusema “Nitachukuliana mpaka lini na mwanadamu afanyaye mambo ya jinsi hiyo?” Ukisikia maneno ya jinsi hii ujue Mungu amekasirika na kuna maangamizo mbele.
Hebu na tulifuatilie jambo hili katika biblia ili tulione uzito wake.
Nuhu na Gharika.
Ni vizuri ukumbuke ya kuwa gharika ilitokea wakati wa Nuhu kwa sababu ya zinaa.
“Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliona hao binti za wanadamu – ni wazuri; WKAJITWALIA WAKE WO WOTE WALIOWACHAGUA. Bwana akasema, ROHO YANGU HAITASHINDANA NA MWANADAMU MILELE, kwa kuwa yeye ni nyama; basi siku zake zitakuwa mia na  ishirini. Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile, tena baada ya hayo, wana wa Mungu WALIPOINGIA kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa. BWANA AKAONA YA KUWA MAOVU YA MWANADAMU NI MAKUBWA DUNIANI NA KWAMBA KILA KUSUDI ANALOWAZA MOYONI MWAKE NI BAYA TU SIKU ZOTE. BWANA AKAGHAIRI KWA KUWA AMEMFANYA MWANADAMU DUNIANI, AKAHUZUNIKA MOYONI. Bwana akasema, Nitamfutilia usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambulisho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana.” (Mwanzo 6:1-8)
Ukiendelea kufuatilia habari hii katika Biblia utaona ya kuwa baada ya gharika ya maji walibaki watu nane tu! Wanadamu wengine wote waliangamia kwa sababu ya nini? – Zinaa!
Sodoma na Gomora
Wasomaji wa Biblia wanafahamu kabisa ya kuwa miji ya Sodoma na Gomora iliteketezwa kwa moto baada ya Mungu kuihukumu kwa sababu ya uasherati uliokuwa ukifanyika ndani yake. Soma Mwanzo 19:4-25.
Na pia katika kitabu cha Yuda 1:7 tunasoma hivi: -
“Kama vile Sodoma na Gomara, na miji iliyokuwa kando kando, waliofuata UASHERATI kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.”
Ikiwa Mungu aliwatenda hivi watu wa Sodoma na Gomora, ni kitu gani kinamfanya mwanadamu wa siku hizi adhani ya kuwa Mungu amebadilika juu ya kuadhibu wale wote wafanyao uasherati? Katika miji hiyo miwili ni watu watatu tu waliobaki – Lutu na watoto wake wawili! Wanadamu wengine waliokuwa katika miji hiyo waliteketezwa kwa sababu ya nini – Zinaa!
 Kuhani Eli na watoto wake.
“Basi Eli alikuwa mzee sana, naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Waisraeli; na jinsi WALIVYOLALA NA WANAWAKE waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania.” (1Samweli 2:22)
Hata baada ya baba yao kuwaonya hawakusikia, na matokeo yake ni:-
1.                  Watoto hao wawili, Hofni na Finehasi walikufa wote siku moja;
2.                  Wana wa Israeli walipigwa na adui zao Wafilisti na Sanduku la agano likatekwa;
3.                  Kuhani Eli alikufa.
Yote haya yalitokea katika taifa ambamo watoto wawili wa kiongozi waliuwa wakifanya mambo ya Zinaa bila hata kujali maonyo.
Je! Bado unajiuliza kwa nini nilitoa machozi baada ya kusikia sauti ya Mungu katika ndoto ikisema “Nitachukuliana mpaka lini na mwanadamu afanyaye mambo ya jinsi hiyo?”
Siku za Mwisho.
“Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi…….Kwa maana katika hao wamo wale WAJIINGIZAYO KATIKA NYUMBA ZA WATU, NA KUCHUKUA MATEKA WANAWAKE WAJINGA WENYE MIZIGO YA DHAMBI, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi. (2 Timotheo 3:1,26).
Je! Siku hizi wanawake hawatekwi mateka na wanaume ili wafanye mambo ya zinaa? Vishawishi vimekuwa vingi, na wanawake wengi wameanguka katika mitego hiyo ya kupenda fedha na anasa, na mwisho wake ni kufanya uzinifu.
Kwa nini wanaume wengi wamekosa akili juu ya jambo hili. Ni kitu gani kimewapofusha macho wasione ya kuwa uzinifu ni mbaya? Biblia inasema; “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomangamiza nafsi yake.” (Mithali 6:32)
Ni dhahiri ya kwamba palipo na zinaa pana uharibufu, na wengi wanaangamia. Na nataka nikuambie ya kuwa Roho Mtakatifu akikuwekea mzigo huo ndani yako na kuliona jambo hili jinsi linavyomhunish Mungu, hakika hutatulia; na hapana budi macho yako yatajaa machozi juu ya kizazi hiki kinachojiangamiza chenyewe kwa sababu ya zinaa.
Sababu ya mambo haya kuandikwa.
Mambo haya hayakuandikwa kwa bahati mbaya, wala si kwa ajili ya kuonyesha historia ya watu Fulani tu. Bali yaliandikwa kwa kusudi maalumu na muhimu.
“Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili KUTUONYA SISI, tuliofikiriwa na miisho ya zamnai – Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.” (1 Wakorintho 10:11,12)
Na mimi nimependa kuyaonyesha wazi ili tujue tunapozungumza juu ya zinaa, Bwana Mungu anakuwa na mawazo gani juu yake. Nafahamu si mara kwa mara hata katika mahubiri na mafundisho, jambo hili huguswa kwa undani. Lakini naona umefika muda wa kulichambua jambo hili kwa undani zaidi.
Hali ilivyo sasa.
          Mtu mmoja aliniuliza “Je, mtu aliyeokoka anaweza kufanya mambo ya uasherati – je, anaweza kuzini?”
          Nikamwambia, “Mtu aliyeokoka hatakiwi kufanya mambo ya uasherati, kwa kuwa kufanya hivyo ni dhambi, lakini asiposimama katika Kristo sawasawa anaweza kuzini.”
          Halafu huyo mtu akaendelea kuuliza, “Je, Unamfahamu Fulani? (Akamtaja jina lake).
            “Ndiyo namfahamu.” Mimi nilimjibu, na nikaendelea kusema; - “ kuwa ni mtumishi wa Mungu, ingawa sijamwona muda mrefu umepita sasa”.
          Ndipo akasema, “Unafahamu ya kuwa alianguka na akazini na msichana Fulani (akamtaja jina lake) ambaye pia ameokoka, na sasa yule msichana amezaa?”
          Mimi nilishangaa na kushutushwa na habari hizo. Nikamuuliza “Unasema kweli ndivyo ilivyotokea?”
          Akasema, “Ndiyo”
          Ndipo Roho wa Mungu aliponikumbusha ndoto ile aliyonipa. Katika ujumbe ule wa ndoto, Mungu alinionyesha mkristo aliyeokoka akifanya mambo ya uasherati.
          Kwa mtu asiyeokoka siwezi kushangaa akifanya uzinzi, kwa kuwa bado yuko gizani, na yuko chini ya mkuu wa giza, ibilisi – kwa hiyo anaweza kufanya lo lote lile. Ndiyo maana mtu anaweza kusema yeye ni mkristo, na huku anazini mara kwa mara.
          Mkristo wa kweli aliyeokoka hatakiwi kuzini, wala kushindwa na dhambi. Kwa nini? Kwa kuwa ndani yake ametengwa mbali na dhambi, na amepewa ushindi juu ya dhambi.
Ushindi dhidi ya dhambi
          Uhusiano wako na dhambi unakuwaje baada ya kuokoka, na kufanyika kiumbe kipya ndani ya Kristo? Watu wengi wakiisha-okoka, huwa bado wanasumbuliwa na kuanguka katika dhambi mara kwa mara, na hasa katika zinaa. Na hii inatokea kwa kuwa hawapati mafundisho ya kutosha ya neno la Mungu juu ya jinsi wanavyotakiwa kuenenda katika maisha mapya waliyopita.
          Kaini aliambiwaje na Mungu? Bwana alimwambia hivi; “ kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa UISHINDE” (Mwanzo 4:7)
          Na ndivyo ilivyo hata sasa. Bado tumo ulimwenguni humu, ingawa aliyezaliwa mara ya pili yeye si wa ulimwengu huu (Yohana 17:16). Lakini kwa kuwa bado  tumo katika ulimwengu uliojaa dhambi inayotutamani kila siku, na tusije tukajisahau. Inatupasa tuishinde.
Yanenaje maandiko?
Imeandikwa katika kitabu cha (Warumi 6:12-14)
“Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. Kwa maana DHAMBI HAITA WATAWALA NINYI, kwa sababu hamuwi chini ya sheria, bali chini ya neema”.
Ikiwa tunaambiwa ya kuwa “Dhambi haitawala ninyi …….” inakuwaje basi wengine wanatawaliwa nayo? Inakuwaje mtu wa Mungu, aliyepakwa mafuta kwa Roho Mtakatifu aanguke katika zinaa? Kitu gani kinampofusha macho ya rohoni?
Je! Ni halali kwa mtu anayekaa ndani ya Kristo kutenda dhambi?
Yanenaje maandiko?
“Kila akaaye ndani yake (Yesu Kristo) HATENDI DHAMBI; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtamua….atendaye dhambi ni wa ibilisi; kwa kuwa ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.” (1 Yohana 3:6,8)
Je! Unaona maneno haya yalivyoandikwa kwa ajili yetu? Sidhani kama unapenda tena kuwa Ibilisi kwa kuwa “Apendaye dhambi ni wa Ibilisi” Kwa hiyo ni muhimu ujilinde usitende dhambi.
Tena imeandikwa:
“Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu UZAO WAKE WAKAA NDANI YAKE; WALA HAWEZI KUTENDA DHAMBI KWA SABABU AMEZALIWA KUTOKANA NA MUNGU.” (1 Yohana 3:9)
Ikiwa umezaliwa mara ya pili kwa Roho wa Mungu, ujue hakika UZAO WA MUNGU unakaa ndani yako. Na uzao huu wa uungu ni Mtakatifu, na unakaa ndani yake bila kutangatanga unakuwezesha kuishi bila kutenda dhambi.
Je! Si jambo la kumshukuru Mungu hilo. Si kwamba anatuambia tusitende dhambi bila kutupa njia ya kutusaidia. Anajua sisi wenyewe hatuwezi kuishinda dhambi, BALI YEYE AKIKAA NDANI YETU NA SISI NDANI YAKE TUNAWEZA KUISHI KATIKA USHINDI DHIDI YA DHAMBI NA MITEGO YAKE YOTE.
Tena imeandikwa;
“Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu HATENDI DHAMBI; bali yeye aliyezaliwa na Mungu HUJILINDA, wala yule mwovu HAMGUSI.” (1 Yohana 5:18)
Ee, mtu wa Mungu, jilinde basi kwa kuwa umezaliwa na Mungu, kwa nini tamaa ya uasherati ikusonge? Je?! umesahau ni uzao wa namna gani ulio ndani yako?
Ni kweli kwamba mtu akitenda dhambi na akatubu, Bwana atamsamehe, (1 Yohana 1:9). Lakini hatutakiwi kutenda dhambi. Ndiyo maana imeandika; “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba MSITENDE DHAMBI”…. (1 Yohana 2:1)
Sasa naona unaweza kuelewa kwa nini inashtusha na kusikitisha unaposikia mtu wa Mungu ameanguka katika dhambi ya zinaa. Ikiwa maisha ya wokovu yatakuwa ni ya kuanguka na kusimama, halafu tena kuanguka na kusimama mara kwa mara; basi ina maana ya kuwa ushindi wa kutosha haukupatikana pale msalabani.
Lakini nataka nikuambie hivi, ushindi kamili ulipatikana pale msalabani bila kubakiza kitu! Ndiyo sababu Yesu Kristo alikuwa na ujasiri wa kusema ‘IMEKWISHA’ pale msalabani.
Tunachotakiwa kufanya ni kuwa watendaji wa neno; na ndiyo ushindi huo utadhihirika katika maisha yetu. Usidhani ya kuwa mapokeo ya wanadamu yanaweza kukusaidia kuishinda dhambi; la hasha! Yesu Kristo peke yake akikaa ndani ya   moyo wako, na neno lake ukilitii, ndiko utapata ushindi halisi na halali dhidi ya dhambi.
Swali la kujiuliza
Idadi ya wakristo waliookoka wanaoanguka katika dhambi ya zinaa inaongezeka siku baada ya siku. Na wengine wameanguka dhambini moja kwa moja, hata haja ya kutaka kusimama upya katika Bwana imepotea. Wanaona aibu! Na wengine wanaanguka na kusimama, halafu tena wanaanguka na kusimama. Na kwa sababu hiyo hawana ushuhuda mzuri mbele za watu. Hawaaminiki tena.
Lakini je! Unadhani Mungu atatuambia tuishinde dhambi wakati anafahamu ya kuwa hatuna uwezo huo? La hasha! Mungu wetu tunayemwamini katika Kristo Yesu si dhalimu kiasi hicho.
Jambo ninalofahamu ni kwamba ametuambia tuishinde dhambi kwa kuwa ndani yetu sisi tuliompokea, ametupa UWEZA WA KUISHINDA DHAMBI – kwa namna gani?
“Kwa sababu UZAO WAKE WAKAA NDANI YAKE (YETU) WALA HAWEZI (HATUWEZI) KUTENDA DHAMBI KWA SABABU AMEZALIWA (TUMEZALIWA) KUTOKANA NA MUNGU”.(1Yohana 3:9)
Uzao wako si uzao wa kuanguka dhambini, bali ni uzao wa kushinda dhambi, kwa kuwa Kristo anakaa ndani yako!
      











SOMO
: IKIMBIENI ZINAA
Wiki ya Pili
MKRISTO ANAANGUKAJE KATIKA ZINAA?
          Kila mara nilipopata habari za watu wa Mungu walioanguka katika dhambi ya zinaa nilikuwa najikuta najiuliza swali hili, “Hivi wanapataje ujasiri wa kutenda tendo hilo?”
          Akili yangu ilikuwa inakataa kabisa kuamini kuwa mtu aliyeokoka (na wakati mwingine amejazwa Roho Mtakatifu) anaweza kuanguka kwenye dhambi ya zinaa. Lakini hata hivyo bado nikawa naendelea kusikia majina ninayoyafahamu ya watu wa Mungu waliookoka waliokubwa na dhambi ya zinaa.
“Wanafanyaje mpaka wanaanguka katika zinaa”? Hili swali lilinisumbua kwa muda mrefu. Na siku moja nilikuwa nyumbani kwangu nikijiuliza swali hili moyoni, nikasikia Roho Mtakatifu akiniuliza ndani ya moyo wangu, akisema, “ Kwani Daudi aliangukaje? Je! Umesahau ya kuwa naye alikuwa mtu wangu, mtumishi wangu niliyempaka mafuta?
          Niliposikia swali hili, nilichukua biblia na kusoma maneno yanayoeleza kuanguka kwa Mfalme Daudi katika dhambi ya zinaa na mke wa mmoja wa askari wake.
          Mambo niliyoyasoma yalinifungua macho kuona jinsi ambavyo hata hivi leo watu wa Mungu wanavyoanguka au wanavyoweza kuanguka katika dhambi ya zinaa.
          Chukua biblia yako na usome habari hizi katika 2 Samweli 11:1-27 na 2 Samweli 12:1-25.
          Chanzo cha kuanguka kwa Mfalme Daudi katika dhambi ya Zinaa, ni KUTOKWENDA VITANI PAMOJA NA ASKARI WAKE.
“Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Daudi akampeleka Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote, wakaangamiza wana wa Amoni, wakakuhusuru Raba. LAKINI DAUDI MWENYEWE AKAKAA YERUSALEMU”. (2 Samweli 11:1)
          Kama kiongozi wao, Daudi alitakiwa kuongozana na watu wake vitani, lakini yeye aliamua kubaki Yerusalemu asiende vitani, na akamtuma mtu mwingine amwakilishe. Na jambo hili lilimpa nafasi nzuri sana ibilisi ya kumpa Daudi kazi nyingine ya kufanya. Ni kazi gani hiyo?
“Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, AKATEMBEA JUU YA DARI ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke ANAOGA; naye huyo mwanamke alikuwa MZURI SANA WA KUPENDEZA MACHO”. (2 Samweli 11:2)
Ni kitu gani kilimfanya Mfalme Daudi aamue kutembea juu ya dari ya jumba lake badala ya kwenda vitani pamoja na watu wake? Na alipomwaona Bathsbeba, mkewe Uria akioga alishindwa kujizuia, mwisho wake ni kuzini naye na huyo mama kupata mimba!
Wakristo wengi wamejikuta wameingia katika mtego wa zinaa kwa sababu ya kutokwenda ‘Vitani’ wakati wanapotakiwa kufanya hivyo. Vita tunavyovisema, si vita vya kimwili.
“Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili, maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome; tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo”. (2 Wakorintho 10:3,4)
Na pia imeandikwa; “ Kwa maana kushindani kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili juu ya majeshi ya pepo wabaya, katika ulimwengu wa roho”. (Waefeso 6:11)
Ndiyo maana Yesu Kristo alisema; “ Kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.” (Mathayo 26:41)
Usipovipiga vita katika maombi, inakuwa ni rahisi sana kuangushwa na majaribu unapokutana nayo. Wakristo wakipoa katika maombi inakuwa rahisi kuanguka katika dhambi, si katika zinaa peke yake, bali katika mtego wowote ambao shetani anauweka mbele yao!
Kutokuwa mwombaji, ni sawa na kutokwenda vitani na wenzako, kama vile Mfalme Daudi alivyofanya.
Kwa hiyo unaona ya kuwa ingawa Mfalme Daudi alikuwa mtu wa Mungu, mtumishi wake, na mpakwa mafuta wake, alianguka katika zinaa. Na hata hivi leo kuna wakristo, tena wameokoka, na kupakwa mafuta kwa Roho Mtakatifu, wanaonguka katika dhambi ya zinaa. Kwa nini? Kwa kuwa hawavipigi vita vya kiroho na wenzao, na wamepoa katika kumtumikia Bwana.
Je! Lutu aliangukaje?
Hili ni swali ambalo Roho Mtakatifu aliniuliza baada ya kunieleza habari za Mfalme Daudi. Ingawa Lutu alikuwa mtu wa Mungu, na licha ya kuwa alikuwa anabebwa kwa maombi ya Ndugu yake Ibrahimu, bado alianguka katika zinaa.
Roho Mtakatifu alikuwa anaendelea kunijibu swali nililokuwa najiuliza ya kuwa, watu waliookoka wanaangukaje katika zinaa?
Habari za kuanguka kwa Lutu zimeandikwa katika kitabu cha Mwanzo 19:30-38.
Lutu alizini na watoto wake wawili wa kike baada ya kuleweshwa mvinyo.
Na ukiisoma habari hii inasikitisha sana. Shetani alipata nafasi ya kumwangusha Lutu si kwa sababu ya binti zake kumlewesha mvinyo, bali kwa kuwa MKE WAKE HAKUWA PAMOJA NAYE. Unadhani mke wake angekuwapo hawa watoto wangepata nafasi ya kumlaghai baba yao? Hapana! Kwa nini?
Kwa maana “ Bwana ameumba jambo jipya duniani, mwanamke atamlinda mwanaume.” (Yeremia 31:22)
Unaweza kujiuliza ni kwa njia gani mke atalimnda mume wake. Kumbuka imeandikwa mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana. Kazi moja ya busara iliyo ndani ya mke ni kumlinda mume kutokana na mashambulizi ya Malaya! Soma Mithali 2:11-22.
Hata hivi leo ndoa ambazo mume na mke hawakai vizuri, huwa ni rahisi kwa wao kuanguka katika dhambi ya zinaa hata kama wameokoka. Na huu siyo ushuhuda mzuri.
Tunamshukuru Mungu kwa wale ambao wamesimama katika ushuhuda ingawa ndoa zao zina matatizo.
Jambo la kujifunza zaidi
Roho Mtakatifu alipokuwa anaendelea kunifundisha akasema ndani ya moyo wangu hivi; “Watu wengi wanadhani zinaa ni tendo la kimwili tu linalofanywa kati ya mwanaume na mwanamke nje ya ndoa, lakinikuna namna zaidi ya moja unayoweza kuanguka katika zinaa.”
Niliposikia hivyo moyoni mwangu, niliichukua biblia na nikaanza kuisoma upya juu ya zinaa na nikaona kuna namna nne ambazo zinaa inatajwa:-
1.     KATIKA MWILI:
“….Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili. Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya Kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? …. Ikimbieni zinaa, kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.” (1 Wakorintho 6:13-20)
2.     KUTAMANI KWA MACHO. Yesu Kristo alisema;
“Mmesikia kwamba imenenwa Usizini; lakini mimi nawaambia, kila mtu AMTAZAMAYE MWANAMKE KWA KUMTAMANI, amekwisha KUZINI NAYE MOYONI MWAKE.” (Mathayo 5:27,28)
3.     KUACHA MKE NA KUOA MWINGINE
Yesu Kristo alisema;
“Kila amwachaye mkewe na kuoa mke mwingine azini ……” (Luka 16:18)
4.     KUOA ALIYEACHWA. Yesu Kristo alisema;
“Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; NAYE AMWOAYE YEYE ALIYEACHWA NA MUMEWE AZINI.” (Luka 16:18)
          Kila mtu na ajipime katika hayo; ikiwa umefanya mambo kama hayo niliyoyataja, biblia inasema UMEZINI! Je       Hakuna waliokoka wanaofanya mambo ya jinsi hii? Wanaowaacha wake zao halali? – Wanaooa walioachwa? – na wanaozini katika mwili?











SOMO
: IKIMBIENI ZINAA
Wiki ya Tatu
USHAURI WA BIBLIA JUU YA KUEPUKANA NA ZINAA
“Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa…..” (Hosea 4:6). Haya ni maneno ambayo Bwana aliyanena kwa kutumia kinywa cha Nabii Hosea kwa watu wake, wana wa Israeli. Lakini maneno haya yanatuhusu watu wake hata leo.
Watu wa Mungu wengi sana nyakati hizi wanaangamizwa kwa kukosa maarifa – maarifa juu ya mapenzi ya Mungu. Na eneo mojawapo ambalo linaangamiza wengi ni eneo la uzinzi.
Kwa kukosa mafundisho ya kutosha juu ya neno la Mungu juu ya kusimama katika Kristo na kuepukana na zinaa, watu wa Mungu wengi wameanguka kiroho. Na wengine wanaishi maisha ya kuanguka na kusimama kuanguka na kusimama, - kitu gani kinawaangusha – zinaa!
Ndiyo maana Nabii Hosea alitumiwa na Bwana kuendelea kusema kuwa; “UZINZI na divai mpya huondoa FAHAMU za wanadamu” (Hosea 4:11). Kukosa fahamu ni sawa na kutojitambua uko wapi na unafanya nini. Na hii ni kweli kabisa, watu wanaofanya uzinzi wangekuwa na fahamu wangetubu na kuacha upesi, kwani madhara yake ni makubwa.
Imeandikwa,
“Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” (Mithali 6:23)
Kukosa kujua neno la Mungu linasema nini juu ya zinaa katika marefu na mapana yake, kumewafanya watu wengi wanaswe na mtego huu mbaya.
Kuna wakati fulani tukiwa kwenye mkutano wa kiroho mji mmoja hapa nchini, aliokoka msichana ambaye alikuwa kahaba katika hotel moja. Na wakati huo alipookoka alijazwa Roho Mtakatifu, akazungumza kwa lugha mpya.
Baada ya wiki kama moja hivi, watu wengine waliokoka waliamua kumtembelea, lakini hali waliomkuta nayo iliwasikitisha. Kwani walimkuta amerudi nyuma kiroho na amerudi kwenye maisha yake ya zamani ya ukahaba.
Alipoulizwa ni kwa nini imekuwa hivyo alijibu “ Naona nilikuwa nadanganywa na mambo ya wokovu, ili niache maisha haya mzuri (ya ukahaba)”
Je! Umeamini ya kuwa uzinzi huondoa fahamu za mwanadamu? Huyu binti atasemaje maisha ya ukahaba ni mazuri kuliko maisha ya wokovu? Ni wazi kwamba fahamu zake zimeondoka. Anafanya jambo la kumwangamiza nafsi yake, na anasema hayo ndiyo maisha mazuri!
Lakini naamini kabisa ya kuwa binti huyu angepewa ushauri wa biblia juu ya tatizo la zinaa, angekuwa na nafasi nzuri ya kuishi maisha ya ushindi katika Kristo. Kwa kukosa mafundisho hayo muhimu, kulisababisha hasara kwa nafsi yake.
Mambo matano muhimu ninayokwenda kuyajadili katika sura hii, ni ushauri mzuri wa biblia utakaoweza kukusaidia kuishinda dhambi hii ya zinaa. Lakini unabidi uwe mtendaji wa neno. Kuyasoma haya bila kuyatenda hayatakusaidia. Bali ukiyatenda, hakika utauona mkono wa Mungu.
1.     DUMU KATIKA MAOMBI
Yesu pale Gethsemane alisema;
“Je! Hamkuweza kukesha pamojanami hata saa moja? Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi. Lakini mwili ni dhaifu” (Mathayo 26:40-41)
Ukisha mpokea Kristo moyoni mwako, roho yako inakuwa radhi kumtii Kristo na kutokutenda dhambi; lakini kumbuka kuwa roho yako bado imo katika mwili ulio dhaifu ambao unataka kutenda dhambi.
Yesu Kristo alipokuwa akifundisha kuomba alisema sehemu mojawapo ya maombi yetu iwe;
“Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu, Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu na utukufu, hata milele, Amina.” (Mathayo 6:13). Watu wengine huwa wanaisema sala hii kikasuku bila kuangalia uzito wa maneno yaliyomo. Lakini ukijua uzito wake hutachoka kuomba kwa “ Na usitutie majaribuni.” Jaribu mojawapo ambalo unapaswa uombe uepushwe nalo ni zinaa.
Wengine wakianguka katika zinaa, utawasikia wakijitetea na kusema; “Nilibanwa mno hata nikashindwa kujizuia – nikaanguka katika zinaa.”
Unaweza ukajitetea hivyo, lakini ungeamua kushinda, Bwana angeuwezesha kushinda. Kwa kuwa imeandikwa; “ Ninyi watoto wadogo mwatokana na Mung; nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye NDANI YENU NI MKUU KULIKO aliye katika dunia.” (1 Yohana 4:4) “ Lakini katika mambo hayo yote TUNASHINDA NA ZAIDI YA KUSHINDANA kwa yeye (Yesu Kristo) aliyetupenda (Warumi 8:73)
Na ni budi pia ukumbuke, kila jaribu lina njia ya kutokea, si katika njia ya kushindwa bali katika mlango wa ushindi.
“Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu, ila Mungu ni mwaminifu, ambaye HATAWAACHA MJARIBIWE KUPITA MWEZAVYO; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.” (1 Wakorintho 10:12-13)
Je! Hili si jambo zuri kufahamu ya kuwa Mungu wetu tunayemwabudu na kumtumikia katika Kristo ni MWAMINIFU? Hili ni zuri sana! Kwa kuwa hatatuacha tujaribiwe kupita tuwezavyo, lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili tuweze kufanya nini? Ili tuweze KUSTAHIMILI! Jina la Bwana libarikiwe daima!
Tafsiri nyingine inasema “Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke. Majaribu mliyokwisha pata ni kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu. Naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.”
2.     DUMU KATIKA NENO LA KRISTO
Ili tuweze kuenenda katika upya wa maisha ndani ya Kristo tuliyempokea mioyoni, tunahitaji kulijua na kulitenda Neno lake.
Tukilikosa neno lake, tutajikuta kila mara tunafanya mambo ya zamani tuliyoyafanya tulipokuwa katika dhambi, ambayo hatupaswi kuyafanya sasa tukiwa ndani ya Kristo. Hii ni kwa kuwa tumekuwa viumbe vipya!
“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama yamekuwa mapya.” (2 Wakorintho 5:17)
Ni kweli umekuwa kiumbe kipya ukiwa NDANI ya Kristo, tamaa ya uzinzi imehama! Ndiyo maana Yesu Kristo aliomba hivi; “Uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndiyo kweli”. (Yohana 17:17)
Tunahitaji utakaso wa Neno kila wakati kwa sababu zifuatazo:-
(a)  Ili tusije tukatenda dhambi tena (Zaburi 119:9,11)
(b)  Ili lituongoze tusije tukapita gizani, kwa kuwa Neno ni taa (Zaburi 119:105)
(c)  Ili lituwezeshe kumtambua mtu mwenye mawazo mabaya ya dhambi anapoongea na sisi. (Waebrania 4:12,13)
(d)  Ili litulinde tusije tukaanguka katika mikono ya Malaya (Mithali 2:1-3,11, 16; Mithali 5:1-23; Mithali 6:20-35; Mithali 7:1-27, Mithali 23:26-28 na Mithali 30:18-20)
Naamini kabisa ya kuwa wakristo wakipata mafundisho ya kutosha ya neno la Mungu maanguko katika dhambi tunayoyasikia sasa hatutayasikia. Kwa kuwa watajifunza kuishi katika ushindi ule ambao Kristo alitushindia pale msalabani.
Lakini inasikitisha kuona ya kuwa masomo ya neno la Mungu ya kuwasimamisha wakristo kiroho hayafundishwi vya kutosha. Na hata yale yanayofundishwa yanafundishwa juu juu tu. Na tuungane pamoja basi katika kumwomba Bwana ainue walimu wengu katika Kanisa, na kwamba awape ujasiri na muda wa kutosha wa kufundisha kile alichowapa kufundisha.
3.     IKIMBIE ZINAA.
“IKIMBIENI ZINAA. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.” (1 Wakorintho 6:18)
Ni kweli ya kwamba, biblia inasema “Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani, naye atawakimbia.” (Yakobo 4:7). Lakini biblia haisemi ipingeni zinaa, bali inasema IKIMBIENI ZINAA!
Watu wengi wameanguka katika zinaa, kwa kuwa wanajaribu kupingana nayo. Mwisho wake wanazidiwa na wanazini. Kwa nini hawafuati ushauri huu wa biblia unaosema ikiembieni zinaa?
Katika kitabu cha Mwanzo 39:6-12 tunasoma habari za Yusufu jinsi alivyokabiliwa na jaribu la uzinzi, na jinsi alivyopona kwa kukimbia!
Hebu na tuisome habari hii:
“Naye Yusufu alikuwa mtu mzuri, na mwenye uso mzuri. Ikiwa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, LALA NAMI. Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyaje ubaya huu mkubwa nikamkosee Mungu? Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye. Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake. AKAKIMBIA. Akatoka nje.”
Matokeo ya Yusufu kuikimbia zinaa ni KUFUKUZWA KAZI NA KUFUNGWA JELA. Yusufu aliuliza; “Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?” Kwa kuwa hakutaka kumkosea Mungu kwa kukubali kuzini, aliamua kukimbia bila kujali kitu kitakachotokea baadaye.
Tunapata ushauri gani katika jambo hili?
Hebu soma haya kwa makini. Ni afadhali ufukuzwe kazi kuliko ukamkosea Mungu kwa kuzini na mwenye nyumba aliyekuajiri!
Ni afadhali ufungwe kuliko ukamkosea Mungu kwa kuzini na hakimu au askari polisi.
Ni afadhali utengwe kanisani, kuliko ukamkosea Mungu kwa kuzini na mchungaji au na kiongozi ye yote wa kanisa!
Ni afadhali ufukuzwe kwa ndugu yako, kuliko ukamkosea Mungu kwa kukubali kuzini naye!
Je! Unasikia ushauri huu wa Roho Mtakatifu anaotufundisha katika neno la Mungu? Je, umesikia?
Usikubaliane na zinaa; wala usipingane nayo; bali IKIMBIE ZINAA!
4.     Usimpe nafasi Ibilisi:
“…..wala usimpe Ibilisi nafasi” (Waefeso 4:27)
Biblia isingesema tusimpe Ibilisi nafasi kama tusingekuwa na uwezo wa kumpa au kutompa nafasi katika maisha yetu. Mara nyingi Ibilisi anapata nafasi ya kuingia katika maisha ya mkristo si kwa sababu amemwonea bali ni kwa sababu amepewa nafasi.
Ni kweli kwamba kuna watu wanaoonewa na Ibilisi. Lakini kwa mtu aliyezaliwa mara ya pili kwa Roho wa Mungu, amepewa mamlaka juu ya nguvu zote za Ibilisi, wala hakuna kitu kitakachomdhuru. Soma Luka 10:19.
Ndiyo maana imeandikwa “…..wala msimpe Ibilisi nafasi.”
Mambo gani yanaweza kumpa nafasi Ibilisi katika maisha yetu, hata atuangushe katika zinaa? Baadhi ya mambo hayo yanaeleza hapa:-
(a) HASIRA
Jambo mojawapo linalompa nafasi Ibilisi kuwaangusha watu katika zinaa ni hasira iliyojaa uchungu.
“Mwe na hasira, ila msitende dhambi, jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi.” (Waefeso 4:26-27)
Kuna wakati Fulani nilimuliza msichana mmoja sababu zilizomfanya azae kabla ya kuolewa; alinijibu hivi, “Wazazi wangu walinigombeza siku moja na kunisingizia kuwa nafanya umalaya, na huku nilikuwa sifanyi. Na kwa kusingiziwa hivyo pamoja na matusi niliyotukanwa nilibanwa na hasira. Na nikaamua kuanza kufanya umalaya kwa kuwa sikuona uhalali kusingiziwa kitu ambacho nilikuwa sifanyi, kwa hiyo nikaone heri nifanye ili nikisemwa; nisemwe juu ya kitu ninachofanya kweli. Na matokeo yake ni kupata mamba na kuzaa kabla ya kuolewa.”
Hali ya msichana huyu inawapata wengi. Na hata katika ndoa, chanzo kikubwa cha mume au mke kutokuwa waaminifu katika unyumba wao ni chuki na hasira iliyo kati yao. Mwingine anazini ili amkomoe mwenzake! Ole!
Hasira siyo tiketi yako ya kukufanya uzini.
“Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya, tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.” (Waefeso 4:31,32)
Ikiwa hasira inakusumbua, badala ya kumkosea Mungu kwa kuzini, jifunze kusemehe na kusahau kwa kutumia uwezo wa Kristo aliye ndani yako.
(b) MAWAZO
Mtu mmoja alikuja kwangu na kuniomba nimwombee apone ugonjwa uliokuwa unamsumbua.
Nikamuuliza; “ Ugonjwa huu ulikuanzaje?”
Akasema; “Wakati Fulani nilianguka katika zinaa, na baada ya hapo nikaanza kuumwa ugonjwa huu.”
Nikamuuliza tena; “Je! Ulitubu baada ya kuzini? Akasema; “Ndiyo nilitubu, hata nikawaomba watu waniombee nipone; wakaomba lakini sikupona.”
Nikamjibu nikasema; “Lakini naona wewe ndiye mwenye shida – hukutubu sawa sawa.
Kwa kuwa imeandikwa; “ Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; NAMI NITAKUONDOLEA UGONJWA KATI YAKO.” (Kutoka 23:25)
Akasema; “ Ni kweli nimetubu na wala sijarudi  tena kuzini, ila kinachonisumbua ni mawazo. Kila wakati nakuta nawaza juu ya yule mwanamke niliyezini naye, lakini kila ninapotaka kwenda kwake najizuia.”
Nikamwambia; “Je hujui ya kuwa unapomwazia mwanamke moyoni mwako kwa kumtamani unazini naye? Na kwa ajili hiyo unahitaji kutubu upya, na usimwazie tena kwa kumtamani.”
Watu wengi wanasumbuliwa na mawazo ya zinaa kama mtu huyu. Na wakati mwingine wanajitahidi wasiwaze lakini wanashindwa. Na wengi wa wale waliofanya zinaa kwa mwili huwa mara nyingi wamekwisha kuzini moyoni.
Usiwaze mawazo mabaya ya uzinzi, na kumpa nafasi Ibilisi! Jaza moyo wako neno la Mungu, na utawaza neno la Mungu. Je hukumbuki kuwa imeandikwa ya kuwa;
“Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya staha, yoyote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, YATAFAKARINI HAYO” (Wafilipi 4:8)
(c) MAENEO YASIYOFAA
Enyi wavulana jihadharini na ndugu zenu wa kike, na enyi wasichana jihadharini na ndugu zenu wa kiume. Soma katika 2 Samweli 13:1-39 uone jinsi mtu na dada yake walivyoanguka katika zinaa. Tafadhali uwe mwangalifu! Ibilisi anaweza kutumia hata ndugu yako mliye damu moja kukuangusha ukimpa nafasi.
Kwa wale walio katika uchumba, angalieni msimpe nafasi Ibilisi kwa kukaa wawili peke yenu katika maeneo ya siri. Na kwa kutoangalia hili, wengi wamezini kabla ya siku yao ya harusi. Tunza usafi wa matendo yako, uwe mwepesi kutofautisha kati ya kupenda na kutamani. Wachumba wanapokuwa peke yao wawili mara kwa mara, upendo wa Kristo kati yao unapoa na huwakiana tamaa inayowaongoza kuzini. Usihalalishe ndoa kabla ya siku ya harusi! Wala usimpe nafasi Ibilisi ya kuwachezea!
Pia, kwako wewe uliyeokoka, mtu wa Mungu, angalia marafiki zako walivyo. Jihadhari nao. Wengi wameanguka katika zinaa kwa sababu ya marafiki zao.
(d) MISINGI YA NDOA IHESHIMIWE:
Katika ndoa, walio wengi wameanguka katika zinaa, baada ya kutokea shida katika uhusiano wa tendo la ndoa.
Kwani maandiko yanasemaje?
Lakini kwa sababu ya ZINAA kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wke mwenyewe, mume ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe muweze haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; na vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpata faragha kwa kusal; mkajiane tena, shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.” (1 Wakorontho 7:2-5)
Madhara yanayotokea baada ya kumnyima mke wako au mume wako uhusiano wa tendo la ndoa ni makubwa. Kwa hiyo, jihadhari usimpe nafasi Ibilisi katika unyumba wako!
5.     ISHI NA ENENDA KWA ROHO:
“Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka….. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, UASHERATI, uchafu, ufisadi…… na mambo yanayofanana na hayo; katika hayo nawaambia mapema kama nilivyokwisha, ya kwamba watu watendao  mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.” (Wagalatia 5:16-21)
“Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho” (Wagalatia 5:25)
“Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili, bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kutii. Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili, bali mwaifuata roho.” (Warumi 8:5-9).












SOMO
: IKIMBIENI ZINAA
Wiki ya Nne
UFANYEJE IKIWA UMEANGUKA KATIKA DHAMBI YA ZINAA?
Ni jambo gani linatokea Mkristo anapoanguka katika dhambi ya zinaa? Ni muhimu ufahamu hili, kabla ya kujua utafanyaje ikiwa umeanguka katika dhambi ya zinaa.
Mambo matatu makubwa yanatokea mkristo anapoanguka katika zinaa;
(a)  Anaukosa Ufalme wa Mungu:
“Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, UASHERATI, Uchafu, Ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo; katika hayo NAWAAMBIA MAPEMA. Kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU.” (Wagalatia 5:9-21)
Kumbuka kuwa Mtume Paulo aliandika waraka huu kwa Wagalatia walio wakristo na siyo kwa Wagalatia ambao siyo wakristo. Waraka unaanza hivi; “Paulo, Mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu), na ndugu wote walio pamoja nami, kwa MAKANISA YA GALATIA” (1:1,2)
Yesu Kristo alisema. “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na WAZINZI, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.”(Ufunuo 22:12-15)
Soma pia kitabu cha Waefeso 5:5
(b)  Anatengwa na Wakristo wenzake.
Mtume Paulo alipokuwa akiwaandikia wakristo wa Korintho alisema hivi:
“Yakini habari imeenea kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika mataifa….. Mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo….. Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyanganyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. Lakini mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyanganyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.” (1 Wakorintho 5:1,2-11)
(c)  Nchi nzima inaadhibiwa
“Lisikieni neno la Bwana, enyi wana wa Israeli, kwa maana Bwana ana mateto nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi. Hapana neno ila kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi, na kuua na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na damu hugusana na damu. Kwa ajili hiyo NCHI ITAOMBOLEZA, na kila mtu akaaye ndani yake ATADHOOFIKA, pamoja na wanyama wa kondeni na ndege wa angani, naam, samaki wa baharini pia wataondolewa….. Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa….. Nao watakula, lakini hawatashiba; watafanya zinaa, lakini hawataongezeka, kwa sababu wameacha kumwangalia Bwana. Uzinzi na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu” (Hosea 4:1-3; 6,10,11)
Kwa sababu ya uzinzi, gharika iliangamiza watu na vitu vilivyokuwa katika nchi, alipona Nuhu na watu wachache na viumbe wachache. Kwa sababu ya zinaa, Sodoma na Gomora iliteketezwa kwa moto, wakapona Lutu na binti zake wawili.
Na kwa sababu ya zinaa siku hizi nchi zimepigwa kwa ugonjwa wa Ukimwi (AIDS). Ni kama Nabii Hosea alivyotabiri, NCHI ZINAOMBOLEZA, WATU WNADHOOFIKA, WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA YA MUNGU, NA WANAPOTELEWA NA FAHAMU!
Ndiyo maana ni muhimu ufahamu ufanye nini ikiwa umeanguka katika zinaa. Si mapenzi ya Mungu uangamie, usiurithi ufalme wake, wakristo wakutenge na kuiangamiza nchi, bali mapenzi yake ni watu wote waifikie toba ya kweli, waokolewe, waziache njia zao mbaya, na wamgeukie na kumfuata daima!
Kwa hiyo kama umeanguka katika zinaa, sikiliza ushauri ufuatao:
(i)               Usiifiche dhambi:
Najua unaweza kuwaficha wanadamu wasijue umezini,lakini unaweza kwenda wapi utakakojificha Mungu asikuone? Soma Zaburi ya 139:7-13. Na imeandikwa:-
“Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.” (Mithali 28:13)
Ukifuatilia habari za Mfalme Daudi, utaona ya kuwa kitu alichokifanya baada ya kuanguka katika zinaa na mke wa mtu, ni kujitahidi kutafuta namna ya kuifunika hiyo dhambi, lakini alishindwa. Na mwisho wake aliamua kutafuta mbinu ya kumuua Uria, ambaye mke wake ndiye aliyezini na Mfalme Daudi. Unaweza ukaona ya kuwa ni kweli kwamba uzinzi huondoa ufahamu za mtu. Kwa nini Mfalme Daudi aliamua kuua ili alifiche kosa alilofanya?
Je! Alidhani Mungu naye hajamwona? Mungu aliinua mtu wake, ambaye alikwenda kwa Mfalme Daudi na kumweleza jinsi Mungu alivyochukizwa na kitendo hicho. Daudi alipojua dhambi iko wazi mbele za Mungu alitubu!
“Bwana asema hivi, Angalia, nitakuondoshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili. Maana wewe ulifanya jambo hili mbele ya Israeli wote na mbele ya jua. Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia Bwana dhambi. Nathani akamwambia Daudi, Bwana naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa. LAKINI, KWA KUWA KWA TENDO HILI UMEWAPA ADUI ZA BWANA NAFASI KUBWA YA KUKUFURU, motto atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa.” (2 Samweli 12:11-14)
Ni kweli kwamba unaweza ukafanya uzinzi kwa siri, Mke wako asijue, au mume wako asijue, au wazazi wako na ndugu zako wasijue, au waliookoka wenzako wasijue, Lakini, FAHAMU HAKIKA YA KUWA MUNGU AMEKUONA.
Na mshahara wa dhambi ni mauti, kwa hiyo kama unataka kudumu katika uzima uliopewa na Kristo, usijaribu kuificha dhambi.
(ii)             Tubu, Tengeneza na Usirudie tena.
Ikiwa umeanguka katika dhambi ya uzinzi, njia iliyo wazi ni wewe kutubu kwa Mungu katika Roho na Kweli,halafu tengeneza (tubu) kwa wale uliowakosea na usirudie tena; na mwisho songa mbele katika wokovu aliokupa Bwana.
Kuna mtu mmoja aliniambia nimsaidie katika kumwombea kwa kuwa kuna wakati alianguka katika zinaa, na baadaye akatubu. Lakini kila wakati yalikuwa yanamjia mawazo ya kuhukumu ya kuwa alizini na kwa hiyo anajiona hafai tena hata kuomba wala kuendelea na wokovu. Ingawa alitubu bado alishitakiwa sana moyoni na kosa alilolifanya. Aliona kama vile Mungu hajamsamehe.
Inawezekana na wewe ukasumbuliwa na  hali ya namna hii. Nafahamu ya kuwa wanadamu ni wagumu kusamehe na kusahau,hata kama wanajua umekwisha tubu na kutengeneza.
Lakini nataka nikuambie hivi, usiupime msamaha anaokupa Mungu unapotubu kwa kuangalia na kusikiliza wanadamu wanasemaje juu yako; bali angalia neno lake katika biblia linasemaje. Imeandikwa hivi;
“Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi anaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zenu, wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote” (1 Yohana 2:1,2)
Tena imeandikwa hivi;
“Tukiziungama dhambi zetu, Yesu ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” (1 Yohana 1:9)
Tena imeandikwa hivi;
“Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundi sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundi kama bendera, zitakuwa kama sufu.” (Isaya 1:8)
Tena imeandikwa hivi;
“Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao zitazikumbuka tena”. (Waebrania 8:12)
Kama ukitubu katika Roho na Kweli, Bwana ameahidi kusamehe na atakusamehe. Na yeye akisamehe, anafuta kosa lako na kulisahau. Sasa kama Mungu amesamehe na kusahau, shetani au mwanadamu anapata wapi – haki ya kukunyoshea kidole cha hukumu? Soma Warumi 8:31-39.
Neno la Mungu ndilo linalokupa uhakika na namna ya kupokea msamaha. Baada ya kutubu na kutengeneza, simama upya ndani ya Kristo, na songa mbele kiroho, na katika kumtumikia Bwana. Kwa kuwa “Katika mambo hayo yote tunashinda na zaidi ya kushinda, kwa yeye (Kristo) aliyetupenda. (Warumi 8:37)
(iii)           Kemea roho ya Uzinzi.
Uzinzi ni roho. Bwana anasema hivi katika kitabu cha Hosea 4:11,12; “Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu. Watu wangu hutaka shauri kwa gongo lao, na fimbo yao huwahubiri mambo; maana Roho ya UZINZI imewakosesha, nao wamekwenda kuzini mbali na Mungu wao”.
Baada ya kutubu na kutengeneza, ikiwa bado utaona unasumbuliwa na tamaa ya kuzini ujue unasumbuliwa na roho ya uzinzi. Kwa hiyo tumia JINA LA YESU KRISTO ulilopewa, na ikemee roho hiyo nayo itaondoka na kukuacha.         










Sura ya Kwanza
KWA NINI SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASKINI?
         Napenda kuanza kukuambia ya kuwa si mapenzi ya Mungu uwe maskini. Kwa sababu tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu huu, Mungu hakupanga kuwa watu wake aliowaumba wawe maskini; bila kujali rangi, kabila, wala taifa.
       Nafahamu ya kuwa katika Mathayo 5:3, Yesu Kristo alisema; “Heri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao.” Watu wengi wanapousoma mstari huu, wanadhani Yesu Kristo alisema “Heri walio maskini wa mahitaji ya MWILI; maana ufalme wa mbinguni ni wao.” Lakini Kristo hakusema hivyo.
        Mtu maskini maana yake ni mtu mhitaji. Yesu Kristo aliposema “Heri walio maskini wa roho …….” Alikuwa ana maana ya kusema ‘Heri walio wahitaji wa mambo ya rohoni; maana ufalme wa mbinguni ni wao. Ndiyo maana aliongeza kusema, “Heri wenye njaa na kiu ya haki; maana hao watashibishwa" (Mathayo 5:6).
         Mtu aliye maskini wa mambo ya mwili ni yule aliye mhitaji wa mambo ya mwili. Na mambo ya mwilini ninayoyasema ni mavazi, chakula na mahali pa kulala. Yesu Kristo hakusema heri wale walio na mahitaji ya chakula, mavazi, afya na malazi.
        Ninaposema mahitaji ya mwili usije ukachanganya na matendo ya mwili yaliyoandikwa katika Wagalatia 5:19-21 ambayo ni uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda na ulevi. Mimi siyazungumzii hayo ninaposema juu ya mahitaji ya mwili. Mahitaji ya mwili ninayoyasema ni mavazi, chakula, nyumba na matibabu.
       Kwa hiyo si sawa kabisa kwa mtu kuhalalisha umaskini wa mwili, yaani ukosefu wa chakula, mavazi, matibabu na nyumba, kwa kutumia maneno ya Bwana Yesu Kristo yaliyo katika Mathayo 5:3:
Nataka kurudia tena; si mapenzi ya Mungu mtu awe maskini.
       Unaweza ukaniuliza na kusema, “Bwana Mwakasege kama si mapenzi ya Mungu mtu awe maskini, mbona basi kuna matajiri na maskini, je! Mungu hakuwaumba wote?
        Ni kweli kwani hata imeandikwa katika Mithali 22:2, kuwa “Tajiri na maskini hukutana pamoja; Bwana ndiye aliyewaumba wote”. Lakini fahamu ya kuwa ingawa matajiri na maskini waliopo wote waliumbwa na Mungu; tangu mwanzo wa uumbaji Mungu hakuyaweka matabaka haya mawili.
        Hapo mwanzo Mungu alipomuumba mtu, hakuweka ndani yake utajiri na umaskini pamoja. Wala hakuumba watu wengine wawe matajiri na wengine wawe maskini.
         Tunafahamu ya kuwa mtu aliumbwa kwa mfano wa Mungu na kwa sura ya Mungu. Na naamini ya kuwa utakubaliana nami nikisema Mungu wetu si maskini kwa hiyo hatukuumbwa kwa mfano wa kimaskini wala sura ya kimaskini.
              Kwa nini nasema na kusisitiza ya kuwa si mapenzi ya Mungu tuwe maskini?
 Ninazo sababu nne ambazo ningependa kukushirikisha:
  1. Mungu ndiye atupaye nguvu za kupata utajiri
“ Bali utamkumbuka Bwana , Mungu wako, maana ndiye akupaye NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo” (Kumb. 8:18).
          Si mapenzi ya Mungu tuwe maskini kwa kuwa yeye mwenyewe ndiye atupaye nguvu ili tupate utajiri! Kama basi Mungu anatupa nguvu za kupata utajiri, ina maana ni wazi kwamba Mungu hapendi tuwe maskini wa mambo ya mwilini.
         Lakini fahamu ya kuwa si matajiri wote waliopo duniani wameupata utajiri kutokana na nguvu walizopewa na Mungu. Wengi wamepata utajiri kwa njia ya dhuluma. Na ndiyo maana sehemu nyingi katika Biblia matajiri wa jinsi hiyo wamekemewa. Soma Amosi 5:11, 12. Kwa sababu hii Mungu hayuko upande wa matajiri hawa. Hii pia haimaanishi kuwa Mungu yuko upande wa KILA  maskini aliopo duniani. La hasha! Mungu yuko upande wa yule ayafanyaye mapenzi yake awe tajiri au maskini (Mathayo 7:21)
        Watu wengi wametajirika kwa njia ya rushwa na kutokusimamia haki pamoja na uchoyo. Na hii si sawa hata mbele za Mungu. Ni dhambi zilizo wazi kabisa. Na wote wafanyayo hayo wanahitaji kutubu!
        Ngoja nikueleze jambo muhimu: Mungu anapokupa nguvu za kupata utajiri, anakupa akiwa na lengo na kusudi muhimu.
              Ni lengo gani hilo?
            Imeandikwa, “………. Ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo”
       Na Yesu Kristo alisema, “ ……. Kikombe hiki ni AGANO JIPYA KATIKA DAMU YANGU, inayomwagika  kwa ajili yenu” (Luka 22:20).
          Mungu akikupa nguvu za kupata utajiri ni kwa ajili ya kulifanya imara agano lake katika damu ya Yesu Kristo. Na hii ina maana utajiri utakaokuwa nao kutoka kwa Mungu ni kwa kueneza injili! Ni kwa ajili ya kueneza habari njema ya ukombozi kutokana na dhambi, mauti, magonjwa na umaskini. Habari njema hii inatakiwa kuenezwa kwa maneno na kwa matendo.
        Kwa kuwa tu kuna matajiri wasio wa haki basi haimaanishi kuwa matajiri wa haki hawapo. Ni budi tuweze kutofautisha utajiri ulio wa haki na utajiri usio wa haki.
  1. Mungu ndiye atufundishaye kupata faida
Mungu wetu tunayemwabudu na kumtumikia katika Kristo Yesu si Mungu wa hasara bali Mungu wa faida. Imeandikwa hivi;
  “ Bwana, Mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi;Mimi ni Bwana, Mungu wako,   nikufundishaye  ili upate faida, nikuongozaye katika njia  ikupasayo kuifuata” (Isaya 48:17).
           Ndiyo maana kila mtu ndani yake ameumbiwa kupenda kufundishwa ili apate faida katika mambo anayoyafanya. Mungu akikufundisha kupata faida; njia utakayotumia kupata faida itakuwa njia ya haki. Na faida hiyo haitakuwa kwa ajili yako mwenyewe, bali utawashirikisha na wengine pia faida hiyo .
          Watu wengine kwa kutokuwa wavumilivu, na kutokujali mafundisho ya Mungu; wameamua kujipatia faida kwa kuwadhulumu, kuwakandamiza na kuwanyonya wengine. Na inasikitisha jinsi wanavyomshirikisha Mungu katika faida najisi namna hiyo waposema ya kuwa ni Mungu aliyewasaidia ‘kudhulumu na kunyonya’. Ni wazi ya kuwa Mungu hakuwasaidia kupata faida kwa njia ya udhalimu.

        Si mapenzi ya Mungu tuwe maskini, ndiyo maana anatufundisha ili tupate faida ya halali. Kwa ajili hiyo imeandikwa; “Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji” (Waefeso 4:28).
        Je! Si jambo la kushukuru hili, la kuwa na Mungu ambaye hapendi tupate hasara?
       Kama Mungu asingekuwa anapenda tufanikiwe katika mahitaji yetu ya mwili, basi ingeandikwa wazi katika Biblia. Lakini badala yake naona maneno kama yafuatavyo; “Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo YOTE na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo” (3Yohana 1:2).
       Kwa maneno mengine anatuombea ya kuwa kwa kadri roho inavyofanikiwa basi tufanikiwe vivyo hivyo katika mahitaji ya mwili – yaani tuwe na chakula, mavazi, n.k.
  1. Vitu vyote vyema ni mali ya Bwana, na vyote vya Bwana ni vyetu ndani ya Kristo
              Katika Zaburi 24:1 imeandikwa;“Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana; Dunia na wote wakaao ndani yake”
            Na pia ukisoma katika Hagai 2:8 unaona imeandikwa hivi “Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi”
             Ngoja nikuulize swali; Je! unadhani vitu vyote hivi Bwana amemwekea nani? Unadhani alimwekea shetani na watu wanyonyaji wachache?
La hasha!
        Mungu aliviweka vitu hvi vyote na mali hii yote kwa ajili ya watu wake wote, ili itumike katika usawa. Kwa nini? Kwa kuwa Mungu hapendi watu wake wawe maskini. Ndiyo maana mtu alipoumbwa aliwekwa awe wakili wa mali yote ya Mungu hapa duniani.

        Utajiri uliomo duniani umetawaliwa na watu wachache na nchi chache siku hizi kwa sababu ya dhambi za uchoyo, ubinafsi, uonevu,unyonyaji, unyang’anyi na dhuluma zilizoingia ndani ya mwanadamu.

       Na hii imefanya watu wengine kufikiri ya kuwa Mungu ndiye aliyegawa matabaka haya mawili, ambavyo si kweli. Na si vizuri kumsingizia Mungu katika jambo ambalo mwanadamu mwenyewe amejiletea uharibufu.
  1. Yesu Kristo alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri
              “ Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi   alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake” (2 Wakorintho 8:9).          
            Je! unafahamu kwa nini Yesu Kristo aliamua kuwa maskini? Ni “…….. ili kwamba ninyi mpate kuwa MATAJIRI kwa umaskini wake”.
           Najua kuna wengine watashangaa kuusoma mstari huu; lakini ndivyo ilivyo.
          Nimewahi kusikia mkristo mmoja akisema: “ Mimi ni maskini kwa kuwa Yesu Kristo alikuwa maskini”.
          Na mwingine alisema; “ Napenda kuwa maskini kwa kuwa Yesu Kristo alikuwa maskini”.
         Nadhani kuwa kuna wakristo wengi ambao wana mawazo kama haya. Ni kweli kwamba Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani alikuwa maskini. Lakini hakuwa maskini ili sisi tuwe maskini; bali alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri! Kama alikuwa maskini ili sisi tuwe maskini kama wengine wanavyodhani, basi kazi hiyo haina faida kwetu. Lakini Yesu Kristo asifiwe kwa kuwa alikuwa maskini ili sisi tuwe MATAJIRI.
        Na ndiyo maana alisema katika Luka 4:18a ya kuwa; “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri MASKINI habari njema.”
        Je! kuna habari njema kwa maskini zaidi ya kumwondoa katika umaskini wake?
       Injili ni habari njema. Na injili ni uweza wa Mungu uuletao wokovu kwa kila aaminiye (Warumi 1:16). Kuokoka si kuenda tu mbinguni; bali kuokoka maana yake ni uokolewe usiende motoni bali uende mbinguni ukifa, PAMOJA na kuokolewa kutoka kwenye  matatizo ukiwa hapa duniani ambayo ni pamoja na umaskini.
       Petro aliposema “Bwana niokoe” alipokuwa anazama katika maji unafikiri alikuwa anataka wakati huo aokoke aende mbinguni? La hasha! Yeye Petro alitaka aokoke ASIZAME KATIKA MAJI. Na Yesu akasikia kilio chake akamwokoa. Hivi leo kuna watu wengi mijini na vijijini wanalia Yesu awaokoe kutokana na njaa, kukosa mavazi, magonjwa, maonezi, nakadhalika. Kanisa kama mwili wa Kristo linatakiwa kuwa mstari wa mbele kuwasaidia watu hao, kwa kuwa kazi hii ni sehemu ya utume wake.

       Wakristo wengine utawasikia wakisema; hapa duniani hawahitaji kitu bali thawabu yao wataipata mbinguni. Lakini matamshi ya namna hii yanaeleza ukweli nusu na usiokamilika. Kuwa mkristo kuna thawabu duniani na kuna thawabu mbinguni.

       Kama hakuna thawabu yoyote tunayoipata tukiwa hapa duniani kwa kumfuata Yesu Kristo; basi ukristo wetu hauna maana na hauna msaada wowote kwa mwanadamu. Ukristo usiotatua matatizo ya mwanadamu ya kila siku, ni ukristo usio na uhai.
        Mtume Petro naye aliwahi kusumbuliwa sana na jambo hili, hata ikabidi amuulize Bwana Yesu.
        “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata, TUTAPATA NINI BASI?” (Mathayo 19:27)
          “Yesu akasema, Amini, nawaambiaeni, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa MARA MIA SASA WAKATI HUU, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele” (Marko 10:29,30).
          Majibu haya ya Bwana Yesu, yanazidi kutudhihirishia ya kwamba si mapenzi ya Mungu tuwe maskini. Yesu Kristo ameeleza wazi kabisa ya kuwa atakayemwamini na kufuata maagizo hayo atapata MARA MIA SASA WAKATI HUU akiwa bado duniani. Na kati ya vitu atakavyopewa ni pamoja na nyumba na mashamba!
          Ni kweli Bwana Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani alikuwa maskini, lakini baada ya kufufuka alirudishiwa utajiri wake. Ndiyo maana Mtume Paulo anazungumzia juu ya “….. utajiri wake Kristo usiopimika”. (Waefeso 3:8). Na katika Wafilipi 4:19 tunasoma hivi; “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu”.
          Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alichukua dhambi zetu na magonjwa yetu , na kwa kupigwa kwake sisi tumepona (Isaya 53:5; Mathayo 8:16,17; 1Petro 2:24). Na kwa kujua hili kanisa linajihusisha na kuombea wagonjwa na kutoa huduma za afya kwa wagonjwa.
        Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alichukua dhambi zetu na akafanyika dhambi kwa ajili yetu, “ Ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye” (2Wakorintho 5:21). Na kwa kujua hili kanisa linahubiri habari za ondoleo la dhambi kwa yeyote atakayemwamini Kristo.

        Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alikuwa maskini, ingawa alikuwa tajiri, ili kwa umaskini wake sisi tupate kuwa matajiri (2 Wakorintho 8:9). Na kwa kujua hili kanisa linajihusisha na miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili mtu aondokane na umaskini.












                                                               Sura ya Pili

MAMBO MANNE UNAYOPASWA KUYAJUA

            Kuna mafundisho ambayo si sahihi yaliyowafanya wakristo wengi hasa wale waliookoka kutokujua cha kuamini juu ya uhusiano wa ukristo wao na utajiri. Na tuangalie maeneo manne yafuatayo ambayo wakati mwingine yamezaa mafundisho yasiyo sahihi:

  1. TAJIRI NA UFALME WA MUNGU:
            Nadhani utakuwa umewahi kusikia watu wakisema; “Matajiri hawataurithi ufalme wa Mungu” Na wanasema ndivyo Bwana Yesu alivyosema baada ya tajiri aliyetaka uzima wa milele kukataa kuuza mali yake.
            Hata mimi mwanzoni ilikuwa karibu sana nikubaliane na usemi huu. Lakini baada ya kuyachunguza maandiko niliona ya kuwa Yesu Kristo hakusema hivyo bali anasingiziwa tu.
            Yesu Kristo alisema hivi;Kwa shida gani wenye mali WATAUINGIA ufalme wa Mungu” (Luka 18:24)
Kwa mstari huu tunajua ya kuwa Yesu Kristo hakusema ya kuwa wenye mali hawatauingia ufalme wa Mungu; bali alisema “kwa shida gani wenye mali watauingia ufalme wa Mungu!”

            Na akaendelea kusema, “ Kwa maana ni vyepesi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.” (Luka 18:25). Na wale waliosikia wakashtuka na kushangaa, kwa maana waliona itakuwa vigumu sana kwa tajiri kuokoka, na naona walifikia mawazo kama waliyonayo wengi siku hizi ya kuwa tajiri hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu. Ndiyo maana wakauliza “Ni nani basi awezaye kuokoka?” (Luka 18:26).
Yesu Kristo akawajibu akasema;“Yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa Mungu” (Luka 18:26).
Kwa maneno mengine alikuwa anasema tajiri anaweza KUWEZESHWA NA MUNGU kuingia katika ufalme wa Mungu akiiamini injili inayookoa. Hata hivyo maskini naye anaokolewa kwa neema ya Mungu.
Na kwa kuamini kuwa tajiri hawezi kuurithi ufalme wa Mungu, wakristo wengi kwa kudhamiria kabisa wameamua kuwa maskini ili wasije wakaukosa ufalme wa Mungu. Lakini hii si sawa na ni kukwepa wajibu wetu tulionao kama mawakili wa mali zote za Mungu.

            Na ni vizuri ufahamu ya kuwa umaskini wa kukosa chakula, mavazi na nyumba ya kukaa siyo tiketi ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Na wala umaskini siyo utakatifu – ingawa kuna maskini walio watakatifu! Na pia utajiri siyo utakatifu ingawa kuna matajiri walio watakatifu.

            Kuna Mkristo mmoja wa dhehebu fulani alikuwa akinieleza hali iliyowasonga katika dhehebu lao; alisema;
“Katika kanisa letu Mchungaji akionekana amevaa vizuri,   wakristo wake wanasema amepoa kiroho. Kwao mtu wa kiroho  ni mtu aliye maskini, asiyevaa nguo nzuri wala viatu vizuri.”
Niliposikia maneno hayo nilisikitika sana, na nikakumbuka maneno ya Mungu aliyosema kwa kutumia kinywa cha nabii Hosea, yasemayo, “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa ….” (Hosea 4:6) na pia Yesu Kristo  aliwahi kusema ya kuwa watu wanapotea kwa kuwa hawajui maandiko wala uwezo wa Mungu.
Kwa hiyo fungua moyo wako uisikie kweli ambayo ndiyo neno la Mungu. Na utaifahamu kweli na hiyo kweli itakuweka huru (Yohana 8:32)
  1. MUNGU NA MALI
            Kuna uhusiano gani kati ya Mungu na Mali? Kuna uhusiano gani kati ya Mkristo na Mali? Kuna uhusiano gani kati ya wokovu na mali?
Je, ni dhambi kwa mkristo kuwa na mali nyingi? Hebu na tuangalie maneno ya Yesu Kristo juu ya Mungu na Mali.
            “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili, Kwa maana  atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu  na Mali” (Mathayo 6:24)
Neno la kiingereza lililotafsiriwa na kuandikwa ‘mali’ ni ‘mammon’ Na neno hili ‘mommon’ ni jina la roho ya ibilisi inayotawala mali. Kwa maneno mengine naweza kusema kuwa ‘mammon’ ni jina la pepo.

            Kwa hiyo, neno ‘mali’ lilivyotumika hapa linamaanisha ‘pepo linaloitwa Mali’ Ndiyo maana Yesu Kristo alisema; “Hakuna  mtu awezaye kutumikia MABWANA wawili ….” Yesu Kristo asingeliita mali kuwa ni mojawapo ya MABWANA kama hakuwa anasema juu ya roho inayoitwa mali. Roho hii ya shetani iitwayo Mali imewafanya watu wengi, hata wakristo waache kumtumikia Mungu aliye hai, na badala yake waitumikie roho inayowasukuma na kuwatamanisha juu ya mali, ili waitumie kwa uchoyo na ubinafsi.
            Wakristo wengine wanadhani wanaweza kumtumikia Mungu na vile vile wamtumikie Mali. Yesu Kristo alisema; “HAKUNA mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana ATAMCHUKIA HUYU, NA KUMPENDA HUYU: AMA ATASHIKAMANA NA HUYU, NA KUMDHARAU HUYU. Hamwezi kumtumikia Mungu na Mali.”
Kwa kusema hivi hakuwa anamaanisha kuwa na vitu vinavyoitwa mali ni vibaya. Kitu anachosema ni kibaya ni KUITUMIKIA MALI! Biblia inasema katika Zaburi 24:1 kuwa, “Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana; Dunia na wate wakaao ndani yake.”
Mtu hakuumbwa ili kuitumikia mali. Mtu aliumbwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu na amtumikie Yeye peke yake. Mali ya dunia iliwekwa kwa ajili ya kumtumikia mtu, na siyo mtu kuitumikia mali! Mtu aliwekwa juu ya mali yote na aliagizwa kuitawala (Mwanzo 1:28 – 30).
Kuwa na mali siyo vibaya, wala siyo dhambi. Mali inakuwa kikwazo katika maisha ya ukristo inapoanza kumfanya mtu amsahau Mungu na mapenzi yake. Ndiyo maana Yesu Kristo alisema; “Kwa shida gani wenye mali watauingia ufalme wa Mungu” (Luka 18:24) siyo kwamba hawezi kuuingia ufalme wa Mungu, bali kwa shida wenye mali watauingia ufalme wa Mungu. Kwa maneno mengine ni kwamba wakimtanguliza na kumtumikia Mungu, mali haitakuwa kwazo katika maisha yao ya ukristo.
Sasa tuishije katika ushauri wa namna hii?
            “Kwa sababu hiyo  nawaambieni, msisumbukie maisha   yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? NI YUPI KWENU AMBAYE AKIJISUMBUA AWEZA KUJIONGEZA KIMO CHAKE HATA MKONO MMOJA? Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini  maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti; nami nawaambia ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, JE! HATAZIDI SANA KUWAVIKA NINYI, ENYI WA IMANI HABA? Msisumbuke basi, mkisema, Tule nini? au Tunywe nini? au Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote” (Mathayo 6:25 – 32)
            Kuna wakristo wengine wameyaelewa vibaya maneno haya ya Bwana Yesu Kristo hata kufikia kutokufanya kazi kwa kisingizio cha kwamba Yesu Kristo alisema tusiyasumbukie maisha. Kwao kufanya kazi ina maana kusumbukia maisha. Lakini napenda kukuambia ya kuwa Yesu Kristo hakuwa ana maana ya kutuambia tusifanye kazi aliposema tusiyasumbukie maisha.
Nadhani unaamini ya kuwa ni Roho wa Kristo aliyemwongoza Mtume Paulo kuwaandikia Wathesalonike juu ya mashauri mbali mbali ya kikristo. Katika 1Wathesalonike 3:10b anasema, “Ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.” Ni muhimu kufanya kazi. Kufanya kazi siyo kusumbuka na maisha. Kusumbuka na maisha siyo kufanya kazi.
Jambo ambalo Bwana Yesu Kristo alitaka tufahamu wakati alipokuwa akisema tusisumbukie maisha, ni kwamba katika kila jambo tumshirikishe Mungu na kumtanguliza Yeye. Wakristo wengine wanadhani wanaweza kula, kunywa na kuvaa bila msaada wa Mungu. Yesu Kristo alisema katika Yohana 15:5b kuwa; “…… maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya NENO LO LOTE” (Hili ni pamoja na kula, kunywa na kuvaa) Ndiyo maana katika Wafilipi 4:13 imeandikwa kuwa “Nayaweza mambo yote katika YEYE anitiaye nguvu” Yesu Kristo ndiye atutuaye nguvu.
Yesu Kristo alitoa mwongozo mzuri sana wa jinsi ya kuishi hapa ulimwenguni aliposema;

“Bali utafuteni KWANZA ufalme wake, na haki yake; na hayo  yote  mtazidishiwa” (Mathayo 6:33)

Ukiyaangalia maisha ya watu wengi waliookoka utadhani Yesu Kristo alisema, “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote MTAONDOLEWA.” Inahuzunisha kuona ya kuwa watu wengi wakiokoka maisha yao yanageuka kuwa duni, wanashindwa kula vizuri, wala kuvaa vizuri.
            Ngoja nirudie kusema kuwa SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASKINI. SI MAPENZI YA MUNGU TUKOSE CHAKULA WALA MAVAZI. Ni Mungu yupi ambaye atawapenda ndege akawavika na kuwalisha, na akawaacha watoto wake aliowaumba kwa mfano wake wakose chakula na mavazi?
            Mungu wetu tunayemwabudu na kumtumikia katika Kristo Yesu, anapenda tuishi maisha mazuri, tule, tunywe na kuvaa vizuri. Tunachotakiwa kufanya ni kuutafuta KWANZA ufalme wake, na haki yake, na hayo yote (chakula na mavazi) TUTAZIDISHIWA na siyo TUTAONDOLEWA.
    Ukiona mtu anasema ameokoka na halafu anajikuta anakosa chakula na mavazi huku anafanya kazi, basi ujue anafanya kazi na kukusanya vitu hivyo pasipo Bwana; kwa kuwa asiyekusanya pamoja na Bwana hutapanya.
  1. FEDHA NA KUPENDA FEDHA
            Nimewahi kumsikia mhubiri mmoja akisema; “Fedha ni shina la maovu, kwa hiyo wakristo wajihadhari nazo.” Na wakristo wengi wamekuwa wakisikika wakisema hivyo, kwa hiyo wanaogopa kuwa na fedha za kutosha.
Lakini ninaposikia watu wakisema hivi, huwa najiuliza wanaupata wapi usemi huu? Biblia haisemi; “Fedha ni shina la maovu.”
Badala yake Biblia inasema hivi;“ Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha;ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi”(1Timotheo 6:10)
Kupenda fedha ni kuwa na tamaa ya fedha; ni kuzitamani fedha. Na kupenda fedha huku ndiko shina moja la mabaya ya kila namna.
Kuwa na fedha nyingi au kidogo siyo dhambi, kwa kuwa fedha ni mali ya Mungu (Hagai 2:8) Lakini kupenda fedha nyingi au kidogo ni shina moja la maovu.
Tamaa ya fedha ndiyo inayoleta wizi, ujambazi, mauaji, dhuluma, kutokutosheka, uchoyo, wivu, uasherati; nakadhalika. Lakini unaweza kuwa na fedha bila ya kufungwa na roho ya kupenda fedha.
Je! Unafahamu ni kwa nini shetani hapendi wakristo safi wawe na fedha? Maana ni kazi ya shetani kuwapiga vita wakristo wanaotaka kujipatia fedha kwa njia ya halali. Akishindwa kuwazuia kupata fedha; atahakikisha zile fedha walizonazo wanazimaliza haraka hata kwa matumizi ambayo hawakupanga.
Je! Unafahamu ni kwa nini?
Kwa sababu anafahamu mkristo safi akiwa na fedha za kutosha, atazitumia hizo kumpiga nazo vita kwa kuihubiri injili! Na shetani anafahamu kuwa Yesu alisema mwisho hautakuja mpaka injili ihubiriwe katika mataifa yote. Kwa hiyo anajua akiweza kuwakosesha wakristo fedha za kutosha ili injili ihubiriwe, yeye anapata muda wa kupumua na kupumzika.
Wengi wameshindwa kujenga makanisa kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Watumishi wa kanisa wanalipwa mishahara kidogo, kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Mikutano ya injili na semina za neno la Mungu hazifanyiki mara kwa mara kwa kukosa fedha. Wainjilisti wanatafuta fedha za kununulia vipaza sauti wanakosa. Na matokeo yake ni kazi ya Mungu kupoa.
Je! Unadhani ni nani ambaye anaweza kutoa fedha yake ili ikahubiri injili kama siyo wakristo wenyewe? Na wakristo watatoaje fedha kama hawana fedha? Na watakuwaje na fedha, kama wanadhani kuwa na fedha nyingi ni dhambi?
Na shetani ameutumia mwanya huu kuzitumia fedha ambazo wanazo watu wasiopenda haki kueneza dhambi na uovu. Je, ni haki kwa nchi nyingine kutumia ma-billioni ya fedha kutengeza silaha ambazo baadaye wanaziharibu tena, huku mamillioni ya watu wanakufa kwa njaa na maafa mengine?
        Kwa hiyo usikubali unaposikia mtu akisema kuwa na fedha ni vibaya; lakini uwe mtu wa kutokupenda fedha. Kwa kuwa ukizitamani fedha utajikuta unaanza kuzitafuta hata kwa njia ambazo ni kinyume cha maadili yetu ya Kikristo; na pia kinyume cha utu wa mwanadamu.
  1. MASKINI NA TAJIRI
            Nafahamu ya kuwa si mpango wa Mungu kwa mtu aliye tajiri kumtawala maskini kwa sababu ya umaskini wake. Na pia nafahamu si mpango wa Mungu kwa nchi zilizo tajiri kuzitawala nchi maskini kwa sababu ya umaskini wake.
    Lakini ni vizuri tufahamu uhusiano uliopo kati ya matabaka haya mawili:-
    Biblia inasema;“Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake  akopeshaye.” (Mithali 22:7)
Maneno haya ni kweli kabisa, na mtu ye yote ambaye ni msomaji wa historia na magazeti, anafahamu majadiliano ya muda mrefu yaliyopo kati ya nchi tajiri na nchi maskini duniani.
Ukoloni mbaya uliopo sasa hivi kati ya nchi na nchi, ni ukoloni wa kiuchumi. Katika ukoloni huu wa kiuchumi nchi tajiri zinatumia utajiri wake katika kuzikandamiza nchi maskini. Na kwa njia hii mamillioni ya watu wamo katika hali mbaya sana kimaisha.
Na njia kuu ambayo nchi hizi tajiri zinatumia kuzitawala nchi maskini ni kwa njia ya kuzipa mikopo. Na nchi maskini zote zimejikuta zimeingia katika utummwa mbaya kwa sababu ya mikopo ambayo haijajulikana kama inaweza kulipwa yote.
Inakisiwa ya kuwa jumla ya madeni yote ya nchi zinazoendelea ni mabilioni ya dola za Kimarekani na yanazidi kuongezeka.
Ni kweli kabisa kwamba utajiri huu wa nchi hizo si wote uliopatikana kwa njia ya halali. Na wafuatiliaji wa mambo ya uchumi duniani, wanafahamu jinsi nchi hizi zilizoendelea zinavyobuni mbinu mbalimbali kuzinyonya nchi zinazoendelea.
Ingawa si mapenzi ya Mungu tuwe maskini, lakini pia si mapenzi ya Mungu tuwe matajiri ili kuwatawala wengine kwa sababu ya umaskini wao. Ole ni kwa matajiri wanaoutumia utajiri wao kuonea na kuwafanya wenzao kuwa watumwa.
Mungu anapotupa nguvu za kupata utajiri ndani ya Kristo ni kwa kusudi muhimu la kuimarisha agano lake la kumhudumia mtu mzima – kiroho na kimwili.
            Ni kweli maskini ana shida, maana hata biblia inasema maneno yake hayasikilizwi (Mhubiri 9:16). Na hii imejionyesha wazi sana katika maoni na malalamiko ya nchi maskini ambayo yanapuuzwa na kutosikilizwa na nchi tajiri.
            Lakini hali hii si kwa nchi tu, bali hata katikati yetu humu humu makanisani. Sehemu nyingi kuna wakristo ambao ni matajiri, na mara kwa mara huwa wanatumia utajiri wao katika kuwatawala viongozi wa kanisa; na hata wakati mwingine kudiriki hata kutaka kubadilisha maamuzi ya vikao vya kanisa.
            Na kwa upande mwingine viongozi wa sharika wanajikuta wameingiwa na hofu na kushindwa kuwakemea matajiri hao wakati wanapokwenda kinyume na maadili ya kikristo. Kama siyo ukoloni wa namna yake ulioingia katika kanisa ni nini basi?
            Naamini ya kuwa wachungaji na viongozi, wengi wao wangekuwa na hali nzuri kiuchumi, baadhi ya matajiri wanaotaka kutawala viongozi wengine wangeshindwa katika mbinu zao. Au wewe unasemaje?
            Shetani amekuwa akijitahidi sana kuwakandamiza wakristo wasiwe matajiri kwa kutumia njia mbali mbali kwa kutegemea mazingira yalivyo. Mahali pengine ametumia mifumo na vyombo vya fedha kama mabenki; pengine ametumia serikali, pengine ametumia mafundisho mabaya kwa wakristo, nakadhalika.
Na shabaha yake ya kufanya hivyo ni:-
(a)               Maneno ya wakristo yasisikilizwe wanapohubiri, kwa kuwa imeaandikwa; “….Walakini hekima ya maskini hudharauliwa wala maneno yake hayasikilizwi” (Mhubiri 9:19b). Kwa lugha nyingine maana yake “hayatiliwi maanani.”
(b)               Wakristo waendelee kuwa watumwa ingawa wanadai ya kuwa wamewekwa huru. Kumbuka imeandikwa hivi; “Tajiri humtawala maskini. Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye” (Mithali 22;7)
        Na maneno haya ni kweli kabisa. Hebu nieleze ni nani atakayesikiliza na kuyaamini maneno ya mchungaji au mwinjilisti au mtumishi yoyote wa Mungu anayesema mtegemee Yesu katika kila kitu wakati yeye mwenyewe ana nguo yenye viraka! Jambo la kwanza ambalo msikilizaji atajiuliza ni kwamba kama huyu Yesu ameshindwa kumpa mtumishi wake nguo nzuri, atawezaje kunisaidia mimi mkristo wa kawaida?
              Kwa hiyo lazima tuwe waangalifu ili tunayosema yawe sawa na tunavyoishi. Na tuishi sawa sawa na ahadi za Mungu tunazozisimamia.
              Siku moja nilimsikia mchungaji mmoja mwanafunzi wa chuo kimoja cha biblia akisema hivi; “Kuna mtu mmoja alikuja kutufundisha kuwa sisi kama wachungaji tusisikitike tunapoona hatuna nguo nzuri, wala chakula kizuri, wala sabuni nzuri za kuogea kwa sababu IKO SIKU MOJA VITU HIVI TUTAVITAWALA NA BWANA MBINGUNI”.
              Mara moja nikamkatisha na nikasema; “ Hayo mafundisho si sawa. Unadhani Mungu aliweka hivi vitu duniani (chakula, mavazi, sabuni) kwa ajili ya shetani na watu wake? Unadhani mbinguni tukifika tutahitaji tena chakula, mavazi na sabuni? Hivi vitu Mungu aliviweka kwa ajili yetu tuvitumie wakati huu.”




























Sura ya Tatu
NANI ANAUPENDA WOKOVU WA KIMASIKINI?
            “Nani anaupenda wokovu wa Ukristo wa kimaskini?” Ukiona mtu amefika hali ya kujiuliza swali la jinsi hii, ujue ana hali ngumu sana kiuchumi.

            Hili swali nilijikuta najiuliza mwenyewe baada ya kuwa na hali ngumu sana kimaisha baada kuokoka. Kuna wakati fulani baada ya kuokoka mimi na mke wangu tulijikuta tumefika mahali pa kukosa hata dawa ya mswaki, nguo, viatu, na chakula kizuri. Licha ya shida hizi zote bado zilifuata zingine baada ya ndugu zetu wawili tuliokuwa tunawalipia masomo yao kufukuzwa na kurudi nyumbani kwa kukosa ada. Na waliambiwa wasirudi shuleni bila nusu ya ada!

            Unadhani tulikuwa na furaha tena? Ingawa tulikuwa tunasema tumeokoka, na mtu akituambia ‘Bwana asifiwe’ tuliitika ‘Amina’ ndani ya mioyo yetu tulikuwa na vita vikali na maswali mengi.

            Ni vigumu kuieleza hali hiyo tuliyoipitia ilivyokuwa ngumu kwa maneno. Lakini utaelewa mtu mwenye familia anavyojisikia anapoona anakosa hata fedha za kuwanunulia mke na watoto wake chakula licha ya mavazi. Wakati huo tulikuwa na mtoto mmoja.

            Hali ilivyozidi kuwa ngumu, ndivyo nilivyozidi kusongwa na mawazo. Ilifika wakati ambapo nilikuwa naona aibu hata kukaa sebuleni, maana niliogopa hata kuwaangalia wale vijana waliofukuzwa shule, nikijua kuwa wataniangalia kwa macho ya huruma ili niwape ada warudi shule. Lakini si kwamba nilikuwa siwahurumii, bali sikuwa na fedha za kuwapa.

            Ningeanzaje kuwaambia kuwa sina fedha, wakati wanajua nafanya kazi, na pia waliona nilikuwa na fedha nyingi kabla sijaokoka? Jambo hili lilinifanya niwaze sana. Inakuwaje kabla sijaokoka nilikuwa na fedha nyingi na baada ya kuokoka najikuta nimefilisika? Ingawa ni kweli kwamba kabla ya kuokoka fedha zingine nilizipata kwa njia zilizo kinyume cha ukristo lakini nilikuwa nazo. Na baada ya kuokoka ilibidi niziache njia hizo – na matokeo yake nilijikuta nimefilisika.

            Lakini nilikuwa nimesoma katika Hagai 2:8 kuwa fedha na dhahabu ni mali ya Mungu. Na pia nilijua kuwa vyote vya Mungu ni vyangu nikiwa ndani ya Kristo. Kwa hiyo ilikuwa vigumu kuelewa kwa nini Mungu aseme fedha ni mali yake, halafu mimi niliye mtoto wake nisiwe nazo.

            Ningewezaje kusema wokovu ni mzuri wakati baada ya kuokoka nimejikuta sina fedha za kutosha kununua chakula, nguo, dawa ya mswaki na hata kukosa ada za watoto! Je ndivyo Mungu anavyotaka tuwe baada ya kuokoka?

            Wakati huo ndipo nilipoelewa kwa nini wana wa Israeli waliyakumbuka masufuria ya nyama ya Misri, ingawa walikula nyama hizo wakiwa utumwani. Ni rahisi sana mtu aliyeokoka kurudia njia au maisha mabaya ya kutafuta fedha kwa njia zilizo kinyume cha ukristo anapokuta anabanwa na matatizo ya kiuchumi maishani mwake. Na hata wakati mwingine unakesha katika maombi ili kumlilia Mungu akupe chakula na mavazi unaona kama vile hasikii.

            Nilipokuwa nasumbuliwa na hali hii ndipo nilipojikuta najiuliza mwenyewe; “ Nani anaupenda wokovu wa kimaskini?” Nilijikuta siupendi kabisa. Ni wokovu gani huu ambao haunisaidii hata kutunza familia yangu?

            Siku moja nilimuuliza mke wangu; nikasema; “Je! wewe unaupenda wokovu wa kimaskini?”

            Akajibu; “Hapa, siupendi!”

            Nikasema; “Naona tuna mawazo yanayofanana. Kwa hiyo naona ni muhimu tumuulize Mungu katika maombi kwa nini tulipokuwa kwa shetani tulikuwa na fedha za kutosha, lakini baada ya kuokoka na kuja kwake tunajikuta hatuna fedha hata za kununulia vitu muhimu?”

            Baada ya kukubaliana hayo, mimi na mke wangu tulianza kumwomba Mungu kwa mfululizo wa siku tatu juu ya jambo moja hilo hilo. Namshukuru Mungu kwa kunipa mke ambaye aliweza kusimama pamoja nami katika maombi juu ya jambo hili. Sijui ningekuwa na hali gani kama angelalamika. Namshukuru Mungu mke wangu hakulalamika bali ALIOMBA PAMOJA NAMI.

            Mungu alitujibu maombi na akaanza kutufundisha mambo mengi ambayo mengine nawashirikisha katika ujumbe huu.

            Tulijua hakika kuwa hayakuwa MAPENZI YA MUNGU tuwe na hali ngumu ya kimaisha namna hiyo – kukosa fedha za kutosha kununulia nguo, chakula na vitu vingine muhimu. Na baada ya kuyaweka katika matendo yale tuliyoambiwa na Bwana yaliyo katika neno lake, hali yetu ilibadilika. Na matatizo tuliyokuwa nayo wakati ule yakaisha. Tukaanza kuona furaha tena katika maisha haya ya wokovu.

            Ni vizuri kujua kuwa Mungu wetu hapendi tuwe maskini. Wala hapendi wokovu wa kimaskini! Ndiyo maana alimtuma Mwana wake wa Pekee, Yesu Kristo kutukomboa.

            Kwa kukumbusha tu, Yesu Kristo aliyafanya yafuatayo kwa kufa na kufufuka kwake:

            "Yesu Kristo alifanyika dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tuhesabiwe haki bure ndani yake ya kusimama tena mbele ya Mungu" 
(2Wakorintho 5:21)

            "Yesu Kristo aliuchukua udhaifu wetu, ili katika mambo yote tuzitegemee nguvu zake" (Mathayo 8:17; Wafilipi 4:13)
            Yesu Kristo aliyachukua magonjwa yetu, ili tusitawaliwe na magonjwa tena na kwa kupigwa kwake tumepona (Isaya 53:4,5; Mathayo 8:17; 1 Petro 2:24)
Yesu Kristo aliyachukua masikitiko na huzuni zetu, ili tukae katika amani yake ipitayo fahamu zote (Isaya 53:34; Wafilipi 4:6,7)
            Yesu Kristo alikuwa maskini kwa ajili yetu ingawa alikuwa tajiri, ili sisi tupate kuwa matajiri katika Yeye (2 Wakorintho 8:9)

Ndiyo maana matunga Zaburi 23 aliandika hivi:

“Bwana ndiye mchungaji wangu, SITAPUNGUKIWA NA KITU.Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake …. Hakika WEMA
NA FADHILI zitanifuata siku zote za maisha yangu; nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele”.


            Ni rahisi sana kusema. “Bwana ndiye mchungaji wangu, SITAPUNGUKIWA NA KITU, lakini je! Ni kweli hujapungukiwa na kitu? Je! Zaburi hii ni ya kweli, au ni maneno mazuri tu ya kutungia nyimbo?

            Lakini napenda kukutia moyo kuwa maneno haya ni ya kweli, ukikaa ndani ya Kristo hutapungukiwa na kitu. Ndiyo maana Mungu alimwambia Yoshua ya kuwa atii maagizo yake yote na kuyafanya HATAMPUNGUKIA WALA KUMUACHA (Yoshua 1:5)

            Kwa kuwa maneno haya ni ya kweli, mbona basi wakristo wengi WAMEPUNGUKIWA NA VITU? Tatizo haliko kwa Mungu, bali kwetu sisi. Na tuwe watendaji wa neno na tutaona mafanikio.


WAJIBU WA WAKRISTO:
            Ni wajibu wa wakristo (a) kusaidiana sisi wenyewe kiuchumi; na (b) Kuwasaidia kiuchumi watu wengine wasio wakristo. Kuna wakati fulani mtu mmoja alikuja kwangu kuomba ushauri.

            Nikamuuliza. “Una tatizo gani linalokukabili?”

            Akasema; “ Baada ya kuokoka ilibidi niache njia fulani fulani ambazo zilikuwa zinanisaidia kupata fedha kwa kuwa zilikuwa ni kinyume cha maadili ya kikristo. Lakini sasa naona napata shida, sina fedha za chakula, wala sijui kodi ya nyumba mwezi huu nitapata wapi. Licha ya hayo, wale niliowakopa fedha kufanyia biashara hizo nilizoziacha wananidai fedha zao. Hata naogopa kukutana nao. Hebu nisaidie mawazo, najua nimeokoka kweli, lakini NITAISHIJE KATIKA HALI HII?”

            Unadhani swali lilikuwa jepesi kujibu? Si swala la kumwambia tuombe halafu umwache aende zake! Yeye anachotaka baada ya kuomba aone msaada unamjia. La sivyo maombi hayo yanakosa maana kwake.

            Swali hili “Nitaishije katika hali hii?” Linawasumbua walio wakristo wengi siku hizi. Na umefika wakati wa kulijibu.

            Ngoja nikuulize swali jingine. Unadhani mwanamke ambaye anafanya uasherati ili kupata fedha za kuwalishia watoto wake hajui kuwa uasherati ni dhambi? Nina uhakika anajua kwa kuwa kuna mwingine hata kama anafanya hayo hakosi kila jumapili kanisani, na wakati mwingine hutoa sadaka kwa fedha hiyo hiyo. Unadhani hajui kuwa uasherati ni dhambi? Unadhani hamwelewi mchungaji anaposema acheni dhambi? Unadhani haogopi magonjwa ya zinaa? Unadhani anapenda kufanya hivyo? Nina hakika walio wengi hawapendi kufanya hivyo. Lakini jambo linalomsumbua, akiacha uasherati atapata wapi fedha za kuwatunza watoto wake? Nina uhakika akijibiwa swali hili ni rahisi kuacha tabia hiyo chafu.

            Wasichana wengi mashuleni wamejikuta wamebeba mimba na kuharibu usichana wao kwa kudanganywa na fedha wanazozihitaji kwa ajili ya kununulia mafuta ya kupaka, nguo, na kutengeneza mitindo ya nywele.

            Vijana wengi wa kiume wamejikuta wamejiingiza katika biashara haramu kwa sababu ya kutaka utajiri wa haraka haraka.

            Kwa sababu ya kutokujua la kufanya wakristo wengi wamepoteza ushuhuda wao kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi.

            Wakristo wenzetu walifanyaje? Tusome kitabu cha Matendo ya Mitume 4:32,34,35.

            “Na jamii ya watu waliamini (Wakristo) walikuwa na MOYO MMOJA NA ROHO MOJA; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na VITU VYOTE SHIRIKA. WALA HAPAKUWA NA MTU MMOJA MIONGONI MWAO MWENYE MAHITAJI; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa; wakaiweka miguuni pa mitume, kila mtu akagawiwa KWA KADRI YA ALIVYOHITAJI”

            Utaona katika habari hii ya kuwa kwa sababu ya Ukarimu na kutokuwa na ubinafsi wakristo hao waliweza kupambana na tatizo la umaskini katikati yao. Ndiyo maana ikandikwa kuwa; “WALA HAPAKUWA NA MTU MMOJA MIONGONI MWAO MWENYE MAHITAJI”. Jina la Bwana libarikiwe!

            Matokeo ya usharika namna hii ni haya; “Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote” (Matendo ya Mitume 4:33)

            Je! Siku hizi hakuna wakristo wenye mahitaji kati yetu? Na tunafanya nini ili kuwasaidia? Je! Kuwaombea tu kunatosha? Je! Unashangaa kwa nini ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu hautangazwi kwa nguvu na wakristo? Nadhani wakristo wengi wanatumia muda wao mwingi sana kujitafutia mahitaji yao kiasi ambacho muda unaobaki hautoshi kufanya kazi ya kushuhudia.

            Wenzetu walisaidiana, na sisi tusaidiane. Wazazi mara nyingi huwa wanawasaidia vijana wao waliowaoza kuanza maisha mapya. Na fahamu kuwa wokovu ni maisha mapya. Tunawajibika sana kuwasaidia wale wanaookoka kiroho na kimwili kuanza maisha mapya ndani ya Kristo. Kwa kukosa msaada wa kiuchumi, wengi wamepoa na kurudi nyuma.

            Niliwahi kushirikishwa ushuhuda mmoja ambao naamini utakusaidia kukuelewesha jambo hili ninalokuambia.

            Kuna mtu mmoja aliokoka baada ya muda mrefu kuwa mganga wa kienyeji na mchawi. Baada ya kuokoka ilibidi aache uchawi na uganga wa kienyeji, shughuli hizi ndizo zilizokuwa zinamsaidia kupata fedha ya matumizi.

            Baada ya kukaa miezi michache katika wokovu, bila ya kuwa na njia nyingine ya kupata fedha, ilibidi atumie akiba yote aliyokuwa nayo. Baada ya hiyo akiba kuisha akaanza kupata shida namna ya kuishi.

            Akiwa katika mahangaiko hayo, wakaja watu nyumbani kwake wakiomba msaada wa kutibiwa magonjwa yao. Hao watu walisikia kuwa yeye ni mganga wa kienyeji, wala hawakujua kuwa alikuwa ameokoka na kuacha uganga huo.

            Kwa sababu ya kukosa fedha, huyo mtu aliyeokoka akawaza moyoni mwake; “Hawa watu hawajui kuwa nimeokoka, kwa hiyo hakuna haja ya kuwaambia, kwani kuna ubaya gani nikienda kuwachimbia dawa ninazozifahamu halafu wanipe fedha inisaidie?”

            Kwa hiyo akaenda akawachimbia hizo dawa akawapa. Na hao watu wakaondoka baada ya kumlipa fedha. Lakini usiku, huyo aliyeokoka alipokuwa amelala aliona katika maono. Katika maono hayo akayaona majini mawili yaliyokuwa yanamsaidia katika uchawi zamani kabla ya hajaokoka. Hayo majini yakasema; “Tulikwaambia hutafanikiwa katika wokovu, sisi ndiyo tumekufilisi mali yako. Na pia sisi ndiyo tuliowatuma wale wagonjwa waje kwako. Ulipochima zile dawa ukatuita tulikokuwa. Sasa tumekuja, mwache Yesu njoo kwetu nasi tutakutajirisha”.

            Huyo mtu aliyeokoka aliposikia hayo, akatambua kosa lake, na mara hiyo akalikumbuka jina la Yesu Kristo. Kwa hiyo akayakemea yale majini nayo yakatoweka. Akamka akiwa anatetemeka.

            Kama asingelikumbuka uwezo wa jina la Yesu Kristo, angefanya nini? Naamini kama angepata msaada wa mahitaji yake toka kwa wakristo wenzake, asingebanwa na mtego huo. Wakristo naomba kuwakumbusha kusaidiana. Ni muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku.

            Ndiyo maana Mtume Paulo aliongozwa na Roho Mtakatifu kuandika hivi:

            “Kwa habari za kuwahudumia watakatifu (Wakristo) sina haja ya kuwaandikia. Maana najua utayari wenu, ninaojisifia kwa ajili yenu kwa Wamakedonia, kwamba Akaya ilikuwa tayari tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo wengi wao ……. Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu (Wakristo) riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu, kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote” (2Wakorintho 9:1,2,12 – 15)

            Ndiyo maana pia katika makanisa kuna mgawanyiko wa huduma. Kuna wengine kazi yao ni kuhubiri na kuwaambia watu waache dhambi kama, uasherati na wizi. Ni wajibu wa wale wanaoshughulika na mambo ya miradi ya maendeleo katika kanisa ni kusaidiana na wahubiri hao kuwaongoza watu waishije baada ya kuacha uasherati na wizi.

            Napenda kukuhimiza hata wewe unayeyasoma haya kuwa, ukiona mwenzako ni mhitaji wa kitu fulani ambacho unacho, usisite kumsaidia. Kumbuka huduma hii ina thawabu yake kama Mtume Paulo anavyosema.

            Hebu jibu swali hili; “Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?" (1Yohana 3:17)

            Mzee Yohana anatushauri anasema, “Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli” (1Yohana 3:18).

            Ni kweli Bwana Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani alikuwa maskini, lakini baada ya kufufuka alirudishiwa utajiri wake. Ndiyo maana Mtume Paulo anazungumzia juu ya “……… utajiri wake Kristo usiopimika” (Waefeso 3:8). Na katika Wafilipi 4:19 tunasoma hivi; “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu”.

            Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alichukua madhaifu yetu na magonjwa yetu yote, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona (Isaya 53:5; Mathayo 8:16, 17; 1Petro 2:24). Na kwa kujua hili kanisa linajihusisha na kuombea wagonjwa na kutoa huduma za afya kwa wagonjwa.

            Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alichukua dhambi zetu na akafanyika dhambi kwa ajili yetu, “Ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye” (2 Wakorintho 5:21). Na kwa kujua hili kanisa linahubiri habari za ondoleo la dhambi kwa ye yote atakayemwamini Kristo.

            Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alikuwa maskini, ingawa alikuwa tajiri, ili kwa umaskini wake sisi tupate kuwa matajiri (2Wakorintho 5:21). Na kwa kujua hili kanisa linajihusisha na miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili mtu aondokane na umaskini. Wakristo binafsi pia wanashauriwa kuwa na miradi isiyovunja maadili ya kikristo, ili waondokane na umaskini.










Sura ya Saba

UKITOA TEGEMEA KUPOKEA

            Sehemu nyingi nilizotembelea nimeona na kufahamu ya kuwa watu wengi wanatoa sadaka – fedha taslimu au vitu au wanyama kwa Mungu BILA KUTEGEMEA KUPOKEA KUTOKA KWA MUNGU.

             Furaha ya utoaji inatokana na kufahamu matokeo ya utoaji huu. Ndiyo maana mkristo yuko tayari kuweka shilingi 10,000/= katika mradi utakaompa faida kuliko kutoa kanisani ambako anafikiri sadaka hiyo haina faida kwake binafsi. Kwa hiyo siku zote atatoa sadaka kidogo kanisani au kwenye kazi ya Mungu.

            Bila ya mkristo kujua kwamba anajua na kuwa na uhakika moyoni mwake kuwa akitoa sadaka anastahili kupokea ZAIDI YA KIWANGO ALICHOTOA KUTOKA KWA  MUNGU – utoaji wake utakuwa chini siku zote.

            Wakristo wengi wanafikiri wakimtolea Mungu kitu, watazidi kupungukiwa na kufilisikia. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba ukimtolea Mungu ulicho nacho UNAFUNGUA MLANGO WA KUFANIKIWA kwa ulivyo navyo. Unapomtolea Mungu hufilisiki bali unatajirika!

             Tunapokuwa ndani ya Kristo, tunachukua na kubeba tabia ya Mungu ndani yetu. Imeandikwa hivi:

“ Bali wote waliompokea(Kristo) aliwapa UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12) “ Kwa kuwa UWEZA wake wa UUNGU umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe” (1Petro 1:13)

        Ni vizuri ufahamu ya kuwa mojawapo ya tabia ya Uungu tuliyo nayo ndani yetu katika Kristo ni tabia ya kutoa HUKU UKITEGEMEA KUPOKEA. Mungu akitoa kitu anategemea kupokea.

Tabia ya Mungu ya Utoaji

            Mungu alipokuwa anamtoa mwana wake wa pekee, alimtoa huku akitegemea kupata watoto wengi wa kiroho. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16)
            Mungu alipokuwa anamtuma Roho Mtakatifu juu ya wanafunzi wake, alimtoa huku akitegemea kupata mashahidi wengi watakaosimama upande wake na kulitetea jina lake hapa duniani. “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalem, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi” (Matendo ya Mtume 1:8)
            Mungu anapotoa utajiri kwa watu wake, anautoa huku akitegemea kupata agano lililo imara kati yake na wanadamu. “ Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako,kama hivi leo” (Kumbukumbu la Torati 8:18).
          
  Hii ndiyo tabia tuliyo nayo ndani ya Kristo, kutoa huku tukitegemea kupokea. Hili jambo la kutoa na kupokea wakati mwingine linajulikana kama KUPANDA na KUVUNA.
            Hakuna mkulima anayepanda mbegu shambani bila kutegemea kuvuna. Kama hana tegemeo la kuvuna, basi hata haja na hamu ya kupanda inapotea – inakuwa haina maana kupanda maana hatapata kitu.
            Katika mambo ya kiroho ni vivyo hivyo. Utakachotoa ndicho utakachopata. Utakachopanda ndicho utakachovuna. Ukipanda fedha utavuna fedha. Ukipanda upendo utavuna upendo. Ukipanda ng’ombe utavuna ng’ombe. Ukitoa vitabu utapokea vitabu. Imeandikwa hivi; “ Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna” (Wagalatia 6:7).
            Hivi ndivyo ilivyo, utakachopanda ndicho utakachovuna. Kwa maneno mengine, ni kwamba ukipanda tegemea kuvuna.

Tumia tabia ya Mungu iliyo ndani yako

            Ikiwa wewe unakaa ndani ya Kristo na Kristo anakaa ndani yako, basi uwe na uhakika ya kuwa tabia ya Uungu ya kutoa na kupokea, kupanda na kuvuna imo ndani yako.
            Inaonekana wazi ya kuwa wakristo wa kanisa la Korintho na Filipi katika nyakati za huduma ya Mtume Paulo – walishiriki sana katika habari hii ya kutoa na kupokea. Siyo kutoa bila kupokea bali kutoa na kupokea. Hii ni tabia iliyoonekana wazi katika ukristo wao. Hebu soma maneno yafuatayo juu ya habari hii katika kitabu cha Wafilipi katika nyakati za huduma ya Mtume Paulo – walishiriki sana katika habari hii ya kutoa na kupokea. Siyo kutoa bila kupokea bali kutoa na kupokea. Hii ni tabia iliyoonekana wazi katika ukristo wao. Hebu soma maneno yafuatayo juu ya habari hii katika kitabu cha Wafilipi 4:10-14;

            “ Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa  mwisho mmehuisha tena fikra zenu kwa ajili yangu,    kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu; lakini mkupata nafasi. Si kwamba nasema haya kwa kuwa  nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali  yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefudishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. LAKINI MLIFANYA VEMA, mliposhiriki nami katika dhiki yangu”.

             Mtume Paulo hapa anawaambia Wafilipi wazi kuwa maisha yake yote na katika mambo yote na katika hali yo yote tumaini lake na ushindi wake ni katika UWEZA WA KRISTO amtiaye nguvu – na wala si katika uweza wake Paulo au huruma za wanadamu. Hata hivyo aliwaambia “MLIFANYA VEMA MLIPOSHIRIKI NAMI KATIKA DHIKI YANGU”. Katika maneno yanayofuata aneleza kwa nini walifanya vema kumhudumia katika dhiki yake.

            “Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa   katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna   kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya     KUTOA NA KUPOKEA, ila ninyi peke yenu. Kwa kuwa  hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji  yangu, wala si mara moja. Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali NAYATAMANI MAZAO YANAYOZIDI KUWA MENGI, katika HESABU YENU” (Wafilipi 4:15 – 17).

            Ni wazi kabisa ya kuwa kwa sababu ya kushiriki katika habari ya KUTOA NA KUPOKEA – Wafilipi hawakufilisika wala kupungukiwa bali MAZAO YALIZIDI KUWA MENGI KATIKA HESABU YAO. Huyu Mungu aliyewafanikisha Wafilipi, ndiye atakayekufanikisha wewe na kuongeza mazao mengi katika habari hii ya KUTOA na KUPOKEA.

            Kumbuka siku zote kuishi kwa kuitumia na kutegemea tabia ya Mungu iliyo ndani yako katika Kristo. Tabia hii itakusaidia kutoa na kutegemea kupokea – kupanda na kutegemea kuvuna. Imeandikwa hivi

            “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa – sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu” (Luka 6:38)











Sura ya Nane 

SADAKA NA WOKOVU

             “Palikuwa na mtu Kaisaria jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu SADAKA NYINGI, na kumwomba Mungu daima. Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio! Akamtazama sana, akaogopa akasema, kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na SADAKA ZAKO zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. Sasa basi, peleka watu Yafa, ukamwite Simoni, aitwaye Petro. Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi, ambaye nyumba yake iko pwani; ATAKUAMBIA YAKUPASAYO KUTENDA” (Matendo ya Mitume 10:1 – 6).
            Tabia hii ya Kornelio ya kuwa mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, na pia tabia ya utoaji wa sadaka na kumwomba Mungu daima, inaonyesha wazi kuwa Kornelio alimpenda Mungu sana na alikuwa anatafuta namna yakukubalika mbele zake na namna ya kumpendeza Yeye.
            Tungezungumza kwa lugha nyepesi zaidi, ni kwamba alitaka kwa MATENDO YAKE aende mbinguni na kuurithi Uzima wa Milele baada ya kufa kwake . Kwa kifupi alimtafuta Mungu kwa njia ya Matendo.
            Hii ina maana ya kuwa Kornelio alitaka kuvuna  baraka za Agano Jipya katika damu Yesu, wa kutumia njia za kupendeza Mungu zilizomo katika Agano la Kale.
            Tena ingawa yeye hakuwa Myahudi kwa kuzaliwa, alitaka sana kuvuna baraka ambazo Mungu aliahidi juu ya Wayahudi.
            Mpaka hivi leo kuna watu wengi wanataka kuvuna baraka toka kwa Mungu bila kutumia utaratibu aliouweka Mungu wa kuzipokea. Ni vigumu sana kupokea ahadi za Mungu nje ya mpango wake.
            Huwezi kupokea ahadi za agano la kale kwa kutumia mbini za agano la kale na huku sasa hivi tumo katika kipindi cha agano jipya.
            Baraka zote zilizomo katika agano la kale aliahidiwa Ibrahimu na uzao wake MILELE. Soma mwenyewe Mwanzo sura ya 17 na 22. Kwa hiyo ukitaka kupokea baraka za agano la kale lililofungwa kati ya Mungu na Ibrahimu, inabidi uwe mzao au mtoto wa Ibrahim. - Kornelio hakufahamu hili; hata leo hii wengi hawafahamu.
            Baraka zote zilizomo katika agano jipya zimeahidiwa wale walio ndani ya Kristo – waliotoa maisha yao kwa Yesu kama vile Yesu Kristo alivyotoa maisha yake kwa ajili yao.
            Ni vigumu kupokea baraka za ahadi za agano la kale na zile za agano jipya NJE YA YESU KRISTO. Imeandikwa hivi katika Wagalatia 3:13,14,29;

“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, baraka ya Ibrahimu IWAFIKILIE MATAIFA KATIKA YESU KRISTO, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani…… Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi. "

  Ndiyo maana Mungu alimtuma Malaika wake ili amwambie Kornelio kuwa amwite Simon Petro ili awaeleze habari za Yesu Kristo – ili baraka ya Ibrahimu iwafikie na wapate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani –  SIYO KWA MATENDO PEKE YAKE.
            Jambo ambalo Mungu alitaka Kornelio ajue na sisi pia tujue ni kuwa matendo mema, maombi na SADAKA bila “kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani” yaani kuzaliwa mara ya pili kwa Roho au kuokoka – haitoshi  kumpendeza Mungu, wala kukubalika mbele zake au kuhesabiwa haki.

            Ndiyo maana Yesu Kristo alimwambia Nikodemo, yule Farisayo kuwa “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu ….. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, HAMNA BUDI kuzaliwa mara ya   pili”(Yohana 3:3,7).
            Haya maneno “Hamna Budi” maana yake ni “lazima” kwa hiyo Yesu Kristo alikuwa anasema “…… LAZIMA kuzaliwa mara ya pili”.
            Yesu Kristo alikuwa anasisitiza kwa Nikodemo, na hata kwetu sote tunaotaka kuurithi ufalme wa Mungu, kuwa hakuna njia nyingine isipokuwa LAZIMA kuzaliwa mara ya pili kwa Roho (au kwa maneno mengine) LAZIMA Kuokoka!
IMANI NA MATENDO
          Matendo peke yake hayatoshi kukupa ufalme wa Mungu. Kuna watu wengi sana ambao ni waaminifu sana katika kusali na kumtolea Mungu sadaka, lakini hawakubaliani na jambo kuokoka. Wanaona kuwa wao tayari wameokoka kwa sababu tu wanasali, wanatoa sadaka na kujitahidi kuishi katika matendo mema. Hebu soma   maneno ya mistari hii uone yanavyopingana na msimamo huu;

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; WALA SI KWA MATENDO, mtu awaye yote asije akajisifu” (Waefeso 2:8,9)

            Tunaokoka kwa njia ya imani itendayo kazi katika Yesu Kristo, “Wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”. Matendo yana faida zaidi kwa mtu baada ya kuokoka. Na pia imani bila matendo, imani hiyo imekufa nafsini mwake. Biblia inasema hivi:
           “Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! ile imani yaweza kumwokoa?…. Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. Lakini mtu atasema, wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha IMANI YANGU KWA NJIA YA MATENDO YANGU …….. Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa” (Yakobo 2:14,17,18,26).
           Jambo ambalo Yakobo alikuwa anasisitiza hapa ni kutaka kuwaonya watu kuwa kusema wewe ni mkristo na huku matendo yako hayalingani na ushuhuda wa mdomo wako ni bure. Wokovu uonekane katika maisha yetu kila siku – la sivyo imani tuliyo nayo inakosa kuzaa matunda ya uzima wa milele. Ndiyo maana Yesu Kristo aliwahi kuzungumza juu ya kukatwa kwa tawi (Mkristo) lisilo zaa, soma Yohana 15:1-8 ili upate picha zaidi juu ya jambo hili.

CHUKUA HATUA LEO

          Malaika alimwambia Kornelio atume watu wakamwite Simoni aitwaye Petro ili AMWAMBIE YAMPASAYO KUTENDA. Mungu kwa uweza wa Roho wake Mtakatifu amekuletea maneno haya mkononi mwako ili UFAHAMU YAKUPASAYO KUTENDA.
          Kama hujaokoka na unadhani unaweza kuokoka kwa kutoa sadaka nyingi NAKUSHAURI KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI uombe sala hii kwa sauti, ili utubu na kumpa Yesu Kristo maisha yako leo. HALAFU endelea kutoa sadaka nyingi ukiwa ndani ya Yesu Kristo.
           Omba sala hii kwa sauti; “Mungu Baba, unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu. Ninatubu kwako. Nitakase kwa damu ya Yesu Kristo. Bwana Yesu Kristo nimefungua moyo wangu nakukaribisha uingie ndani yangu, kwa uwezo wa Roho wako. Uwe Bwana na Mwokozi wa maisha yangu – sasa na hata milele. Asante kwa kunisamehe dhambi na kuniokoa. Amina”.
            Ikiwa umeisema sala hii kwa uaminifu, basi umefanyika kiumbe kipya – umezaliwa mara ya pili na Mungu hakumbuki dhambi zako tena. Soma 2Wakorintho 5:17, Waebrania 8:12. Karibu sana katika ufalme wa Mungu kwa jina la Yesu Kristo!
         Hili ndilo lililotokea kwa Kornelio na jamaa yake, Simoni Petro alipofika kwao aliwaambia habari za Yesu Kristo – walisikia maneno hayo wakamwamini Yesu na kujazwa na nguvu za Roho Mtakatifu wakati huo huo.










Sura ya Tisa
NATOA LAKINI SIPOKEI – NIFANYEJE?
             Kuna wakati fulani, mtu mmoja alinifuata baada ya kipindi nilichokuwa nafundisha Neno la Mungu juu ya utoaji, na akaniuliza hivi; “Kwa nini mimi nimekuwa natoa zaka na sadaka nyingi lakini sipokei? Hata miradi niliyo nayo haifanikiwi nilivyokusudia – ni kwa nini iwe hivyo.
            Inawezekana na wewe unayesoma ujumbe huu sasa una maswali kama haya. Hayo ni maswali ya msingi na ni muhimu tupate ufumbuzi wake. Hata mkulima ambaye alipanda mbegu katika shamba, na asipate kitu au apate mavuno machache, atajiuliza maswali kumetokea kitu gani.
           Tukumbuke ya kuwa si mapenzi ya Mungu tuwe maskini – tuwe na hali ngumu kimavazi, chakula na kiafya. Pia, tukumbuke ya kuwa ni tabia ya kiuungu mtu kutoa na kutegemea kupokea. Ingawa si lazima upate toka kwa mtu huyo huyo uliyempa, - maana Mungu anaweza kumgusa mtu mwingine akupe – lakini utaratibu wa Mungu unabaki pale pale, ukitoa tegemea kupokea.
            Ni kitu gani kinasababisha mtu asipokee na huku amekuwa akijitahidi kutoa? Biblia inatuambia ya kuwa tukiwa waaminifu katika utoaji, Mungu atatumwagia baraka, “hata isiwepo nafasi ya kutosha ya kuziweka” – Je! umewahi kumsikia mkristo yo yote akisema amepata baraka nyingi mno hata amekosa mahali pa kuziweka?
Sababu zifuatazo zitatusaidia kujua ni kwa nini hatufanikiwi katika utoaji wetu – na hata hatupokei kama tulivyotegemea na kutarajia;
1. KUVUNJA MIIKO AU UTARATIBU WA UTOAJI

            Kila jambo lina utaratibu wake – usipoufuata usitegemee mavuno mazuri. Kilimo cha mahindi kina utaratibu wake wa upandaji na palizi tofauti na kilimo cha ngano au cha kabichi. Ndiyo maana wataalamu wa kilimo, walianzisha kampeni za kuwafundisha wakulima juu ya “kilimo cha kisasa” ili kiwasaidie wakulima kupata “mavuno” zaidi toka katika mashamba yao.

        Hata katika “kupanda na kuvuna” au “kutoa na kupokea” katika mambo ya Mungu kuna utaratibu wake. Ukienda kinyume na utaratibu huo, usitegemee mavuno ya kuridhisha toka katika utoaji wako 
Kwa mfano hebu soma na kutafakari maneno haya yafuatayo:

            “Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama ilivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana   Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu” (2Wakorintho 9:6,7).

“….wala si kama kitu kitolewacho kwa unyimivu” (2Wakorintho 9:5).
            Utaona katika mistari hiyo Mungu ametueleza kwa kiasi fulani utaratibu ambao anataka ufuatwe mtu akitaka kuvuna katika utoaji wake. Je! unafuata utaratibu huu katika utoaji wako?
           Utaratibu huo ni huu; utoaji wako uwe si haba (au kidogo) bali uwe kwa ukarimu. Ukitoa kidogo utapata kidogo – bali ukitoa vingi utapata vingi. Ndiyo maana imeandikwa;
            “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. KWA KUWA KIPIMO KILE KILE MPIMACHO NDICHO MTAKACHOPIMIWA” (Luka 6:38)
           Kama unataka kutoa sadaka tu “ kama ulivyokusudia moyoni mwako”. Kama ulikusudia kutoa shilingi 100/= toa shilingi 100/=. Fanya hivi siku zote na utafanikiwa.
           Tena, utoaji unatakiwa ufanyike “si kwa huzuni; wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu  “… na wala si kwa unyimivu”.
           Michango mingi iliyomo makanisani siku hizi  wakati mwingine inafanyika kwa kulazimishana. Mtu anatakiwa atoe kwa kupenda kwake toka moyoni mwake – SI KWA LAZIMA. Kumlazimisha mtu kutoa ni kwenda kinyume cha utaratibu wa utoaji.
           Wakristo wengi wamekosa baraka au mafanikio katika utoaji kwa sababu wanatoa huku WANAHUZUNIKA AU WANALALAMIKA! Wengi wanawanung’unikia viongozi wa makanisa yao kuwa wanatumia fedha au vitu vibaya. Kama una wasiwasi na matumizi ya matoleo yako – yaombee kwa Mungu ayalinde yatumike kwa utukufu wake kuliko kulalamika.
             Wengine wanahuzunika na kulalamika kuwa michango imezidi. Je! umewahi kumsikia mkulima akihuzunika au kulalamika kwa kuwa ameongezewa shamba la kulima na kupanda? Hakuna. Mkulima halalamiki bali anafurahi kwa kuwa amepata eneo kubwa zaidi la kupanda umeongezewa eneo la KUPANDA ili AVUNE ZAIDI. Ni eneo la kukusaidia kutoa zaidi ili UPOKEE ZAIDI!
2. IBILISI AMEZUIA BARAKA ZAKO;

           Kati ya baraka ambazo zinapatikana kutokana na mtu kuwa mwaminifu katika utoaji wa zaka (fungu la kumi) na dhabihu (matoleo mbalimbali) na kuzidiwa wakati wa matatizo, Mungu alisema hivi;

         “Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba ….” (Malaki 3:11).

            Ni wazi kuwa aliye nyuma ya kuharibika kwa mazao shambani au biashara ni yule ‘alaye’ ambaye ni Ibilisi. (Hii ni kama mkulima au mfanya biashara amefanya anachotakiwa kukifanya kilicho ndani ya uwezo wake).

            Kinyume cha jambo hili ni kwamba usipokuwa mwaminifu kutoa fungu la kumi toka katika mazao ya shamba lako, usitegemee Mungu akupiganie wakati mharibu anapoingilia mimea yako na kuiharibu. Vile vile usipokuwa mwaminifu kutoa fungu la kumi toka katika mapato ya biashara yako, usitegemee Mungu akusaidie wakati mharibu anapoingilia biashara yako na kuiharibu.
            Inawezekana unatoa sadaka, na huoni baraka zozote zinazotokana na kutoa kwako – hebu angalia na jichunguze kama umekuwa mwaminifu katika kutoa ZAKA KAMILI. Kwa mfano kama fungu la kumi la pato lako ni shilingi 2,000 – toa zaka kamili yaani shilingi 200/=. Usitoe pungufu ya hiyo maana haitakuwa zaka KAMILI.
           Ikiwa umekuwa mwaminifu katika kutoa Zaka kamili na dhabihu halafu huoni matokeo yake basi, tumia mamlaka ya Jina la Yesu Kristo – mfunge na kumkemea ibilisi ambaye ndiye mharibu wa mali yako aondoe mikono yake juu ya mali yako.

 Kumbuka Yesu Kristo alisema;
            “Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalofunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Mathayo 16:19).

    Kuna mtumishi mmoja wa Mungu ambaye anasimulia jinsi ambavyo mkulima mmoja wa pamba alivyosaidika na uwezo wa jina la Yesu Kristo.
    Huyo Mkulima alikuwa mwaminifu katika kumtolea Mungu fungu la kumi la mapato ya shamba lake kila mwaka, na alikuwa haelewi kwa nini pamba yake ilikuwa haifunguki ingawa muda wa kufunguka na kuchanua ulikuwa umefika. Wataalamu wa kilimo cha pamba walikuja kuliangalia shamba hilo lakini hawakuweza kumsaidia mkulima huyo kutatua tatizo hilo.
    Mtumishi wa Mungu huyo alifika hapo, na alisikia habari ya mahangaiko ya mkulima huyo. Baada ya kufahamu ya kuwa mkulima huyo alikuwa mwaminifu katika kutoa fungu la kumi – alimwambia waende shambani ili waombe.
    Huyo mtumishi wa Mungu wakiwa shambani na mkulima huyo; - akimkumbusha Mungu juu ya ahadi yake ya Malaki 3:7-11. Na mwishoni akamwamuru ibilisi aondoke kwenye pamba hiyo. Mara tu baada ya kumaliza sala hiyo – pamba ilianza kufunguka na kuchanua! Bwana asifiwe sana kwa uwezo huu ulivyo wa ajabu.
        Usibaki unalalamika na kuhangaika kama vile mtu asiyejua ahadi za Mungu. Simamia haki zako ndani ya Kristo kwa kuwa mtendaji wa neno na utafanikiwa.
3. KUTOKUPANDA KATIKA UDONGO MZURI

           Utoaji ni sawasawa na upandaji. Mtu akipanda anategemea kuvuna pia. Kwa hiyo mtu akitoa anategemea kupokea.

    Mkulima yo yote akitaka mavuno mazuri toka shambani mwake kati ya vitu anavyoviangalia ni aina ya mbegu na aina ya udongo. Siku zote atapanda kwenye udongo mzuri wenye rutuba.
            Mfanya biashara siku zote anataka aweke mtaji wake katika vitu vitakavyomletea faida kibiashara na siyo hasara.
            Lakini, inasikitisha kuona kuwa inapofika wakati wa utoaji – wakristo wanatoa tu bila kuangalia kwanza “udongo mzuri” ni upi ili utoaji wao uwaletee matokeo mazuri.
    Biblia inatuambia katika mfano wa mpanzi ya kuwa mbegu zingine“…. Zikaanguka penye udongo ulio mzuri, zikazaa matunda, zikimea na kukua, na kuzaa, moja thelathini, moja sitini, na moja mia” (Mathayo 4:8).
         Je, “udongo mzuri” unaoleta faida nzuri ni upi? Sehemu za kutoa zenye matokeo au mavuno mazuri ni hizi zifuatazo;
(a)         Katika nyumba ya Mungu – kanisani ili kuendeleza kazi ya Mungu – soma Malaki 3:10-11; na Kumbukumbu ya Torati 8:18.
(b)        Kuwasaidia watumishi wa Mungu na watakatifu wake kwa vitu/mali ulizo nazo. Soma 1Wafalme 17:10-24 na 2Wakorintho 9:10-13.
(c)         Kuwasaidia maskini kwa vitu/mali ulizo nazo. Soma 2Wakorintho 9:8-9.
    Angalia upandaji wako katika utoaji – je! umepanda kwenye udongo ulio mzuri?
4.  KUKATA TAMAA

           Wagalatia 6:9 inasema hivi; “Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho”.
Tafsiri iliyo nyepesi inasema, “maana tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa”.
            Wakristo wengi wanatoa lakini hawana uvumilivu. Mkulima asipokuwa mvumilivu kusubiri mazao ya shamba lake yanayokuja kwa wakati wake – hawezi kuvuna alichopanda.
            Vile vile mtoaji asiyejifunza kumvumilia Mungu ili amletee matokeo ya utoaji huo kwa WAKATI WAKE – hawezi kuvuna alichopanda.
            Mungu si mwongo! Wala ahadi zake hazijui kusema uongo. Alichoahidi atatenda. Ukitoa utapokea KWA WAKATI WAKE USIPOKATA TAMAA.
            Usianze kutafuta njia za mkato ili ufanikiwe – uwe mvumilivu ulichopanda kwenye udongo mzuri utavuna.
            Mkumbuke Ibrahimu alivyovumilia. Biblia inasema hivi;
            “Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi” (Warumi 4:20-21).

5.KUTOA KWA MAJIVUNO NA KUTAFUTA KUSIFIWA NA WATU

            “Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili WATUKUZWE NA WATU. Amin, nawaambieni,wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na BABA YAKO AONAYE SIRINI ATAKUJAZI” (Mathayo 6:1- 4)











Sura ya Kumi
UFANYEJE KATIKA HALI NGUMU YA UCHUMI?
Matatizo ya ugumu wa uchumi katika dunia hii siyo mapya. Tangu baada ya mwanadamu kuanguka katika dhambi – amekuwa mara kwa mara akisumbuliwa na matatizo ya uchumi. Ukisoma habari za Isaka na za Yakobo utaona jinsi hali hii ilivyojitokeza.
Lakini biblia inaeleza wazi kuwa siku hizi ni mwisho. Katika siku hizi za mwisho, biblia pia inasema wazi kabisa kuwa dunia itapita kwenye vipindi vigumu vya uchumi
Kwa Mfano: Katika Mathayo 24:7 na Ufunuo wa Yohana 6:3-6 tunaona ya kuwa katika siku hizi za mwisho kutatokea njaa – au upungufu wa chakula. Sababu ya kuja kwa njaa hiyo ni vita vitakavyokuwa vinatokea katika nchi mbalimbali. Ni wazi kabisa kuwa palipo na vita au palipo na ugomvi, panakuwa na matatizo ya ulimaji mashamba na usafiri wa kuleta chakula toka sehemu zingine. Matokeo ni hilo eneo au nchi kukosa chakula, haya mambo yaliyotabiriwa kutokea siku hizi za mwisho wa dunia.
Ukisoma katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana sura za 17 na 18 utaona ya kuwa hali ngumu ya kibiashara imetabiriwa kutokea katika siku hizi za mwisho. Kuuza au kununua kutafanyika kwa vibali. Watu watapenda fedha sana kuliko kumpenda Mungu. Kutakuwa na uhusiano mkubwa sana kati ya utajiri na biashara na uasherati. Wafanya biashara wa siku hizi za mwisho watakuwa na sehemu kubwa katika utawala wa miji au vijiji wanavyokaa – hata wakati mwingine katika maongozi ya nchi au mataifa mbalimbali.
Matokeo ya hali namna hii inawafanya watu watafute njia au mbinu za kuweza kuishi katika vipindi vya namna hiyo. Lakini ni wazi kuwa si mbinu zote au njia zote ambazo wanadamu wanazitumia katika kuishi wakati wa hali ngumu ya uchumi zinampendeza Mungu.
Kunapotokea hali ngumu ya uchumi, tabia za watu zinabadilika. Mara kwa mara mambo yafuatayo hutokea;
Kubana matumizi Kununua vitu kwa wingi na kuvirundika Uchoyo – kupunguza tabia ya utoaji na ukarimu Watu huacha kumtumikia Mungu na badala yake mtu huitumikia mali Rushwa, wizi na dhuluma huwa ni vitu vya kawaida Miradi ya kila namna huibuka kuanzia kwa watoto hadi watu wazima.
Jambo linalowafanya watu wawe na tabia hizi, ni lile la kutaka kutafuta namna ya kuishi katika kipindi kigumu cha uchumi. Je!mkristo afanye nini ili aishi katika kipindi hiki kigumu cha uchumi bila kufanya mambo yatakayomkosea Mungu?
Wakristo wengine wamefika mahali pa kuhalalisha miradi ya kuwapatia fedha ambayo ni kinyume na ushuhuda wa kikristo – Je! hii ni sawa?
Wengine wamefika hata mahali pa kufunga nira na wasioamini (wasio wakristo) KWA JINSI ISIYO SAWASAWA (yaani isiyokubalika) na neno la Mungu ili waweze kupata fedha kutokana na mradi wanaofanya pamoja. IKO "jinsi iliyo sawasawa" na utaifahamu ikiwa utakuwa mtendaji wa neno la Mungu.
Wakristo si wa ulimwengu huu
Ndugu au Dada unayesoma sasa mambo haya – sikiliza! Sisi kama wakristo si wa ulimwengu huu ingawa tunaishi hapa ulimwenguni. Fahamu na kumbuka hili kila wakati. Yesu Kristo alisema hivi;
"Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni" (Yohana 17:14-18).
Je! unafikiri Yesu Kristo anaweza kututuma hapa duniani bila kutuandaa kuishi kiushindi katika majaribu yaliyomo ndani yake na hali ngumu ya uchumi?
Je! unadhani Yesu Kristo anaweza kukuokoa halafu asikutunze kiuchumi katika maisha mapya ya wokovu? Nafahamu kuna wakristo wengi walioanguka kiroho kwa sababu ya kutafuta njia za kujisaidia kimaisha.
Biblia inatuambia ya kuwa Yesu Kristo huwalisha na kuwatunza watu wake ili ajiletee kanisa (wakristo) walio watakatifu. Soma Waefeso 5:25-33.
Katika vipindi vyote vya matatizo ya uchumi, Mungu ameweza kuwalisha na kuwatunza watu wake. Wamekula na kuvaa na kulala ndani ya mpango wake bila kumkosea.
Katika siku hizi za mwisho, Kristo anazungumza na kulikumbusha kanisa (wakristo) juu ya njia au mbinu za kuchukua wakati wa hali ngumu ya uchumi mahali walipo.
Mashauri muhimu ya kufanya
Fuata maongozi ya Mungu na siyo ya dunia: Ni rahisi sana kusikia na kufuata ushauri wa wanadamu kuliko ushauri wa Mungu hasa mtu anapobanwa na shida. Lakini kwa mkristo nakushauri siku zote kuwe na shida au kusiwe na shida, fuata ushauri wa Mungu kama vile anavyokuongoza kwa Roho Mtakatifu katika neno lake. Tuangalie jinsi Isaka alivyofanya alipokumbwa na hali ya njaa.
"Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Ibrahimu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari. Bwana akamtokea, akasema, usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia …. Nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki …" (Mwanzo 25:1-3).
Njaa ilipotokea huko Gerari, watu walianza kuondoka huko na kwenda Misri, ili kutafuta chakula. Ni wazi ya kuwa hata Isaka alitaka kufanya hivyo. Bwana akamzuia akamwambia asiondoke bali akae katika nchi aliyomwambia na katika nchi hiyo atakuwa pamoja naye na kumbariki au kumfanikisha.
Nataka kukukumbusha ya kuwa baraka za Mungu kwetu hazitegemei jinsi hali ya hewa na uchumi wa dunia hii unavyokwenda bali zinategemea NENO LA KRISTO.
Isaka akatii, hakuondoka bali alibaki katika nchi hiyo ambayo watu walikuwa hawapati chakula wakilima.
"Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, Bwana akambariki" (Mwanzo 26:12).
Siku zote kaa na kufanya kazi mahali ambapo Mungu amekuongoza kukaa. Usihame mahali au kuacha kazi, bila uongozi wa Mungu. Kufanikiwa kwako hakutegemei mipango yako bali kunategemea mpango wa Mungu.
Ukiwa ndani ya Kristo utafanikiwa mahali po pote pale ambapo Mungu atakapokuweka hata kama mazingira yake kibinadamu si mazuri kwa kufanikiwa. Ukiwa ndani ya Kristo, "Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani … utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa utokapo …. Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako" (Kumbukumbu ya Torati 28:3,6,8).
Endelea kutoa hata wakati wa upungufu
Katika hali ya kibinadamu upungufu unapotokea mahali watu wanabana matumizi – na hali ya ukarimu na utoaji huwa inafifia sana hata wakati mwingine kupokea kabisa. Wakristo wengi pia wamekumbwa na hali hii – wanasema wamepunguza utoaji kwa kuwa wamepungukiwa na hali ya uchumi ni ngumu. Je! hii ni sawa?
Wakati wa ukame ulipotokea wakati wa maisha ya Nabii Eliya Mtishbi; Bwana alimwambia Eliya, "Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe" (1Wafalme 17:9).
Unakumbuka jinsi yule mama alivyojitetea wakati Eliya alipofika kwake ili alishwe? Yule mama alijitetea kama watu wengine wanavyojitetea siku hizi wakitakiwa kutoa au kuchanga walivyo navyo kwa ajili ya kazi ya Mungu. Naye yule Mjane akasema;
"Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tule tukafe" (1Wafalme 17:12).
Kwa jinsi ya kibinadamu, Eliya angeweza kumwonea huruma yule mama, asile chakula chake; na aondoke na aende kwa matajiri wa siku zile kupata chakula. Lakini Eliya hakufanya hivyo- bali ALITII MAAGIZO YA MUNGU. Eliya akamwambia yule mjane hivi;
"Usiogope;enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie KWANZA mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao" (1Wafalme 17:13).
Ndivyo yule mama alivyofanya – alimpa KWANZA MUNGU kwa kupitia mtumishi wake. Mungu akambariki yule mama kwa ukarimu na utoaji wake wakati alipokuwa na upungufu. "Lile pipa la unga HALIKUPUNGUKA, wala ile chupa ya mafuta HAIKUISHA sawasawa na NENO LA BWANA alilolinena kwa kinywa cha Eliya" (1Wafalme 17:16).
Katika hali ya upungufu ulionao, usiwe mchoyo bali endelea kumtolea Mungu, naye atakubariki na kukufanikisha. Na hii itaonyesha ni kwa kiasi gani unamtegemea Mungu wako na Neno lake.
Lazima ufahamu ya kuwa Yesu Kristo anaangalia sana jinsi tutoavyo. Siku moja akiangalia jinsi watu watoavyo fedha; "Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la Hazina; maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia" (Marko 12:43-44). Soma na kuyatafakari tena maneno hayo ya Yesu Kristo, halafu jiangalie jinsi utoavyo. Huyu mjane hakuwa na mali ya kutosha alikuwa maskini, lakini bado aliendelea kumtolea Mungu! Je wewe una la kujitetea katika kutomtolea Mungu wakati wa upungufu wako?

Weka hazina yako mbinguni
Yesu Kristo alisema;"Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo,na wezi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wezi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako" (Mathayo 6:19 – 21).
Utoaji wako utaonyesha kama moyo wako uko kwa Yesu au unaitegemea dunia. Moyo wako ukimtegemea sana Yesu, utatoa zaidi kwa ajili ya kazi ya Mungu kuliko mahali pengine. Mkristo anapopoa kiroho, utoaji wake HASA kwa kazi ya kuhubiri injili nao unapungua. Hata hivyo Biblia inatuambia katika siku za mwisho upendo wa wengi utapoa.
Mtolee Mungu zaka na dhabihu (matoleo) bila kuchoka, nawe utakuwa umeweka hazina yako mbinguni – mikononi mwa Mungu – ambamo wezi hawawezi kukuibia. Naye Bwana atakurudishia mara nyingi zaidi. Mradi mzuri na wenye uhakika wa mavuno kwa Mungu na kwako wakati wa hali ngumu ya uchumi ni mradi wa kuhubiri injili. Kwa hiyo siku zote hakikisha umeweka kiasi fulani katika mradi wa kuhubiri injili.
Dumu katika maombi
Hili ni muhimu sana. Kwa kuwa wakristo wengi wakiwa katika hali ya ugumu wa maisha na uchumi, wanapoa katika maombi – na wanakumbwa na majaribu ambayo mara nyingi yanachafua ushuhuda wao. Soma Luka 21:36, Mathayo 24:42 – 51 na Mathayo 26:41. Kwa hiyo dumu katika maombi, usikate tamaa, hata wakati wa hali ngumu kiuchumi kwa upande wako – bado zidi kudumu katika maombi.