Friday, July 6, 2012
usajili unaendelea
http://www.bbc.co.uk/sport/0/football/gossip/
LIGI MBALI MBALI ZA NCHI DUNIANI ZINAENDELEA KUFANYA USAJILI WA WACHEZAJI WAPYA
Sunday, April 22, 2012
MAN UNITED YAVUTWA, MAN CITY YACHANJA MBUGA
TIME YA MANCHESTER UNITED LEO IMEVUTWA SHATI BAADA YA KULAZIMISHWA KUTOKA SARE YA 4 KWA 4 KATI YAKE NA EVERTON, MPINZANI WAKE KATIKA MBIO ZA UBINGWA MAN CITY IMEIBUGIZA WOLVE KWA JUMLA YA MAGOLI 2 kufuatia kazi nzuri ya nasri na aguelo sasa mahasimu hao wanapishana kwa point 3 tu ambapo mchezo unaofuata utawakutanisha wao wenyewe tarehe 30 april
http://www.bbc.co.uk/sport/0/football/17718140
http://www.bbc.co.uk/sport/0/football/17718154
WEEKEND LEO "KIGAMBONI"
Wakati watanzania kote nchini wakiwa wamegubikwa na tetesi za kujiuzuru kwa mawaziri sita, shughuli za starehe katika jiji la Dar es salaam ziliendelea kama kawaida. hapa kamera yetu ilivinjari viwanja vya kigamboni katika maeneo mbalimbali
Friday, April 6, 2012
Sunday, April 1, 2012
CHADEMA YASHINDA UBUNGE ARUMERU
hot nuuuuuuz: CHADEMA YASHINDA KITI CHA UBUNGE ARUMERU MASHARIKI, MATOKEO YATANGAZWA ASUBUHI HII
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi58_eY5OBEEC45O7mX9dGMOuHoHYKtPWxUyp9mNTzJJCZ1VZXnbxGyJhnH2ow3e9eR1VnuwWNY-Ph9Mace56znZntrHNbMZS1PQOcQQnwYqTrOTAhgSkyylR1ExTn976UopVI4SAV_kTk/s640/jo.jpg
Mbunge mteule wa Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nasari akiongea
baada ya kutangazwa kuwa mshindi asubuhi hii huko Arumeru
Matokeo ya kura za Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki yametangazwa sasa hivi na Msimamizi wa Uchaguzi na Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Bw Gracias Kagenzi amemtangaza mgombea wa CHADEMA Bw Joshua Nassari kuwa mshindi baada ya kupata kura 32,972 dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka CCM Bw Sioi Sumari aliyepata kura 26,757
Matokeo kwa Vyama vingine sita vilivyoshiriki ni kama ifuatavyo
DP -77
NRA - 35
AFP - 139
UPDB - 18
TLP - 18
SAU - 22
Kwa mujibu wa Bw Kagenzi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na aliojitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696 ambapo kura halali zilikuwa 60,038 na zilizoharibika ni kura 661.
Wakati huo huo, habari kutoka Mwanza zinasema CHADEMA kimeshinda katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kirumba mkoani Mwanza.
Msimamizi wa uchaguzi huo, Bw. Aloyce Mkono, amemtangaza kuwa mshindi mgombea wa Chadema Mh Dany Kahungu kwa kura 2,938 dhidi ya mgombea wa CCM Mh Jackson Masamaki aaliyepata kura 2,131.
Wagombea wengine walioshindwa vibaya katika uchaguzi ni pamoja na Mh Haji Issa wa CUF aliyepata kura 184, Mh Kasala Muhana wa UDP amepata kura 7 na Mh Athuman Jumanne wa NCCR Mageuzi aliyeambulia 0 katika uchaguzi huo .
Msimamizi huyo alisema kuwa uchaguzi huo umefanyika katika hali ya amani na utulivu,na kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo na kuonyesha utulivu mkubwa wakati wa uchaguzi na zoezi la kutangazwa kwa matokeo.
Kwa hisani ya Michuzi Blog
Sunday, March 25, 2012
SIMBA UWANJANI TENA LEO KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
Timu ya Simba ya Tanzania itachuana na wawakilishi kutoka Algeria timu ya ES Satif katika mashindano ya kombe la wawakilishi hatua ya kwanza. mchezo huo utachezwa katika uwanja wa taifa kuanzia saa 9 alasiri. makocha wa timu zote mbili wamejigamba kuibuka na ushindi. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki wawakilishi pekee wa Tanzania Simba spoti klabu.
Friday, March 23, 2012
IFAHAMU SIMBA SPORT CLUB
SIMBA SC: Imetoka wapi?
NCHINI Tanzania, Simba ni jina kubwa kuliko kinywaji cha Cocacola. Ni miongoni mwa timu mbili zenye washabiki wengi zaidi si tu nchini humu, lakini katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki.
Ina majina mbalimbali ya utani kama vile Wekundu wa Msimbazi na Lunyasi na ina makao yake makuu katika mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Timu hii ilianzishwa mwaka 1936 jijini Dar es Salaam ikitumia jina la Queens lakini baadaye lilibadilisha jina na kuitwa Eagle kabla ya kubadilishwa tena na kuitwa Sunderland –jina lililotumika hadi mwaka 1971 ambapo ndipo jina la Simba Sports Club lilianza kutumika.
Ingawa tayari jina la Sunderland lilikuwa maarufu na kubwa tayari, lilibadilishwa na kuwa Simba; jina la mfalme wa msituni, ikiwa ni kutokana na pendekezo la aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, ambaye alishauri jina libadilishwe wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la makao makuu ya klabu mtaa wa Msimbazi.
Katika majina yaliyopendekezwa, jina la Simba lilikubaliwa zaidi na wengi na likaamuliwa kutumika kuanzia mwaka huo wa 1971.
Simba ilianza kutanuka zaidi wakati ikitumia jina la Sunderland. Ilikuwa na matawi yake katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ambapo ziliundwa timu zilizokuwa na kazi ya kupika wachezaji waliokuja kuchezea Simba baadaye.
Miongoni mwa timu hizo ni Morning Stars, Canada Dry, Liverpool na Ilala Stuff, ambako huko mchezaji aliyeonekana kukomaa alipelekwa kukipiga Sunderland.
Majina Maarufu
Zaidi ya jina la Simba, kama zilivyo timu nyingine maarufu duniani, timu hii pia hutambulika kwa majina mengine tofauti.
Hufahamika pia kwa jina la Wekundu wa Msimbazi, Taifa Kubwa na Lunyasi.
Jezi
Klabu ya Simba huvaa jezi nyekundu katika uwanja wake wa nyumbani na nyeupe inapokuwa ugenini. Wakati mwingine huvaa jezi zenye mchanganyiko wa rangi hizo mbili.
Uongozi
CHOMBO cha juu kabisa cha maamuzi katika klabu ya Simba ni Mkutano Mkuu wa Wanachama ambao ndiyo huchagua viongozi wa klabu.
Shughuli za kila siku husimamiwa na Kamati ya Utendaji ingawa sekretarieti ndiyo huzifanya kwa maelekezo ya kamati. Kiongozi wa Kamati ya Utendaji ni Mwenyekiti wa klabu na yeye pamoja na kamati yake yote inawajibika kwa wanachama moja kwa moja.
Safu ya Uongozi kwa Sasa
Mwenyekiti
Ismail Aden Rage
Makamu Mwenyekiti
Geofrey Nyange
Katibu Mkuu
Evodius Mtawala
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji
Joseph Itang’are
Said Pamba
Daniel Manembe
Francis Waya
Sued Mkwabi
Ibrahim Masoud
Zakaria Hans Pope
NB: Kwa nyadhifa zao, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa nyadhifa zao
MATAJI
KATIKA historia yake, Simba imetwaa jumla ya mataji 36, yakiwamo 17 ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, katika michuano mbalimbali ambayo imeshiriki tangu ianzishwe.
Mataji hayo yanajumuisha ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi ya Muungano, Kombe la Nyerere, Kagame na Kombe la Mapinduzi.
Haya Ndiyo Mataji Yaliyochulikuwa na Simba
UBINGWA WA LIGI KUU:
1965, 1966, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004 na 2007 (Ligi Ndogo) na 2010.
LILILOKUWA KOMBE LA NYERERE:
1984, 1995 na 2000
LILILOKUWA KOMBE LA MUUNGANO:
1993, 1994, 1995, 2001, na 2002
KOMBE LA TUSKER:
2001, 2002, 2003 na 2005
KOMBE LA CAF:
Ilifika fainali mwaka 1993
KOMBE LA KAGAME:
1974, 1991, 1992, 1995, 1996 na 2002
LIGI YA MABINGWA AFRIKA:
Kucheza hatua ya makundi 2003
KLABU BINGWA AFRIKA:
Kucheza Nusu Fainali 1974
KWA TAARIFA ZAIDI TEMBELEA TOVUTI HII http://simba.co.tz/club-info
WANYARWANDA KUCHEZESHA MECHI YA SIMBA NA ES SATIF
HUDU Munyemana ametangazwa kuwa mwamuzi wa pambano la Kombe la CAF baina ya Simba na ES Setif kutoka Algeria lililopangwa kufanyika Machi 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), mwamuzi wa kati katika pambano hilo atakuwa Hudu Munyemana kutoka Rwanda ambaye atasaidiwa na Felicien Kabanda na Theogene Ndagijimana huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Edouard Bahizi.
Kwa mujibu wa CAF, Kamisaa wa pambano hilo atakuwa ni Felix Tangawarima kutoka Zimbabwe na waamuzi hao watakiwa kuwasili nchini siku mbili au tatu kabla ya mechi kulingana na usafiri ulivyo.
Mwamuzi Munyemana amewahi kuchezesha mechi mbalimbali za Simba katika Kombe la Kagame na pia mwaka juzi alikuwa mwamuzi katika mchuano wa Kombe la CAF baina ya Doula ya Cameroon na ES Entente ya Algeria inayocheza na Simba.
http://simba.co.tz/sites/default/files/imagecache/news_full/news/huuudu.JPG
http://simba.co.tz/news/club-news/2012/03/17/warwanda-kuchezesha-mechi-ya-simba-na-es-setif.html
PRIMIER LEAGUE THIS WEEKEND
LIGI YA UINGLEZA ITAENDELEA TENA KESHO KWA MECHI NNE AMBAPO CHELSEA WATAIKARIBISHA SPURS SAA 9.45 ALASIRI BAADAYE SAA 12.OO JIONI ARSENAL WATAIKARIBISHA ASTON VILLA, LIVER POOL WATAKUWA WENYEJI WA WIGANI NA BOLTON WATAIKARIBISHA TIMU ILIYOZINDUKA YA BLACKBURN
ZAIDI TEMBELEA TOVUTI IFUATAYO
http://www.bbc.co.uk/sport/football/premier-league/fixtures
Friday, March 16, 2012
RATIBA LIGI YA MABINGWA ULAYA UEFA HATUA YA NANE BORA HADHARANI
Timu ya Chelsea ya England itakutana na Benifica ya Ureno katika hatua ya nane bora, ratiba kamili ya mechi hizo iliyotolewa leo inaonesha kama ifuatavyo:-
CHAMPIONS LEAGUE FIXTURES
Tuesday 27 March: Benfica v Chelsea, Apoel v Real Madrid
Wednesday 28 March: Marseille v Bayern Munich, AC Milan v Barcelona
Tuesday 3 April: Bayern Munich v Marseille, Barcelona v AC Milan
Wednesday 4 April: Chelsea v Benfica, Real Madrid v Apoel
Tuesday 17 April: Marseille or Bayern Munich v Apoel or Real Madrid
Wednesday 18 April: Benfica or Chelsea v AC Milan or Barcelona
Tuesday 24 April: AC Milan or Barcelona v Benfica or Chelsea
Wednesday 25 April: Apoel or Real Madrid v Marseille or Bayern Munich
Saturday 19 May: Final
Wednesday, March 14, 2012
Anzhi Makhachkala chasing Messi, Ronaldo and Bendtner,
TRANSFER GOSSIP
Germany international striker Lukas Podolski, 26, has had a medical paving the way for his £10m move from Cologne to Arsenal.
Sun
Full story: Daily Star
Lille midfielder Eden Hazard says he was "excited" to hear of Sir Alex Ferguson's scouting trip to see him, and would be interested in joining Manchester United.
Full story: The Telegraph
Blackburn Rovers manager Steve Kean says he has not given up hope of keeping 21-year-old winger Junior Hoilett, who is out of contract in the summer.
Full story: Lancashire Telegraph
Russian side Anzhi Makhachkala are ready to offer striker Nicklas Bendtner a route out of Arsenal in the summer, with Sunderland unlikely to make his loan permanent.
Full story: Metro
Liverpool and Arsenal have both joined the race to sign Spanish winger Jose Manuel Jurado, who currently plays for Schalke.
Full story: Footy Latest
Roberto Carlos hopes to sign both Cristiano Ronaldo and Lionel Messi for Russian side Anzhi Makhachkala.
Full story: Marca (in Spanish)
Steve Bruce set to open talks with Wolves
Bruce was sacked as Sunderland manager in November
Napoli have told Chelsea and Manchester City that they will have to pay 'crazy' money to sign Uruguayan striker Edinson Cavani.
Full story: the Sun
OTHER GOSSIP
Former Sunderland boss Steve Bruce is ready to resume talks with Wolves about becoming their next manager.
Full story: Daily Mail
Jack Wilshere has told his Arsenal team-mates that he could return to action from an ankle injury at the end of this month.
Full story: Daily Express
Carlos Tevez could remain at Manchester City beyond the end of the season after impressing with his attitude and desire to regain match fitness since returning to the club in February.
Full story: the Guardian
Former Arsenal star Ian Wright believes son Shaun Wright-Phillips and his Queens Park Rangers team-mates will be relegated and will be lucky to get a point from their remaining 10 league matches.
Daily Mirror
Full story: London Evening Standard
Relegation would hit QPR hard financially because most of this season's big-name arrivals signed lucrative deals which do not include relegation clauses.
Full story: the Mirror
Chelsea interim coach Roberto di Matteo believes Fernando Torres has failed to score goals because he has a "psychological problem".
Full story: Metro
Real Madrid star Cristiano Ronaldo has ruled out a return to England instead insisting he will stay with the Spanish club.
Full story: talkSPORT
England fans travelling to Ukraine for Euro 2012 are being urged to make sure they are vaccinated against measles after an outbreak of the disease.
Full story: Daily Mail
AND FINALLY
Tottenham playmaker Rafael van der Vaart has posted footage on Twitter of his five-year-old son Damian showing some impressive football skills.
Tuesday, March 13, 2012
ROSISKY SIGN NEW DEAL FOR ARSENAL
Rosisky amesaini mkataba mpya zaidi ingia hapa http://www.bbc.co.uk/sport/0/football/17340418
WAKATI HUO HUO ARSENAL JANA IMEPATA USHINDI WA 2 KWA 1 DHIDI YA NEWCASTLE zaidi ingia hapa http://www.bbc.co.uk/sport/0/football/17254808
YANGA YAKUMBANA NA RUNGU LA TFF
Timu ya yanga imeadhibiwa na shirikisho la soka la Tanzania kufuatia tafrani ya jumamosi ambapo wachezaji wake walimpiga refa wa pambano hilo. picha ifutayo inaonesha sakata hilo
wachezaji wa yanga wakimpiga refa Nkongo Jumamosi iliyopita.zaidi bonyeza hapa http://www.mwanaspoti.co.tz/wcreadnews.php?id=10962
Saturday, March 10, 2012
NENO LA UZIMA
![]() |
||
|
||
![]() |
![]() |
![]() |
SOMO: IKIMBIENI ZINAA
Wiki ya Kwanza
Je! Unaamini ya kuwa Mungu anaweza kusema na watu kwa njia ya ndoto? Najua ni
rahisi kuamini kuwa Mungu alisema na watu zamani kwa njia ya ndoto kama tunavyosoma katika Biblia; lakini je! Unaamini ya
kuwa Mungu anasema na watu kwa njia ya ndoto siku hizi?
Najua kuna watu wanaoamini na wengine hawaamini. Sijui wewe uko upande gani.
Lakini nataka nikueleze hivi; Kufuatana na Biblia kuna ndoto za aina tatu;
(a)
Kuna ndoto kutoka kwa
Mungu. Soma kitabu cha Hesabu 12:6, na Yoeli 2:28.
(b)
Kuna ndoto zinakuja kwa
sababu ya shughuli nyingi. Soma kitabu cha Mhubiri 5:3.
(c)
Kuna ndoto za uongo
zinazotoka kwa shetani aliye baba wa uongo. Soma kitabu cha Yeremia 23:52 na
Yohana 8:44.
Unaweza kutofautisha kwa namna gani tofauti iliyopo kati ya hizi
ndoto? Na utajuaje kuwa ndoto uliyoiota imetoka kwa Mungu? Kila ndoto lazima
ipimwe na Neno la Mungu. Ikiwa imetoka kwa Mungu, ni lazima utakuta neno la
Mungu ambalo linaeleza maana yake. Mara nyingine ndoto toka kwa Mungu huja
kama fumbo; lakini Roho Mtakatifu ajuaye kuyafumbua mafumbo ya Mungu (1
Wakorintho 2:10,11), atalifunua fumbo hilo
kwa kukuonyesha neno la Mungu linalofanana na ndoto hiyo.
Si busara kuzikubali ndoto zote unazoota bila ya kuzipima katika Neno
la Mungu. Na pia si busara kuzikataa ndoto zote bila kuzipima katika Neno la
Mungu.
Nimeona nianze kwa kukueleza haya kwa kuwa chanzo cha kuandika kitabu
hiki, ni ujumbe wa Mungu ulionijia kwa njia ya ndoto.
Ndoto yenyewe ilikuwa hivi: Niliona katika ndoto mtu mmoja mkristo,
tena aliyeokoka akifanya mambo ya zinaa bila hata kuogopa. Na wakati
nilipokuwa nikimtazama na kusikitika, nikasikia sauti toka juu yangu ikisema;
“ NITACHUKULIANA MPAKA LINI NA MWANADAMU AFANYAYE MAMBO YA JINSI
HIYO?” Baada ya kusikia maneno
hayo nikaamka.
Wakati huo ulikuwa ni alfajiri, na ndoto hiyo ilinipa maswali na
masononeko mengi moyoni mwangu. Na niliamua kumshirikisha mke wangu Diana juu
ya ndoto hiyo.
Mke wangu akaniuliza; “ Maana yake nini ndoto hiyo?”
Nilipotaka kufungua kinywa ili nimjibu uchungu mzito ulijaa moyoni
mwangu, nikasikia kuugua rohoni, na mara nikaanza kulia!
Unaweza ukaniuliza; “Mwakasege kwa nini ndoto ikulize machozi?”
Hili ni swali zuri. Hata mimi nilijiuliza kwa nini nitoe machozi kwa
ajili ya ndoto. Lakini baada ya kulifuatilia jambo hili katika maombi na
katika neno la Mungu nilielewa sababu yake.
Je! Unafahamu matokeo ya Mungu kusema “Nitachukuliana mpaka lini na
mwanadamu afanyaye mambo ya jinsi hiyo?” Ukisikia maneno ya jinsi hii
ujue Mungu amekasirika na kuna maangamizo mbele.
Hebu na tulifuatilie jambo hili katika biblia ili tulione uzito wake.
Nuhu na
Gharika.
Ni vizuri ukumbuke ya kuwa gharika ilitokea wakati wa Nuhu kwa sababu
ya zinaa.
“Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike
walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliona hao binti za wanadamu – ni wazuri;
WKAJITWALIA WAKE WO WOTE WALIOWACHAGUA. Bwana akasema, ROHO YANGU
HAITASHINDANA NA MWANADAMU MILELE, kwa kuwa yeye ni nyama; basi siku zake
zitakuwa mia na ishirini. Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile,
tena baada ya hayo, wana wa Mungu WALIPOINGIA kwa binti za wanadamu, wakazaa
nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa. BWANA AKAONA
YA KUWA MAOVU YA MWANADAMU NI MAKUBWA DUNIANI NA KWAMBA KILA KUSUDI ANALOWAZA
MOYONI MWAKE NI BAYA TU SIKU ZOTE. BWANA AKAGHAIRI KWA KUWA AMEMFANYA
MWANADAMU DUNIANI, AKAHUZUNIKA MOYONI. Bwana akasema, Nitamfutilia usoni pa
nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambulisho na ndege wa angani; kwa maana
naghairi ya kwamba nimewafanya. Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana.” (Mwanzo 6:1-8)
Ukiendelea kufuatilia habari hii katika Biblia utaona ya kuwa baada ya
gharika ya maji walibaki watu nane tu! Wanadamu wengine wote waliangamia kwa
sababu ya nini? – Zinaa!
Sodoma na Gomora
Wasomaji wa Biblia wanafahamu kabisa ya kuwa miji ya Sodoma na Gomora
iliteketezwa kwa moto baada ya Mungu kuihukumu kwa sababu ya uasherati
uliokuwa ukifanyika ndani yake. Soma Mwanzo 19:4-25.
Na pia katika kitabu cha Yuda 1:7 tunasoma hivi: -
“Kama vile Sodoma na Gomara, na miji iliyokuwa kando kando, waliofuata
UASHERATI kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya
asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.”
Ikiwa Mungu aliwatenda hivi watu wa Sodoma na Gomora, ni kitu gani
kinamfanya mwanadamu wa siku hizi adhani ya kuwa Mungu amebadilika juu ya
kuadhibu wale wote wafanyao uasherati? Katika miji hiyo miwili ni watu watatu
tu waliobaki – Lutu na watoto wake wawili! Wanadamu wengine waliokuwa katika
miji hiyo waliteketezwa kwa sababu ya nini – Zinaa!
Kuhani
Eli na watoto wake.
“Basi
Eli alikuwa mzee sana, naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe
waliwatenda Waisraeli; na jinsi WALIVYOLALA NA WANAWAKE waliokuwa wakitumika
mlangoni pa hema ya kukutania.” (1Samweli 2:22)
Hata
baada ya baba yao kuwaonya hawakusikia, na matokeo yake ni:-
1.
Watoto hao wawili, Hofni
na Finehasi walikufa wote siku moja;
2.
Wana wa Israeli walipigwa
na adui zao Wafilisti na Sanduku la agano likatekwa;
3.
Kuhani Eli alikufa.
Yote haya yalitokea katika taifa ambamo watoto wawili wa kiongozi
waliuwa wakifanya mambo ya Zinaa bila hata kujali maonyo.
Je! Bado unajiuliza kwa nini nilitoa machozi baada ya kusikia sauti ya
Mungu katika ndoto ikisema “Nitachukuliana mpaka lini na mwanadamu
afanyaye mambo ya jinsi hiyo?”
Siku za Mwisho.
“Lakini
ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana
watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu,
wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio
safi…….Kwa maana katika hao wamo wale WAJIINGIZAYO KATIKA NYUMBA ZA WATU, NA
KUCHUKUA MATEKA WANAWAKE WAJINGA WENYE MIZIGO YA DHAMBI, waliochukuliwa na
tamaa za namna nyingi. (2 Timotheo 3:1,26).
Je! Siku hizi wanawake hawatekwi mateka na wanaume ili wafanye mambo
ya zinaa? Vishawishi vimekuwa vingi, na wanawake wengi wameanguka katika
mitego hiyo ya kupenda fedha na anasa, na mwisho wake ni kufanya uzinifu.
Kwa nini wanaume wengi wamekosa akili juu ya jambo hili. Ni kitu gani
kimewapofusha macho wasione ya kuwa uzinifu ni mbaya? Biblia inasema; “Mtu
aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomangamiza nafsi
yake.” (Mithali 6:32)
Ni dhahiri ya kwamba palipo na zinaa pana uharibufu, na wengi
wanaangamia. Na nataka nikuambie ya kuwa Roho Mtakatifu akikuwekea mzigo huo
ndani yako na kuliona jambo hili jinsi linavyomhunish Mungu, hakika
hutatulia; na hapana budi macho yako yatajaa machozi juu ya kizazi hiki
kinachojiangamiza chenyewe kwa sababu ya zinaa.
Sababu ya mambo haya
kuandikwa.
Mambo haya hayakuandikwa kwa bahati mbaya, wala si kwa ajili ya
kuonyesha historia ya watu Fulani tu. Bali
yaliandikwa kwa kusudi maalumu na muhimu.
“Basi
mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili KUTUONYA SISI,
tuliofikiriwa na miisho ya zamnai – Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na
aangalie asianguke.” (1 Wakorintho 10:11,12)
Na mimi nimependa kuyaonyesha wazi ili tujue tunapozungumza juu ya
zinaa, Bwana Mungu anakuwa na mawazo gani juu yake. Nafahamu si mara kwa mara
hata katika mahubiri na mafundisho, jambo hili huguswa kwa undani. Lakini
naona umefika muda wa kulichambua jambo hili kwa undani zaidi.
Hali ilivyo sasa.
Mtu mmoja aliniuliza “Je, mtu aliyeokoka anaweza kufanya mambo ya
uasherati – je, anaweza kuzini?”
Nikamwambia, “Mtu aliyeokoka hatakiwi kufanya mambo ya uasherati, kwa kuwa
kufanya hivyo ni dhambi, lakini asiposimama katika Kristo sawasawa anaweza
kuzini.”
Halafu huyo mtu akaendelea kuuliza, “Je, Unamfahamu Fulani? (Akamtaja jina
lake).
“Ndiyo namfahamu.” Mimi nilimjibu, na nikaendelea kusema; - “ kuwa ni mtumishi wa
Mungu, ingawa sijamwona muda mrefu umepita sasa”.
Ndipo akasema, “Unafahamu ya kuwa alianguka na akazini na msichana Fulani
(akamtaja jina lake) ambaye pia ameokoka, na sasa yule msichana amezaa?”
Mimi nilishangaa na kushutushwa na habari hizo. Nikamuuliza “Unasema kweli
ndivyo ilivyotokea?”
Akasema, “Ndiyo”
Ndipo Roho wa Mungu aliponikumbusha ndoto ile aliyonipa. Katika ujumbe ule wa
ndoto, Mungu alinionyesha mkristo aliyeokoka akifanya mambo ya uasherati.
Kwa mtu asiyeokoka siwezi kushangaa akifanya uzinzi, kwa kuwa bado yuko
gizani, na yuko chini ya mkuu wa giza,
ibilisi – kwa hiyo anaweza kufanya lo lote lile. Ndiyo maana mtu anaweza
kusema yeye ni mkristo, na huku anazini mara kwa mara.
Mkristo wa kweli aliyeokoka hatakiwi kuzini, wala kushindwa na dhambi. Kwa
nini? Kwa kuwa ndani yake ametengwa mbali na dhambi, na amepewa ushindi juu
ya dhambi.
Ushindi dhidi ya dhambi
Uhusiano wako na dhambi unakuwaje baada ya kuokoka, na kufanyika kiumbe kipya
ndani ya Kristo? Watu wengi wakiisha-okoka, huwa bado wanasumbuliwa na
kuanguka katika dhambi mara kwa mara, na hasa katika zinaa. Na hii inatokea
kwa kuwa hawapati mafundisho ya kutosha ya neno la Mungu juu ya jinsi
wanavyotakiwa kuenenda katika maisha mapya waliyopita.
Kaini aliambiwaje na Mungu? Bwana alimwambia hivi; “ kama
ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea
mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa UISHINDE” (Mwanzo 4:7)
Na ndivyo ilivyo hata sasa. Bado tumo ulimwenguni humu, ingawa aliyezaliwa
mara ya pili yeye si wa ulimwengu huu (Yohana 17:16). Lakini kwa kuwa
bado tumo katika ulimwengu uliojaa dhambi inayotutamani kila siku, na
tusije tukajisahau. Inatupasa tuishinde.
Yanenaje maandiko?
Imeandikwa
katika kitabu cha (Warumi 6:12-14)
“Basi,
dhambi isitawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na mauti, hata mkazitii
tamaa zake; wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa
dhambi, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na
viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi, bali jitoeni wenyewe kwa
Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za
haki. Kwa maana DHAMBI HAITA WATAWALA NINYI, kwa sababu hamuwi chini ya
sheria, bali chini ya neema”.
Ikiwa
tunaambiwa ya kuwa “Dhambi haitawala ninyi …….” inakuwaje basi wengine
wanatawaliwa nayo? Inakuwaje mtu wa Mungu, aliyepakwa mafuta kwa Roho
Mtakatifu aanguke katika zinaa? Kitu gani kinampofusha macho ya rohoni?
Je! Ni
halali kwa mtu anayekaa ndani ya Kristo kutenda dhambi?
Yanenaje
maandiko?
“Kila
akaaye ndani yake (Yesu Kristo) HATENDI DHAMBI; kila atendaye dhambi
hakumwona yeye, wala hakumtamua….atendaye dhambi ni wa ibilisi; kwa kuwa
ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu
alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.” (1 Yohana 3:6,8)
Je!
Unaona maneno haya yalivyoandikwa kwa ajili yetu? Sidhani kama unapenda tena
kuwa Ibilisi kwa kuwa “Apendaye dhambi ni wa Ibilisi” Kwa hiyo ni
muhimu ujilinde usitende dhambi.
Tena imeandikwa:
“Kila
mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu UZAO WAKE WAKAA NDANI
YAKE; WALA HAWEZI KUTENDA DHAMBI KWA SABABU AMEZALIWA KUTOKANA NA MUNGU.” (1 Yohana 3:9)
Ikiwa
umezaliwa mara ya pili kwa Roho wa Mungu, ujue hakika UZAO WA MUNGU unakaa
ndani yako. Na uzao huu wa uungu ni Mtakatifu, na unakaa ndani yake bila
kutangatanga unakuwezesha kuishi bila kutenda dhambi.
Je! Si
jambo la kumshukuru Mungu hilo.
Si kwamba anatuambia tusitende dhambi bila kutupa njia ya kutusaidia. Anajua
sisi wenyewe hatuwezi kuishinda dhambi, BALI YEYE AKIKAA NDANI YETU NA SISI
NDANI YAKE TUNAWEZA KUISHI KATIKA USHINDI DHIDI YA DHAMBI NA MITEGO YAKE
YOTE.
Tena
imeandikwa;
“Twajua
ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu HATENDI DHAMBI; bali yeye aliyezaliwa
na Mungu HUJILINDA, wala yule mwovu HAMGUSI.” (1 Yohana 5:18)
Ee, mtu
wa Mungu, jilinde basi kwa kuwa umezaliwa na Mungu, kwa nini tamaa ya
uasherati ikusonge? Je?! umesahau ni uzao wa namna gani ulio ndani yako?
Ni
kweli kwamba mtu akitenda dhambi na akatubu, Bwana atamsamehe, (1 Yohana
1:9). Lakini hatutakiwi kutenda dhambi. Ndiyo maana imeandika; “Watoto
wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba MSITENDE DHAMBI”…. (1 Yohana
2:1)
Sasa
naona unaweza kuelewa kwa nini inashtusha na kusikitisha unaposikia mtu wa
Mungu ameanguka katika dhambi ya zinaa. Ikiwa maisha ya wokovu yatakuwa ni ya
kuanguka na kusimama, halafu tena kuanguka na kusimama mara kwa mara; basi
ina maana ya kuwa ushindi wa kutosha haukupatikana pale msalabani.
Lakini
nataka nikuambie hivi, ushindi kamili ulipatikana pale msalabani bila
kubakiza kitu! Ndiyo sababu Yesu Kristo alikuwa na ujasiri wa kusema ‘IMEKWISHA’
pale msalabani.
Tunachotakiwa
kufanya ni kuwa watendaji wa neno; na ndiyo ushindi huo utadhihirika katika
maisha yetu. Usidhani ya kuwa mapokeo ya wanadamu yanaweza kukusaidia
kuishinda dhambi; la hasha! Yesu Kristo peke yake akikaa ndani ya
moyo wako, na neno lake
ukilitii, ndiko utapata
ushindi halisi na halali dhidi ya dhambi.
Swali la kujiuliza
Idadi
ya wakristo waliookoka wanaoanguka katika dhambi ya zinaa inaongezeka siku
baada ya siku. Na wengine wameanguka dhambini moja kwa moja, hata haja ya
kutaka kusimama upya katika Bwana imepotea. Wanaona aibu! Na wengine
wanaanguka na kusimama, halafu tena wanaanguka na kusimama. Na kwa sababu
hiyo hawana ushuhuda mzuri mbele za watu. Hawaaminiki tena.
Lakini
je! Unadhani Mungu atatuambia tuishinde dhambi wakati anafahamu ya kuwa
hatuna uwezo huo? La hasha! Mungu wetu tunayemwamini katika Kristo Yesu si
dhalimu kiasi hicho.
Jambo
ninalofahamu ni kwamba ametuambia tuishinde dhambi kwa kuwa ndani yetu sisi
tuliompokea, ametupa UWEZA WA KUISHINDA DHAMBI – kwa namna gani?
“Kwa
sababu UZAO WAKE WAKAA NDANI YAKE (YETU) WALA HAWEZI (HATUWEZI) KUTENDA
DHAMBI KWA SABABU AMEZALIWA (TUMEZALIWA) KUTOKANA NA MUNGU”.(1Yohana 3:9)
Uzao
wako si uzao wa kuanguka dhambini, bali ni uzao wa kushinda dhambi, kwa kuwa
Kristo anakaa ndani yako!
|
|
![]() |
SOMO: IKIMBIENI ZINAA
Wiki ya Pili
MKRISTO ANAANGUKAJE KATIKA ZINAA?
Kila mara nilipopata habari za watu wa Mungu walioanguka katika dhambi ya
zinaa nilikuwa najikuta najiuliza swali hili, “Hivi wanapataje ujasiri wa
kutenda tendo hilo?”
Akili yangu ilikuwa inakataa kabisa kuamini kuwa mtu aliyeokoka (na wakati
mwingine amejazwa Roho Mtakatifu) anaweza kuanguka kwenye dhambi ya zinaa.
Lakini hata hivyo bado nikawa naendelea kusikia majina ninayoyafahamu ya watu
wa Mungu waliookoka waliokubwa na dhambi ya zinaa.
“Wanafanyaje
mpaka wanaanguka katika zinaa”? Hili swali lilinisumbua kwa muda mrefu. Na siku moja nilikuwa
nyumbani kwangu nikijiuliza swali hili moyoni, nikasikia Roho Mtakatifu
akiniuliza ndani ya moyo wangu, akisema, “ Kwani Daudi aliangukaje? Je!
Umesahau ya kuwa naye alikuwa mtu wangu, mtumishi wangu niliyempaka mafuta?
Niliposikia swali hili, nilichukua biblia na kusoma maneno yanayoeleza
kuanguka kwa Mfalme Daudi katika dhambi ya zinaa na mke wa mmoja wa askari
wake.
Mambo niliyoyasoma yalinifungua macho kuona jinsi ambavyo hata hivi leo watu
wa Mungu wanavyoanguka au wanavyoweza kuanguka katika dhambi ya zinaa.
Chukua biblia yako na usome habari hizi katika 2 Samweli 11:1-27 na 2 Samweli
12:1-25.
Chanzo cha kuanguka kwa Mfalme Daudi katika dhambi ya Zinaa, ni KUTOKWENDA
VITANI PAMOJA NA ASKARI WAKE.
“Hata
ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Daudi
akampeleka Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote,
wakaangamiza wana wa Amoni, wakakuhusuru Raba. LAKINI DAUDI MWENYEWE AKAKAA
YERUSALEMU”. (2
Samweli 11:1)
Kama kiongozi wao, Daudi alitakiwa
kuongozana na watu wake vitani, lakini yeye aliamua kubaki Yerusalemu asiende
vitani, na akamtuma mtu mwingine amwakilishe. Na jambo hili lilimpa nafasi
nzuri sana
ibilisi ya kumpa Daudi kazi nyingine ya kufanya. Ni kazi gani hiyo?
“Ikawa
wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, AKATEMBEA JUU YA DARI ya jumba la
mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke ANAOGA; naye huyo mwanamke
alikuwa MZURI SANA WA KUPENDEZA MACHO”. (2 Samweli 11:2)
Ni kitu
gani kilimfanya Mfalme Daudi aamue kutembea juu ya dari ya jumba lake badala
ya kwenda vitani pamoja na watu wake? Na alipomwaona Bathsbeba, mkewe Uria
akioga alishindwa kujizuia, mwisho wake ni kuzini naye na huyo mama kupata
mimba!
Wakristo
wengi wamejikuta wameingia katika mtego wa zinaa kwa sababu ya kutokwenda ‘Vitani’
wakati wanapotakiwa kufanya hivyo. Vita tunavyovisema, si vita vya kimwili.
“Maana
ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili, maana
silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha
ngome; tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu
ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo”. (2 Wakorintho 10:3,4)
Na pia
imeandikwa; “ Kwa maana kushindani kwetu sisi si juu ya damu na nyama;
bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili juu ya majeshi ya pepo wabaya,
katika ulimwengu wa roho”. (Waefeso 6:11)
Ndiyo
maana Yesu Kristo alisema; “ Kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni;
roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.” (Mathayo 26:41)
Usipovipiga
vita katika maombi, inakuwa ni rahisi sana
kuangushwa na majaribu unapokutana nayo. Wakristo wakipoa katika maombi
inakuwa rahisi kuanguka katika dhambi, si katika zinaa peke yake, bali katika
mtego wowote ambao shetani anauweka mbele yao!
Kutokuwa
mwombaji, ni sawa na kutokwenda vitani na wenzako, kama
vile Mfalme Daudi alivyofanya.
Kwa
hiyo unaona ya kuwa ingawa Mfalme Daudi alikuwa mtu wa Mungu, mtumishi wake,
na mpakwa mafuta wake, alianguka katika zinaa. Na hata hivi leo kuna
wakristo, tena wameokoka, na kupakwa mafuta kwa Roho Mtakatifu, wanaonguka
katika dhambi ya zinaa. Kwa nini? Kwa kuwa hawavipigi vita vya kiroho na wenzao,
na wamepoa katika kumtumikia Bwana.
Je! Lutu aliangukaje?
Hili ni
swali ambalo Roho Mtakatifu aliniuliza baada ya kunieleza habari za Mfalme
Daudi. Ingawa Lutu alikuwa mtu wa Mungu, na licha ya kuwa alikuwa anabebwa
kwa maombi ya Ndugu yake Ibrahimu, bado alianguka katika zinaa.
Roho
Mtakatifu alikuwa anaendelea kunijibu swali nililokuwa najiuliza ya kuwa,
watu waliookoka wanaangukaje katika zinaa?
Habari
za kuanguka kwa Lutu zimeandikwa katika kitabu cha Mwanzo 19:30-38.
Lutu
alizini na watoto wake wawili wa kike baada ya kuleweshwa mvinyo.
Na
ukiisoma habari hii inasikitisha sana.
Shetani alipata nafasi ya kumwangusha Lutu si kwa sababu ya binti zake
kumlewesha mvinyo, bali kwa kuwa MKE WAKE HAKUWA PAMOJA NAYE. Unadhani mke
wake angekuwapo hawa watoto wangepata nafasi ya kumlaghai baba yao? Hapana! Kwa nini?
Kwa
maana “ Bwana ameumba jambo jipya duniani, mwanamke atamlinda mwanaume.”
(Yeremia 31:22)
Unaweza
kujiuliza ni kwa njia gani mke atalimnda mume wake. Kumbuka imeandikwa mke
mwenye busara, mtu hupewa na Bwana. Kazi moja ya busara iliyo ndani ya mke ni
kumlinda mume kutokana na mashambulizi ya Malaya!
Soma Mithali 2:11-22.
Hata
hivi leo ndoa ambazo mume na mke hawakai vizuri, huwa ni rahisi kwa wao
kuanguka katika dhambi ya zinaa hata kama
wameokoka. Na huu siyo ushuhuda mzuri.
Tunamshukuru
Mungu kwa wale ambao wamesimama katika ushuhuda ingawa ndoa zao zina
matatizo.
Jambo la kujifunza zaidi
Roho
Mtakatifu alipokuwa anaendelea kunifundisha akasema ndani ya moyo wangu hivi;
“Watu wengi wanadhani zinaa ni tendo la kimwili tu linalofanywa kati ya
mwanaume na mwanamke nje ya ndoa, lakinikuna namna zaidi ya moja unayoweza
kuanguka katika zinaa.”
Niliposikia
hivyo moyoni mwangu, niliichukua biblia na nikaanza kuisoma upya juu ya zinaa
na nikaona kuna namna nne ambazo zinaa inatajwa:-
1. KATIKA MWILI:
“….Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa
mwili. Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae
viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya Kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa
yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? …. Ikimbieni zinaa, kila
dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa
hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni
hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu
wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika
miili yenu.” (1
Wakorintho 6:13-20)
2. KUTAMANI KWA MACHO. Yesu Kristo alisema;
“Mmesikia kwamba imenenwa Usizini; lakini mimi nawaambia, kila mtu
AMTAZAMAYE MWANAMKE KWA KUMTAMANI, amekwisha KUZINI NAYE MOYONI MWAKE.” (Mathayo 5:27,28)
3. KUACHA MKE NA KUOA MWINGINE
Yesu Kristo alisema;
“Kila amwachaye mkewe na kuoa mke mwingine azini ……” (Luka 16:18)
4. KUOA ALIYEACHWA. Yesu Kristo alisema;
“Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; NAYE AMWOAYE YEYE
ALIYEACHWA NA MUMEWE AZINI.” (Luka 16:18)
Kila mtu na ajipime katika hayo; ikiwa umefanya mambo kama
hayo niliyoyataja, biblia inasema UMEZINI! Je
Hakuna waliokoka wanaofanya mambo ya jinsi hii? Wanaowaacha wake zao halali?
– Wanaooa walioachwa? – na wanaozini katika mwili?
|
|
![]() |
SOMO: IKIMBIENI ZINAA
Wiki ya Tatu
USHAURI WA BIBLIA JUU YA KUEPUKANA NA ZINAA
“Watu
wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa…..” (Hosea 4:6). Haya ni maneno ambayo Bwana
aliyanena kwa kutumia kinywa cha Nabii Hosea kwa watu wake, wana wa Israeli.
Lakini maneno haya yanatuhusu watu wake hata leo.
Watu wa
Mungu wengi sana
nyakati hizi wanaangamizwa kwa kukosa maarifa – maarifa juu ya mapenzi ya
Mungu. Na eneo mojawapo ambalo linaangamiza wengi ni eneo la uzinzi.
Kwa
kukosa mafundisho ya kutosha juu ya neno la Mungu juu ya kusimama katika
Kristo na kuepukana na zinaa, watu wa Mungu wengi wameanguka kiroho. Na
wengine wanaishi maisha ya kuanguka na kusimama kuanguka na kusimama, - kitu
gani kinawaangusha – zinaa!
Ndiyo
maana Nabii Hosea alitumiwa na Bwana kuendelea kusema kuwa; “UZINZI na
divai mpya huondoa FAHAMU za wanadamu” (Hosea 4:11). Kukosa fahamu ni
sawa na kutojitambua uko wapi na unafanya nini. Na hii ni kweli kabisa, watu
wanaofanya uzinzi wangekuwa na fahamu wangetubu na kuacha upesi, kwani
madhara yake ni makubwa.
Imeandikwa,
“Mtu
aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” (Mithali 6:23)
Kukosa
kujua neno la Mungu linasema nini juu ya zinaa katika marefu na mapana yake,
kumewafanya watu wengi wanaswe na mtego huu mbaya.
Kuna
wakati fulani tukiwa kwenye mkutano wa kiroho mji mmoja hapa nchini, aliokoka
msichana ambaye alikuwa kahaba katika hotel moja. Na wakati huo alipookoka
alijazwa Roho Mtakatifu, akazungumza kwa lugha mpya.
Baada
ya wiki kama moja hivi, watu wengine
waliokoka waliamua kumtembelea, lakini hali waliomkuta nayo iliwasikitisha.
Kwani walimkuta amerudi nyuma kiroho na amerudi kwenye maisha yake ya zamani
ya ukahaba.
Alipoulizwa
ni kwa nini imekuwa hivyo alijibu “ Naona nilikuwa nadanganywa na mambo ya
wokovu, ili niache maisha haya mzuri (ya ukahaba)”
Je!
Umeamini ya kuwa uzinzi huondoa fahamu za mwanadamu? Huyu binti atasemaje
maisha ya ukahaba ni mazuri kuliko maisha ya wokovu? Ni wazi kwamba fahamu
zake zimeondoka. Anafanya jambo la kumwangamiza nafsi yake, na anasema hayo
ndiyo maisha mazuri!
Lakini
naamini kabisa ya kuwa binti huyu angepewa ushauri wa biblia juu ya tatizo la
zinaa, angekuwa na nafasi nzuri ya kuishi maisha ya ushindi katika Kristo.
Kwa kukosa mafundisho hayo muhimu, kulisababisha hasara kwa nafsi yake.
Mambo
matano muhimu ninayokwenda kuyajadili katika sura hii, ni ushauri mzuri wa
biblia utakaoweza kukusaidia kuishinda dhambi hii ya zinaa. Lakini unabidi
uwe mtendaji wa neno. Kuyasoma haya bila kuyatenda hayatakusaidia. Bali ukiyatenda, hakika utauona mkono wa Mungu.
1. DUMU KATIKA MAOMBI
Yesu pale Gethsemane alisema;
“Je! Hamkuweza kukesha pamojanami hata saa moja? Kesheni, mwombe,
msije mkaingia majaribuni; roho i radhi. Lakini mwili ni dhaifu” (Mathayo 26:40-41)
Ukisha mpokea Kristo moyoni mwako, roho yako inakuwa radhi kumtii
Kristo na kutokutenda dhambi; lakini kumbuka kuwa roho yako bado imo katika
mwili ulio dhaifu ambao unataka kutenda dhambi.
Yesu Kristo alipokuwa akifundisha kuomba alisema sehemu mojawapo ya
maombi yetu iwe;
“Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu, Kwa kuwa ufalme
ni wako, na nguvu na utukufu, hata milele, Amina.” (Mathayo 6:13). Watu
wengine huwa wanaisema sala hii kikasuku bila kuangalia uzito wa maneno
yaliyomo. Lakini ukijua uzito wake hutachoka kuomba kwa “ Na usitutie
majaribuni.” Jaribu mojawapo ambalo unapaswa uombe uepushwe nalo ni zinaa.
Wengine wakianguka katika zinaa, utawasikia wakijitetea na kusema; “Nilibanwa
mno hata nikashindwa kujizuia – nikaanguka katika zinaa.”
Unaweza ukajitetea hivyo, lakini ungeamua kushinda, Bwana angeuwezesha
kushinda. Kwa kuwa imeandikwa; “ Ninyi watoto wadogo mwatokana na Mung;
nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye NDANI YENU NI MKUU KULIKO aliye
katika dunia.” (1 Yohana 4:4) “ Lakini katika mambo hayo yote
TUNASHINDA NA ZAIDI YA KUSHINDANA kwa yeye (Yesu Kristo) aliyetupenda
(Warumi 8:73)
Na ni budi pia ukumbuke, kila jaribu lina njia ya kutokea, si katika
njia ya kushindwa bali katika mlango wa ushindi.
“Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. Jaribu
halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu, ila Mungu ni
mwaminifu, ambaye HATAWAACHA MJARIBIWE KUPITA MWEZAVYO; lakini pamoja na lile
jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.” (1 Wakorintho 10:12-13)
Je! Hili si jambo zuri kufahamu ya kuwa Mungu wetu tunayemwabudu na
kumtumikia katika Kristo ni MWAMINIFU? Hili ni zuri sana! Kwa kuwa hatatuacha tujaribiwe kupita
tuwezavyo, lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili
tuweze kufanya nini? Ili tuweze KUSTAHIMILI!
Jina la Bwana libarikiwe daima!
Tafsiri nyingine inasema “Anayedhani amesimama imara ajihadhari
asianguke. Majaribu mliyokwisha pata ni kawaida kwa binadamu. Mungu ni
mwaminifu. Naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na
majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo
salama.”
2. DUMU KATIKA NENO LA KRISTO
Ili tuweze kuenenda katika upya wa maisha
ndani ya Kristo tuliyempokea mioyoni, tunahitaji kulijua na kulitenda Neno
lake.
Tukilikosa neno lake, tutajikuta kila mara tunafanya mambo ya zamani
tuliyoyafanya tulipokuwa katika dhambi, ambayo hatupaswi kuyafanya sasa
tukiwa ndani ya Kristo. Hii ni kwa kuwa tumekuwa viumbe vipya!
“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale
yamepita; tazama yamekuwa mapya.” (2 Wakorintho 5:17)
Ni kweli umekuwa kiumbe kipya ukiwa NDANI ya Kristo, tamaa ya uzinzi
imehama! Ndiyo maana Yesu Kristo aliomba hivi; “Uwatakase kwa ile kweli,
neno lako ndiyo kweli”. (Yohana 17:17)
Tunahitaji utakaso wa Neno kila wakati kwa sababu zifuatazo:-
(a) Ili tusije tukatenda dhambi
tena (Zaburi 119:9,11)
(b) Ili lituongoze tusije
tukapita gizani, kwa kuwa Neno ni taa (Zaburi 119:105)
(c) Ili lituwezeshe kumtambua
mtu mwenye mawazo mabaya ya dhambi anapoongea na sisi. (Waebrania 4:12,13)
(d) Ili litulinde tusije
tukaanguka katika mikono ya Malaya (Mithali
2:1-3,11, 16; Mithali 5:1-23; Mithali 6:20-35; Mithali 7:1-27, Mithali
23:26-28 na Mithali 30:18-20)
Naamini
kabisa ya kuwa wakristo wakipata mafundisho ya kutosha ya neno la Mungu
maanguko katika dhambi tunayoyasikia sasa hatutayasikia. Kwa kuwa watajifunza
kuishi katika ushindi ule ambao Kristo alitushindia pale msalabani.
Lakini
inasikitisha kuona ya kuwa masomo ya neno la Mungu ya kuwasimamisha wakristo
kiroho hayafundishwi vya kutosha. Na hata yale yanayofundishwa yanafundishwa
juu juu tu. Na tuungane pamoja basi katika kumwomba Bwana ainue walimu wengu
katika Kanisa, na kwamba awape ujasiri na muda wa kutosha wa kufundisha kile
alichowapa kufundisha.
3. IKIMBIE ZINAA.
“IKIMBIENI ZINAA. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili
wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.” (1 Wakorintho 6:18)
Ni kweli ya kwamba, biblia inasema “Basi mtiini Mungu. Mpingeni
shetani, naye atawakimbia.” (Yakobo 4:7). Lakini biblia haisemi ipingeni
zinaa, bali inasema IKIMBIENI ZINAA!
Watu wengi wameanguka katika zinaa, kwa kuwa wanajaribu kupingana
nayo. Mwisho wake wanazidiwa na wanazini. Kwa nini hawafuati ushauri huu wa
biblia unaosema ikiembieni zinaa?
Katika kitabu cha Mwanzo 39:6-12 tunasoma habari za Yusufu jinsi
alivyokabiliwa na jaribu la uzinzi, na jinsi alivyopona kwa kukimbia!
Hebu na tuisome habari hii:
“Naye Yusufu alikuwa mtu mzuri, na mwenye uso mzuri. Ikiwa baada ya
mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, LALA NAMI.
Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu
kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.
Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote
ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyaje ubaya huu mkubwa nikamkosee Mungu?
Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale
naye, wala aongee naye. Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake,
wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; huyo mwanamke akamshika
nguo zake, akisema, lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake.
AKAKIMBIA. Akatoka nje.”
Matokeo ya Yusufu kuikimbia zinaa ni KUFUKUZWA KAZI NA KUFUNGWA JELA.
Yusufu aliuliza; “Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?” Kwa
kuwa hakutaka kumkosea Mungu kwa kukubali kuzini, aliamua kukimbia bila
kujali kitu kitakachotokea baadaye.
Tunapata ushauri gani katika jambo hili?
Hebu soma haya kwa makini. Ni afadhali ufukuzwe kazi kuliko ukamkosea
Mungu kwa kuzini na mwenye nyumba aliyekuajiri!
Ni afadhali ufungwe kuliko ukamkosea Mungu kwa kuzini na hakimu au
askari polisi.
Ni afadhali utengwe kanisani, kuliko ukamkosea Mungu kwa kuzini na
mchungaji au na kiongozi ye yote wa kanisa!
Ni afadhali ufukuzwe kwa ndugu yako, kuliko ukamkosea Mungu kwa kukubali
kuzini naye!
Je! Unasikia ushauri huu wa Roho Mtakatifu anaotufundisha katika neno
la Mungu? Je, umesikia?
Usikubaliane na zinaa; wala usipingane nayo; bali IKIMBIE ZINAA!
4. Usimpe nafasi Ibilisi:
“…..wala usimpe Ibilisi nafasi” (Waefeso 4:27)
Biblia isingesema tusimpe Ibilisi nafasi kama
tusingekuwa na uwezo wa kumpa au kutompa nafasi katika maisha yetu. Mara
nyingi Ibilisi anapata nafasi ya kuingia katika maisha ya mkristo si kwa
sababu amemwonea bali ni kwa sababu amepewa nafasi.
Ni kweli kwamba kuna watu wanaoonewa na Ibilisi. Lakini kwa mtu
aliyezaliwa mara ya pili kwa Roho wa Mungu, amepewa mamlaka juu ya nguvu zote
za Ibilisi, wala hakuna kitu kitakachomdhuru. Soma Luka 10:19.
Ndiyo maana imeandikwa “…..wala msimpe Ibilisi nafasi.”
Mambo gani yanaweza kumpa nafasi Ibilisi katika maisha yetu, hata
atuangushe katika zinaa? Baadhi ya mambo hayo yanaeleza hapa:-
(a) HASIRA
Jambo mojawapo linalompa nafasi Ibilisi kuwaangusha watu katika zinaa
ni hasira iliyojaa uchungu.
“Mwe na hasira, ila msitende dhambi, jua lisichwe na uchungu wenu bado
haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi.” (Waefeso 4:26-27)
Kuna wakati Fulani nilimuliza msichana mmoja sababu zilizomfanya azae
kabla ya kuolewa; alinijibu hivi, “Wazazi wangu walinigombeza siku moja na
kunisingizia kuwa nafanya umalaya, na huku nilikuwa sifanyi. Na kwa
kusingiziwa hivyo pamoja na matusi niliyotukanwa nilibanwa na hasira. Na
nikaamua kuanza kufanya umalaya kwa kuwa sikuona uhalali kusingiziwa kitu
ambacho nilikuwa sifanyi, kwa hiyo nikaone heri nifanye ili nikisemwa;
nisemwe juu ya kitu ninachofanya kweli. Na matokeo yake ni kupata mamba na
kuzaa kabla ya kuolewa.”
Hali ya msichana huyu inawapata wengi. Na hata katika ndoa, chanzo
kikubwa cha mume au mke kutokuwa waaminifu katika unyumba wao ni chuki na
hasira iliyo kati yao.
Mwingine anazini ili amkomoe mwenzake! Ole!
Hasira siyo tiketi yako ya kukufanya uzini.
“Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke
kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya, tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi,
wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu
katika Kristo alivyowasamehe ninyi.” (Waefeso 4:31,32)
Ikiwa hasira inakusumbua, badala ya kumkosea Mungu kwa kuzini, jifunze
kusemehe na kusahau kwa kutumia uwezo wa Kristo aliye ndani yako.
(b) MAWAZO
Mtu mmoja alikuja kwangu na kuniomba nimwombee apone ugonjwa uliokuwa
unamsumbua.
Nikamuuliza; “ Ugonjwa huu ulikuanzaje?”
Akasema; “Wakati Fulani nilianguka katika zinaa, na baada ya hapo
nikaanza kuumwa ugonjwa huu.”
Nikamuuliza tena; “Je! Ulitubu baada ya kuzini? Akasema; “Ndiyo
nilitubu, hata nikawaomba watu waniombee nipone; wakaomba lakini sikupona.”
Nikamjibu nikasema; “Lakini naona wewe ndiye mwenye shida – hukutubu
sawa sawa.
Kwa kuwa imeandikwa; “ Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu naye
atakibarikia chakula chako, na maji yako; NAMI NITAKUONDOLEA UGONJWA KATI
YAKO.” (Kutoka 23:25)
Akasema; “ Ni kweli nimetubu na wala sijarudi tena kuzini,
ila kinachonisumbua ni mawazo. Kila wakati nakuta nawaza juu ya yule mwanamke
niliyezini naye, lakini kila ninapotaka kwenda kwake najizuia.”
Nikamwambia; “Je hujui ya kuwa unapomwazia mwanamke moyoni mwako
kwa kumtamani unazini naye? Na kwa ajili hiyo unahitaji kutubu upya, na
usimwazie tena kwa kumtamani.”
Watu wengi wanasumbuliwa na mawazo ya zinaa kama
mtu huyu. Na wakati mwingine wanajitahidi wasiwaze lakini wanashindwa. Na
wengi wa wale waliofanya zinaa kwa mwili huwa mara nyingi wamekwisha kuzini
moyoni.
Usiwaze mawazo mabaya ya uzinzi, na kumpa nafasi Ibilisi! Jaza moyo
wako neno la Mungu, na utawaza neno la Mungu. Je hukumbuki kuwa imeandikwa ya
kuwa;
“Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya
staha, yoyote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza,
yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote,
YATAFAKARINI HAYO” (Wafilipi 4:8)
(c) MAENEO YASIYOFAA
Enyi wavulana jihadharini na ndugu zenu wa kike, na enyi wasichana
jihadharini na ndugu zenu wa kiume. Soma katika 2 Samweli 13:1-39 uone jinsi
mtu na dada yake walivyoanguka katika zinaa. Tafadhali uwe mwangalifu!
Ibilisi anaweza kutumia hata ndugu yako mliye damu moja kukuangusha ukimpa
nafasi.
Kwa wale walio katika uchumba, angalieni msimpe nafasi Ibilisi kwa
kukaa wawili peke yenu katika maeneo ya siri. Na kwa kutoangalia hili, wengi
wamezini kabla ya siku yao
ya harusi. Tunza usafi wa matendo yako, uwe mwepesi kutofautisha kati ya
kupenda na kutamani. Wachumba wanapokuwa peke yao
wawili mara kwa mara, upendo wa Kristo kati yao unapoa na huwakiana tamaa inayowaongoza
kuzini. Usihalalishe ndoa kabla ya siku ya harusi! Wala usimpe nafasi Ibilisi
ya kuwachezea!
Pia, kwako wewe uliyeokoka, mtu wa Mungu, angalia marafiki zako
walivyo. Jihadhari nao. Wengi wameanguka katika zinaa kwa sababu ya marafiki
zao.
(d) MISINGI YA NDOA
IHESHIMIWE:
Katika ndoa, walio wengi wameanguka katika zinaa, baada ya kutokea
shida katika uhusiano wa tendo la ndoa.
Kwani maandiko yanasemaje?
“Lakini kwa sababu ya ZINAA kila mwanamume na awe na mke wake
mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wke mwenyewe, mume ampe mkewe haki
yake, na vivyo hivyo mke na ampe muweze haki yake. Mke hana amri juu ya mwili
wake, bali mumewe; na vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali
mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpata faragha kwa kusal;
mkajiane tena, shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.” (1
Wakorontho 7:2-5)
Madhara yanayotokea baada ya kumnyima mke wako au mume wako uhusiano
wa tendo la ndoa ni makubwa. Kwa hiyo, jihadhari usimpe nafasi Ibilisi katika
unyumba wako!
5. ISHI NA ENENDA KWA ROHO:
“Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za
mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na
mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka….. Basi
matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, UASHERATI, uchafu, ufisadi…… na
mambo yanayofanana na hayo; katika hayo nawaambia mapema kama
nilivyokwisha, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi
ufalme wa Mungu.” (Wagalatia 5:16-21)
“Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho” (Wagalatia 5:25)
“Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili, bali wale
waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui
juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kutii. Wale
waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa
ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili, bali mwaifuata roho.” (Warumi 8:5-9).
|
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
SOMO: IKIMBIENI ZINAA
Wiki ya Nne
UFANYEJE IKIWA UMEANGUKA
KATIKA DHAMBI YA ZINAA?
Ni jambo gani linatokea Mkristo anapoanguka katika dhambi ya zinaa? Ni
muhimu ufahamu hili, kabla ya kujua utafanyaje ikiwa umeanguka katika dhambi
ya zinaa.
Mambo matatu makubwa yanatokea mkristo anapoanguka katika zinaa;
(a) Anaukosa Ufalme wa Mungu:
“Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, UASHERATI, Uchafu,
Ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina,
faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo; katika
hayo NAWAAMBIA MAPEMA. Kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao
mambo ya jinsi hiyo HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU.” (Wagalatia 5:9-21)
Kumbuka kuwa Mtume Paulo aliandika waraka huu kwa Wagalatia walio
wakristo na siyo kwa Wagalatia ambao siyo wakristo. Waraka unaanza hivi; “Paulo,
Mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo,
na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu), na ndugu wote walio pamoja nami,
kwa MAKANISA YA GALATIA”
(1:1,2)
Yesu Kristo alisema. “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja
nami kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Mimi ni Alfa na Omega mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao
nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa
milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na WAZINZI, na wauaji, na hao
waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.”(Ufunuo
22:12-15)
Soma pia kitabu cha Waefeso 5:5
(b) Anatengwa na Wakristo
wenzake.
Mtume Paulo alipokuwa akiwaandikia wakristo wa Korintho alisema hivi:
“Yakini habari imeenea kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna
isiyokuwako hata katika mataifa….. Mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba
aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo….. Naliwaandikia katika waraka wangu,
kwamba msichangamane na wazinzi. Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia
hii, au na wenye kutamani, au na wanyanganyi, au na wenye kuabudu sanamu;
maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. Lakini mambo yalivyo,
naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au
mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyanganyi;
mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.” (1 Wakorintho 5:1,2-11)
(c) Nchi nzima inaadhibiwa
“Lisikieni neno la Bwana, enyi wana wa Israeli, kwa maana Bwana ana
mateto nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala
kumjua Mungu katika nchi. Hapana neno ila kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi,
na kuua na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na damu hugusana na damu. Kwa
ajili hiyo NCHI ITAOMBOLEZA, na kila mtu akaaye ndani yake ATADHOOFIKA, pamoja
na wanyama wa kondeni na ndege wa angani, naam, samaki wa baharini pia
wataondolewa….. Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa….. Nao watakula,
lakini hawatashiba; watafanya zinaa, lakini hawataongezeka, kwa sababu
wameacha kumwangalia Bwana. Uzinzi na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu” (Hosea 4:1-3; 6,10,11)
Kwa sababu ya uzinzi, gharika iliangamiza watu na vitu vilivyokuwa
katika nchi, alipona Nuhu na watu wachache na viumbe wachache. Kwa sababu ya
zinaa, Sodoma na Gomora iliteketezwa kwa moto, wakapona Lutu na binti zake
wawili.
Na kwa sababu ya zinaa siku hizi nchi zimepigwa kwa ugonjwa wa Ukimwi
(AIDS). Ni kama Nabii Hosea alivyotabiri, NCHI ZINAOMBOLEZA, WATU
WNADHOOFIKA, WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA YA MUNGU, NA WANAPOTELEWA NA
FAHAMU!
Ndiyo maana ni muhimu ufahamu ufanye nini ikiwa umeanguka katika
zinaa. Si mapenzi ya Mungu uangamie, usiurithi ufalme wake, wakristo
wakutenge na kuiangamiza nchi, bali mapenzi yake ni watu wote waifikie toba
ya kweli, waokolewe, waziache njia zao mbaya, na wamgeukie na kumfuata daima!
Kwa hiyo kama umeanguka katika zinaa, sikiliza ushauri ufuatao:
(i)
Usiifiche dhambi:
Najua unaweza kuwaficha wanadamu wasijue umezini,lakini unaweza kwenda
wapi utakakojificha Mungu asikuone? Soma Zaburi ya 139:7-13. Na imeandikwa:-
“Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali
yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.” (Mithali 28:13)
Ukifuatilia habari za Mfalme Daudi, utaona ya kuwa kitu alichokifanya
baada ya kuanguka katika zinaa na mke wa mtu, ni kujitahidi kutafuta namna ya
kuifunika hiyo dhambi, lakini alishindwa. Na mwisho wake aliamua kutafuta
mbinu ya kumuua Uria, ambaye mke wake ndiye aliyezini na Mfalme Daudi.
Unaweza ukaona ya kuwa ni kweli kwamba uzinzi huondoa ufahamu za mtu. Kwa
nini Mfalme Daudi aliamua kuua ili alifiche kosa alilofanya?
Je! Alidhani Mungu naye hajamwona? Mungu aliinua mtu wake, ambaye
alikwenda kwa Mfalme Daudi na kumweleza jinsi Mungu alivyochukizwa na kitendo
hicho. Daudi alipojua dhambi iko wazi mbele za Mungu alitubu!
“Bwana asema hivi, Angalia, nitakuondoshea uovu katika nyumba yako,
nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye
atalala na wake zako mbele ya jua hili. Maana wewe ulifanya jambo hili mbele
ya Israeli wote na mbele ya jua. Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia Bwana
dhambi. Nathani akamwambia Daudi, Bwana naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa.
LAKINI, KWA KUWA KWA TENDO HILI UMEWAPA ADUI ZA BWANA NAFASI KUBWA YA
KUKUFURU, motto atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa.” (2 Samweli 12:11-14)
Ni kweli kwamba unaweza ukafanya uzinzi kwa siri, Mke wako asijue, au
mume wako asijue, au wazazi wako na ndugu zako wasijue, au waliookoka wenzako
wasijue, Lakini, FAHAMU HAKIKA YA KUWA MUNGU AMEKUONA.
Na mshahara wa dhambi ni mauti, kwa hiyo kama
unataka kudumu katika uzima uliopewa na Kristo, usijaribu kuificha dhambi.
(ii)
Tubu, Tengeneza na
Usirudie tena.
Ikiwa umeanguka katika dhambi ya uzinzi, njia iliyo wazi ni wewe
kutubu kwa Mungu katika Roho na Kweli,halafu tengeneza (tubu) kwa wale uliowakosea
na usirudie tena; na mwisho songa mbele katika wokovu aliokupa Bwana.
Kuna mtu mmoja aliniambia nimsaidie katika kumwombea kwa kuwa kuna
wakati alianguka katika zinaa, na baadaye akatubu. Lakini kila wakati
yalikuwa yanamjia mawazo ya kuhukumu ya kuwa alizini na kwa hiyo anajiona
hafai tena hata kuomba wala kuendelea na wokovu. Ingawa alitubu bado
alishitakiwa sana
moyoni na kosa alilolifanya. Aliona kama vile Mungu hajamsamehe.
Inawezekana na wewe ukasumbuliwa na hali ya namna hii. Nafahamu
ya kuwa wanadamu ni wagumu kusamehe na kusahau,hata kama
wanajua umekwisha tubu na kutengeneza.
Lakini nataka nikuambie hivi, usiupime msamaha anaokupa Mungu
unapotubu kwa kuangalia na kusikiliza wanadamu wanasemaje juu yako; bali
angalia neno lake
katika biblia
linasemaje. Imeandikwa hivi;
“Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na
kama mtu akitenda dhambi anaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zenu, wala si kwa dhambi zetu tu, bali na
kwa dhambi za ulimwengu wote” (1 Yohana 2:1,2)
Tena imeandikwa hivi;
“Tukiziungama dhambi zetu, Yesu ni mwaminifu na wa haki hata
atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” (1 Yohana 1:9)
Tena imeandikwa hivi;
“Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundi
sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundi kama bendera,
zitakuwa kama sufu.” (Isaya 1:8)
Tena imeandikwa hivi;
“Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao zitazikumbuka tena”. (Waebrania 8:12)
Kama ukitubu katika Roho na Kweli, Bwana
ameahidi kusamehe na atakusamehe. Na yeye akisamehe, anafuta kosa lako na
kulisahau. Sasa kama Mungu amesamehe na kusahau, shetani au mwanadamu anapata
wapi – haki ya kukunyoshea kidole cha hukumu? Soma Warumi 8:31-39.
Neno la Mungu ndilo linalokupa uhakika na namna ya kupokea msamaha.
Baada ya kutubu na kutengeneza, simama upya ndani ya Kristo, na songa mbele
kiroho, na katika kumtumikia Bwana. Kwa kuwa “Katika mambo hayo yote
tunashinda na zaidi ya kushinda, kwa yeye (Kristo) aliyetupenda. (Warumi
8:37)
(iii) Kemea roho ya Uzinzi.
Uzinzi ni roho. Bwana anasema hivi katika kitabu cha Hosea 4:11,12; “Uzinzi
na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu. Watu wangu hutaka shauri
kwa gongo lao, na fimbo yao huwahubiri mambo; maana Roho ya UZINZI
imewakosesha, nao wamekwenda kuzini mbali na Mungu wao”.
|
![]() |
Sura ya Kwanza
KWA NINI SI MAPENZI YA
MUNGU TUWE MASKINI?
Napenda kuanza kukuambia ya kuwa si
mapenzi ya Mungu uwe maskini. Kwa sababu tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu
huu, Mungu hakupanga kuwa watu wake aliowaumba wawe maskini; bila kujali
rangi, kabila, wala taifa.
Nafahamu ya kuwa katika Mathayo 5:3, Yesu Kristo alisema; “Heri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni
wao.” Watu wengi wanapousoma mstari huu, wanadhani Yesu Kristo alisema
“Heri walio maskini wa mahitaji ya MWILI; maana ufalme wa mbinguni ni wao.”
Lakini Kristo hakusema hivyo.
Mtu maskini maana yake ni mtu mhitaji. Yesu Kristo aliposema “Heri walio maskini wa roho …….” Alikuwa ana maana
ya kusema ‘Heri walio wahitaji wa mambo ya rohoni; maana ufalme wa mbinguni
ni wao. Ndiyo maana aliongeza kusema, “Heri wenye
njaa na kiu ya haki; maana hao watashibishwa" (Mathayo 5:6).
Mtu aliye maskini wa mambo ya mwili ni yule aliye mhitaji wa mambo ya mwili.
Na mambo ya mwilini ninayoyasema ni mavazi, chakula na mahali pa kulala. Yesu
Kristo hakusema heri wale walio na mahitaji ya chakula, mavazi, afya na
malazi.
Ninaposema mahitaji ya mwili usije ukachanganya na matendo ya mwili
yaliyoandikwa katika Wagalatia 5:19-21 ambayo ni uasherati, uchafu, ufisadi,
ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
husuda na ulevi. Mimi siyazungumzii hayo ninaposema juu ya mahitaji ya mwili.
Mahitaji ya mwili ninayoyasema ni mavazi, chakula, nyumba na matibabu.
Kwa hiyo si sawa kabisa kwa mtu kuhalalisha umaskini wa mwili, yaani ukosefu
wa chakula, mavazi, matibabu na nyumba, kwa kutumia maneno ya Bwana Yesu
Kristo yaliyo katika Mathayo 5:3:
Nataka kurudia
tena; si mapenzi ya Mungu mtu awe maskini.
Unaweza ukaniuliza na kusema, “Bwana Mwakasege kama si mapenzi ya Mungu mtu
awe maskini, mbona basi kuna matajiri na maskini, je! Mungu hakuwaumba wote?
Ni kweli kwani hata imeandikwa katika Mithali 22:2, kuwa “Tajiri na maskini hukutana pamoja; Bwana ndiye
aliyewaumba wote”. Lakini fahamu ya kuwa ingawa matajiri na maskini
waliopo wote waliumbwa na Mungu; tangu mwanzo wa uumbaji Mungu hakuyaweka
matabaka haya mawili.
Hapo mwanzo Mungu alipomuumba mtu, hakuweka ndani yake utajiri na umaskini
pamoja. Wala hakuumba watu wengine wawe matajiri na wengine wawe maskini.
Tunafahamu ya kuwa mtu aliumbwa kwa mfano wa Mungu na kwa sura ya Mungu. Na
naamini ya kuwa utakubaliana nami nikisema Mungu wetu si maskini kwa hiyo
hatukuumbwa kwa mfano wa kimaskini wala sura ya kimaskini.
Kwa nini
nasema na kusisitiza ya kuwa si mapenzi ya Mungu tuwe maskini?
Ninazo
sababu nne ambazo ningependa kukushirikisha:
“ Bali utamkumbuka Bwana , Mungu wako, maana
ndiye akupaye NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI; ili alifanye imara
agano lake alilowapa baba zako, kama hivi
leo” (Kumb. 8:18).
Si mapenzi ya Mungu tuwe maskini
kwa kuwa yeye mwenyewe ndiye atupaye nguvu ili tupate utajiri! Kama basi Mungu anatupa nguvu za kupata utajiri, ina
maana ni wazi kwamba Mungu hapendi tuwe maskini wa mambo ya mwilini.
Lakini fahamu ya kuwa si matajiri wote waliopo duniani wameupata utajiri
kutokana na nguvu walizopewa na Mungu. Wengi wamepata utajiri kwa njia ya
dhuluma. Na ndiyo maana sehemu nyingi katika Biblia matajiri wa jinsi hiyo
wamekemewa. Soma Amosi 5:11, 12. Kwa sababu hii Mungu hayuko upande wa
matajiri hawa. Hii pia haimaanishi kuwa Mungu yuko upande wa KILA maskini
aliopo duniani. La hasha! Mungu yuko upande wa yule ayafanyaye mapenzi yake
awe tajiri au maskini (Mathayo 7:21)
Watu wengi wametajirika kwa njia ya rushwa na kutokusimamia haki pamoja na
uchoyo. Na hii si sawa hata mbele za Mungu. Ni dhambi zilizo wazi kabisa. Na
wote wafanyayo hayo wanahitaji kutubu!
Ngoja nikueleze jambo muhimu: Mungu anapokupa nguvu za kupata utajiri,
anakupa akiwa na lengo na kusudi muhimu.
Ni
lengo gani hilo?
Imeandikwa, “………. Ili alifanye imara agano lake alilowapa
baba zako, kama hivi leo”
Na Yesu Kristo alisema, “
……. Kikombe hiki ni AGANO JIPYA KATIKA DAMU YANGU, inayomwagika kwa
ajili yenu” (Luka 22:20).
Mungu akikupa nguvu za kupata
utajiri ni kwa ajili ya kulifanya imara agano lake katika
damu ya Yesu Kristo. Na hii ina maana utajiri utakaokuwa nao kutoka kwa Mungu
ni kwa kueneza injili! Ni kwa ajili ya kueneza habari njema ya ukombozi
kutokana na dhambi, mauti, magonjwa na umaskini. Habari njema hii inatakiwa
kuenezwa kwa maneno na kwa matendo.
Kwa kuwa tu kuna matajiri wasio wa haki basi haimaanishi kuwa matajiri wa
haki hawapo. Ni budi tuweze kutofautisha utajiri ulio wa haki na utajiri usio
wa haki.
Mungu wetu tunayemwabudu na kumtumikia katika Kristo Yesu si Mungu wa
hasara bali Mungu wa faida. Imeandikwa hivi;
“ Bwana, Mkombozi wako, Mtakatifu wa
Israeli, asema hivi;Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye
ili upate faida, nikuongozaye katika njia ikupasayo kuifuata” (Isaya 48:17).
Ndiyo maana kila mtu ndani
yake ameumbiwa kupenda kufundishwa ili apate faida katika mambo anayoyafanya.
Mungu akikufundisha kupata faida; njia utakayotumia kupata faida itakuwa njia
ya haki. Na faida hiyo haitakuwa kwa ajili yako mwenyewe, bali
utawashirikisha na wengine pia faida hiyo .
Watu wengine kwa kutokuwa wavumilivu, na kutokujali mafundisho ya Mungu;
wameamua kujipatia faida kwa kuwadhulumu, kuwakandamiza na kuwanyonya
wengine. Na inasikitisha jinsi wanavyomshirikisha Mungu katika faida najisi
namna hiyo waposema ya kuwa ni Mungu aliyewasaidia ‘kudhulumu na kunyonya’.
Ni wazi ya kuwa Mungu hakuwasaidia kupata faida kwa njia ya udhalimu.
Si mapenzi ya Mungu tuwe maskini, ndiyo maana anatufundisha ili tupate faida ya halali. Kwa ajili hiyo imeandikwa; “Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji” (Waefeso 4:28).
Je! Si jambo la kushukuru hili, la kuwa na
Mungu ambaye hapendi tupate hasara?
Kama Mungu asingekuwa anapenda tufanikiwe katika mahitaji yetu ya mwili, basi
ingeandikwa wazi katika Biblia. Lakini badala yake naona maneno kama
yafuatavyo; “Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo
YOTE na kuwa na afya yako, kama vile roho
yako ifanikiwavyo” (3Yohana 1:2).
Kwa maneno mengine anatuombea ya kuwa kwa kadri roho inavyofanikiwa basi
tufanikiwe vivyo hivyo katika mahitaji ya mwili – yaani tuwe na chakula,
mavazi, n.k.
Katika Zaburi 24:1 imeandikwa;“Nchi na
vyote viijazavyo ni mali
ya Bwana; Dunia na wote wakaao ndani yake”
Na pia ukisoma katika Hagai 2:8 unaona imeandikwa hivi “Fedha ni mali
yangu, na dhahabu ni mali
yangu, asema Bwana wa majeshi”
Ngoja nikuulize swali; Je! unadhani vitu vyote hivi Bwana amemwekea nani?
Unadhani alimwekea shetani na watu wanyonyaji wachache?
La
hasha!
Mungu aliviweka vitu hvi vyote na mali hii yote kwa ajili ya watu wake wote, ili itumike katika usawa. Kwa nini? Kwa kuwa Mungu hapendi watu wake wawe maskini. Ndiyo maana mtu alipoumbwa aliwekwa awe wakili wa mali yote ya Mungu hapa duniani. Utajiri uliomo duniani umetawaliwa na watu wachache na nchi chache siku hizi kwa sababu ya dhambi za uchoyo, ubinafsi, uonevu,unyonyaji, unyang’anyi na dhuluma zilizoingia ndani ya mwanadamu. Na hii imefanya watu wengine kufikiri ya kuwa Mungu ndiye aliyegawa matabaka haya mawili, ambavyo si kweli. Na si vizuri kumsingizia Mungu katika jambo ambalo mwanadamu mwenyewe amejiletea uharibufu.
“ Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu
Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa
tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake” (2
Wakorintho 8:9).
Je! unafahamu kwa nini
Yesu Kristo aliamua kuwa maskini? Ni “…….. ili kwamba ninyi mpate kuwa
MATAJIRI kwa umaskini wake”.
Najua kuna wengine
watashangaa kuusoma mstari huu; lakini ndivyo ilivyo.
Nimewahi kusikia mkristo mmoja akisema: “ Mimi ni
maskini kwa kuwa Yesu Kristo alikuwa maskini”.
Na mwingine alisema; “ Napenda kuwa maskini
kwa kuwa Yesu Kristo alikuwa maskini”.
Nadhani kuwa kuna wakristo wengi ambao wana mawazo kama
haya. Ni kweli kwamba Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani alikuwa maskini.
Lakini hakuwa maskini ili sisi tuwe maskini; bali alikuwa maskini ili sisi
tuwe matajiri! Kama alikuwa maskini ili sisi tuwe maskini kama
wengine wanavyodhani, basi kazi hiyo haina faida kwetu. Lakini Yesu Kristo
asifiwe kwa kuwa alikuwa maskini ili sisi tuwe MATAJIRI.
Na ndiyo maana alisema katika Luka 4:18a ya kuwa;
“Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri MASKINI
habari njema.”
Je! kuna habari njema kwa maskini zaidi ya
kumwondoa katika umaskini wake?
Injili ni habari njema. Na injili ni uweza wa Mungu uuletao wokovu kwa kila
aaminiye (Warumi 1:16). Kuokoka si kuenda tu mbinguni; bali kuokoka maana
yake ni uokolewe usiende motoni bali uende mbinguni ukifa, PAMOJA na
kuokolewa kutoka kwenye matatizo ukiwa hapa duniani ambayo ni pamoja na
umaskini.
Petro aliposema “Bwana niokoe” alipokuwa anazama katika maji unafikiri
alikuwa anataka wakati huo aokoke aende mbinguni? La hasha! Yeye Petro
alitaka aokoke ASIZAME KATIKA MAJI. Na Yesu akasikia kilio chake akamwokoa.
Hivi leo kuna watu wengi mijini na vijijini wanalia Yesu awaokoe kutokana na
njaa, kukosa mavazi, magonjwa, maonezi, nakadhalika. Kanisa kama mwili wa
Kristo linatakiwa kuwa mstari wa mbele kuwasaidia watu hao, kwa kuwa kazi hii
ni sehemu ya utume wake.
Wakristo wengine utawasikia wakisema; hapa duniani hawahitaji kitu bali thawabu yao wataipata mbinguni. Lakini matamshi ya namna hii yanaeleza ukweli nusu na usiokamilika. Kuwa mkristo kuna thawabu duniani na kuna thawabu mbinguni. Kama hakuna thawabu yoyote tunayoipata tukiwa hapa duniani kwa kumfuata Yesu Kristo; basi ukristo wetu hauna maana na hauna msaada wowote kwa mwanadamu. Ukristo usiotatua matatizo ya mwanadamu ya kila siku, ni ukristo usio na uhai.
Mtume Petro naye aliwahi kusumbuliwa sana
na jambo hili, hata ikabidi amuulize Bwana Yesu.
“Ndipo Petro akajibu, akamwambia, tazama, sisi
tumeacha vyote tukakufuata, TUTAPATA NINI BASI?” (Mathayo 19:27)
“Yesu
akasema, Amini, nawaambiaeni, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au
ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa
ajili ya Injili, ila atapewa MARA MIA SASA WAKATI HUU, nyumba, na ndugu
waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na
katika ulimwengu ujao uzima wa milele” (Marko 10:29,30).
Majibu haya ya Bwana Yesu, yanazidi kutudhihirishia ya kwamba si mapenzi ya
Mungu tuwe maskini. Yesu Kristo ameeleza wazi kabisa ya kuwa atakayemwamini
na kufuata maagizo hayo atapata MARA MIA SASA WAKATI HUU akiwa bado duniani.
Na kati ya vitu atakavyopewa ni pamoja na nyumba na mashamba!
Ni kweli Bwana Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani alikuwa maskini, lakini
baada ya kufufuka alirudishiwa utajiri wake. Ndiyo maana Mtume Paulo
anazungumzia juu ya “….. utajiri wake Kristo
usiopimika”. (Waefeso 3:8). Na katika Wafilipi 4:19 tunasoma hivi; “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri
ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu”.
Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alichukua dhambi zetu na magonjwa yetu , na kwa
kupigwa kwake sisi tumepona (Isaya 53:5; Mathayo 8:16,17; 1Petro 2:24). Na
kwa kujua hili kanisa linajihusisha na kuombea wagonjwa na kutoa huduma za
afya kwa wagonjwa.
Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alichukua dhambi zetu na akafanyika dhambi kwa
ajili yetu, “ Ili
sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye” (2Wakorintho 5:21). Na kwa
kujua hili kanisa linahubiri habari za ondoleo la dhambi kwa yeyote
atakayemwamini Kristo.
Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alikuwa maskini, ingawa alikuwa tajiri, ili kwa umaskini wake sisi tupate kuwa matajiri (2 Wakorintho 8:9). Na kwa kujua hili kanisa linajihusisha na miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili mtu aondokane na umaskini. |
|
|
![]() |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
![]() |
Sura ya Tatu
NANI ANAUPENDA WOKOVU WA
KIMASIKINI?
“Nani anaupenda wokovu wa Ukristo wa
kimaskini?” Ukiona mtu amefika hali ya kujiuliza swali la jinsi hii,
ujue ana hali ngumu sana
kiuchumi.
Hili swali nilijikuta najiuliza mwenyewe baada ya kuwa na hali ngumu sana kimaisha baada kuokoka. Kuna wakati fulani baada ya kuokoka mimi na mke wangu tulijikuta tumefika mahali pa kukosa hata dawa ya mswaki, nguo, viatu, na chakula kizuri. Licha ya shida hizi zote bado zilifuata zingine baada ya ndugu zetu wawili tuliokuwa tunawalipia masomo yao kufukuzwa na kurudi nyumbani kwa kukosa ada. Na waliambiwa wasirudi shuleni bila nusu ya ada! Unadhani tulikuwa na furaha tena? Ingawa tulikuwa tunasema tumeokoka, na mtu akituambia ‘Bwana asifiwe’ tuliitika ‘Amina’ ndani ya mioyo yetu tulikuwa na vita vikali na maswali mengi. Ni vigumu kuieleza hali hiyo tuliyoipitia ilivyokuwa ngumu kwa maneno. Lakini utaelewa mtu mwenye familia anavyojisikia anapoona anakosa hata fedha za kuwanunulia mke na watoto wake chakula licha ya mavazi. Wakati huo tulikuwa na mtoto mmoja. Hali ilivyozidi kuwa ngumu, ndivyo nilivyozidi kusongwa na mawazo. Ilifika wakati ambapo nilikuwa naona aibu hata kukaa sebuleni, maana niliogopa hata kuwaangalia wale vijana waliofukuzwa shule, nikijua kuwa wataniangalia kwa macho ya huruma ili niwape ada warudi shule. Lakini si kwamba nilikuwa siwahurumii, bali sikuwa na fedha za kuwapa. Ningeanzaje kuwaambia kuwa sina fedha, wakati wanajua nafanya kazi, na pia waliona nilikuwa na fedha nyingi kabla sijaokoka? Jambo hili lilinifanya niwaze sana. Inakuwaje kabla sijaokoka nilikuwa na fedha nyingi na baada ya kuokoka najikuta nimefilisika? Ingawa ni kweli kwamba kabla ya kuokoka fedha zingine nilizipata kwa njia zilizo kinyume cha ukristo lakini nilikuwa nazo. Na baada ya kuokoka ilibidi niziache njia hizo – na matokeo yake nilijikuta nimefilisika. Lakini nilikuwa nimesoma katika Hagai 2:8 kuwa fedha na dhahabu ni mali ya Mungu. Na pia nilijua kuwa vyote vya Mungu ni vyangu nikiwa ndani ya Kristo. Kwa hiyo ilikuwa vigumu kuelewa kwa nini Mungu aseme fedha ni mali yake, halafu mimi niliye mtoto wake nisiwe nazo. Ningewezaje kusema wokovu ni mzuri wakati baada ya kuokoka nimejikuta sina fedha za kutosha kununua chakula, nguo, dawa ya mswaki na hata kukosa ada za watoto! Je ndivyo Mungu anavyotaka tuwe baada ya kuokoka? Wakati huo ndipo nilipoelewa kwa nini wana wa Israeli waliyakumbuka masufuria ya nyama ya Misri, ingawa walikula nyama hizo wakiwa utumwani. Ni rahisi sana mtu aliyeokoka kurudia njia au maisha mabaya ya kutafuta fedha kwa njia zilizo kinyume cha ukristo anapokuta anabanwa na matatizo ya kiuchumi maishani mwake. Na hata wakati mwingine unakesha katika maombi ili kumlilia Mungu akupe chakula na mavazi unaona kama vile hasikii. Nilipokuwa nasumbuliwa na hali hii ndipo nilipojikuta najiuliza mwenyewe; “ Nani anaupenda wokovu wa kimaskini?” Nilijikuta siupendi kabisa. Ni wokovu gani huu ambao haunisaidii hata kutunza familia yangu? Siku moja nilimuuliza mke wangu; nikasema; “Je! wewe unaupenda wokovu wa kimaskini?” Akajibu; “Hapa, siupendi!” Nikasema; “Naona tuna mawazo yanayofanana. Kwa hiyo naona ni muhimu tumuulize Mungu katika maombi kwa nini tulipokuwa kwa shetani tulikuwa na fedha za kutosha, lakini baada ya kuokoka na kuja kwake tunajikuta hatuna fedha hata za kununulia vitu muhimu?” Baada ya kukubaliana hayo, mimi na mke wangu tulianza kumwomba Mungu kwa mfululizo wa siku tatu juu ya jambo moja hilo hilo. Namshukuru Mungu kwa kunipa mke ambaye aliweza kusimama pamoja nami katika maombi juu ya jambo hili. Sijui ningekuwa na hali gani kama angelalamika. Namshukuru Mungu mke wangu hakulalamika bali ALIOMBA PAMOJA NAMI. Mungu alitujibu maombi na akaanza kutufundisha mambo mengi ambayo mengine nawashirikisha katika ujumbe huu. Tulijua hakika kuwa hayakuwa MAPENZI YA MUNGU tuwe na hali ngumu ya kimaisha namna hiyo – kukosa fedha za kutosha kununulia nguo, chakula na vitu vingine muhimu. Na baada ya kuyaweka katika matendo yale tuliyoambiwa na Bwana yaliyo katika neno lake, hali yetu ilibadilika. Na matatizo tuliyokuwa nayo wakati ule yakaisha. Tukaanza kuona furaha tena katika maisha haya ya wokovu. Ni vizuri kujua kuwa Mungu wetu hapendi tuwe maskini. Wala hapendi wokovu wa kimaskini! Ndiyo maana alimtuma Mwana wake wa Pekee, Yesu Kristo kutukomboa. Kwa kukumbusha tu, Yesu Kristo aliyafanya yafuatayo kwa kufa na kufufuka kwake: "Yesu Kristo alifanyika dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tuhesabiwe haki bure ndani yake ya kusimama tena mbele ya Mungu" (2Wakorintho 5:21) "Yesu Kristo aliuchukua udhaifu wetu, ili katika mambo yote tuzitegemee nguvu zake" (Mathayo 8:17; Wafilipi 4:13) Yesu Kristo aliyachukua magonjwa yetu, ili tusitawaliwe na magonjwa tena na kwa kupigwa kwake tumepona (Isaya 53:4,5; Mathayo 8:17; 1 Petro 2:24) Yesu Kristo aliyachukua masikitiko na huzuni zetu, ili tukae katika amani yake ipitayo fahamu zote (Isaya 53:34; Wafilipi 4:6,7) Yesu Kristo alikuwa maskini kwa ajili yetu ingawa alikuwa tajiri, ili sisi tupate kuwa matajiri katika Yeye (2 Wakorintho 8:9) Ndiyo maana matunga Zaburi 23 aliandika hivi: “Bwana ndiye mchungaji wangu, SITAPUNGUKIWA NA KITU.Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake …. Hakika WEMA NA FADHILI zitanifuata siku zote za maisha yangu; nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele”. Ni rahisi sana kusema. “Bwana ndiye mchungaji wangu, SITAPUNGUKIWA NA KITU, lakini je! Ni kweli hujapungukiwa na kitu? Je! Zaburi hii ni ya kweli, au ni maneno mazuri tu ya kutungia nyimbo? Lakini napenda kukutia moyo kuwa maneno haya ni ya kweli, ukikaa ndani ya Kristo hutapungukiwa na kitu. Ndiyo maana Mungu alimwambia Yoshua ya kuwa atii maagizo yake yote na kuyafanya HATAMPUNGUKIA WALA KUMUACHA (Yoshua 1:5) Kwa kuwa maneno haya ni ya kweli, mbona basi wakristo wengi WAMEPUNGUKIWA NA VITU? Tatizo haliko kwa Mungu, bali kwetu sisi. Na tuwe watendaji wa neno na tutaona mafanikio. WAJIBU WA WAKRISTO: Ni wajibu wa wakristo (a) kusaidiana sisi wenyewe kiuchumi; na (b) Kuwasaidia kiuchumi watu wengine wasio wakristo. Kuna wakati fulani mtu mmoja alikuja kwangu kuomba ushauri. Nikamuuliza. “Una tatizo gani linalokukabili?” Akasema; “ Baada ya kuokoka ilibidi niache njia fulani fulani ambazo zilikuwa zinanisaidia kupata fedha kwa kuwa zilikuwa ni kinyume cha maadili ya kikristo. Lakini sasa naona napata shida, sina fedha za chakula, wala sijui kodi ya nyumba mwezi huu nitapata wapi. Licha ya hayo, wale niliowakopa fedha kufanyia biashara hizo nilizoziacha wananidai fedha zao. Hata naogopa kukutana nao. Hebu nisaidie mawazo, najua nimeokoka kweli, lakini NITAISHIJE KATIKA HALI HII?” Unadhani swali lilikuwa jepesi kujibu? Si swala la kumwambia tuombe halafu umwache aende zake! Yeye anachotaka baada ya kuomba aone msaada unamjia. La sivyo maombi hayo yanakosa maana kwake. Swali hili “Nitaishije katika hali hii?” Linawasumbua walio wakristo wengi siku hizi. Na umefika wakati wa kulijibu. Ngoja nikuulize swali jingine. Unadhani mwanamke ambaye anafanya uasherati ili kupata fedha za kuwalishia watoto wake hajui kuwa uasherati ni dhambi? Nina uhakika anajua kwa kuwa kuna mwingine hata kama anafanya hayo hakosi kila jumapili kanisani, na wakati mwingine hutoa sadaka kwa fedha hiyo hiyo. Unadhani hajui kuwa uasherati ni dhambi? Unadhani hamwelewi mchungaji anaposema acheni dhambi? Unadhani haogopi magonjwa ya zinaa? Unadhani anapenda kufanya hivyo? Nina hakika walio wengi hawapendi kufanya hivyo. Lakini jambo linalomsumbua, akiacha uasherati atapata wapi fedha za kuwatunza watoto wake? Nina uhakika akijibiwa swali hili ni rahisi kuacha tabia hiyo chafu. Wasichana wengi mashuleni wamejikuta wamebeba mimba na kuharibu usichana wao kwa kudanganywa na fedha wanazozihitaji kwa ajili ya kununulia mafuta ya kupaka, nguo, na kutengeneza mitindo ya nywele. Vijana wengi wa kiume wamejikuta wamejiingiza katika biashara haramu kwa sababu ya kutaka utajiri wa haraka haraka. Kwa sababu ya kutokujua la kufanya wakristo wengi wamepoteza ushuhuda wao kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi. Wakristo wenzetu walifanyaje? Tusome kitabu cha Matendo ya Mitume 4:32,34,35. “Na jamii ya watu waliamini (Wakristo) walikuwa na MOYO MMOJA NA ROHO MOJA; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na VITU VYOTE SHIRIKA. WALA HAPAKUWA NA MTU MMOJA MIONGONI MWAO MWENYE MAHITAJI; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa; wakaiweka miguuni pa mitume, kila mtu akagawiwa KWA KADRI YA ALIVYOHITAJI” Utaona katika habari hii ya kuwa kwa sababu ya Ukarimu na kutokuwa na ubinafsi wakristo hao waliweza kupambana na tatizo la umaskini katikati yao. Ndiyo maana ikandikwa kuwa; “WALA HAPAKUWA NA MTU MMOJA MIONGONI MWAO MWENYE MAHITAJI”. Jina la Bwana libarikiwe! Matokeo ya usharika namna hii ni haya; “Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote” (Matendo ya Mitume 4:33) Je! Siku hizi hakuna wakristo wenye mahitaji kati yetu? Na tunafanya nini ili kuwasaidia? Je! Kuwaombea tu kunatosha? Je! Unashangaa kwa nini ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu hautangazwi kwa nguvu na wakristo? Nadhani wakristo wengi wanatumia muda wao mwingi sana kujitafutia mahitaji yao kiasi ambacho muda unaobaki hautoshi kufanya kazi ya kushuhudia. Wenzetu walisaidiana, na sisi tusaidiane. Wazazi mara nyingi huwa wanawasaidia vijana wao waliowaoza kuanza maisha mapya. Na fahamu kuwa wokovu ni maisha mapya. Tunawajibika sana kuwasaidia wale wanaookoka kiroho na kimwili kuanza maisha mapya ndani ya Kristo. Kwa kukosa msaada wa kiuchumi, wengi wamepoa na kurudi nyuma. Niliwahi kushirikishwa ushuhuda mmoja ambao naamini utakusaidia kukuelewesha jambo hili ninalokuambia. Kuna mtu mmoja aliokoka baada ya muda mrefu kuwa mganga wa kienyeji na mchawi. Baada ya kuokoka ilibidi aache uchawi na uganga wa kienyeji, shughuli hizi ndizo zilizokuwa zinamsaidia kupata fedha ya matumizi. Baada ya kukaa miezi michache katika wokovu, bila ya kuwa na njia nyingine ya kupata fedha, ilibidi atumie akiba yote aliyokuwa nayo. Baada ya hiyo akiba kuisha akaanza kupata shida namna ya kuishi. Akiwa katika mahangaiko hayo, wakaja watu nyumbani kwake wakiomba msaada wa kutibiwa magonjwa yao. Hao watu walisikia kuwa yeye ni mganga wa kienyeji, wala hawakujua kuwa alikuwa ameokoka na kuacha uganga huo. Kwa sababu ya kukosa fedha, huyo mtu aliyeokoka akawaza moyoni mwake; “Hawa watu hawajui kuwa nimeokoka, kwa hiyo hakuna haja ya kuwaambia, kwani kuna ubaya gani nikienda kuwachimbia dawa ninazozifahamu halafu wanipe fedha inisaidie?” Kwa hiyo akaenda akawachimbia hizo dawa akawapa. Na hao watu wakaondoka baada ya kumlipa fedha. Lakini usiku, huyo aliyeokoka alipokuwa amelala aliona katika maono. Katika maono hayo akayaona majini mawili yaliyokuwa yanamsaidia katika uchawi zamani kabla ya hajaokoka. Hayo majini yakasema; “Tulikwaambia hutafanikiwa katika wokovu, sisi ndiyo tumekufilisi mali yako. Na pia sisi ndiyo tuliowatuma wale wagonjwa waje kwako. Ulipochima zile dawa ukatuita tulikokuwa. Sasa tumekuja, mwache Yesu njoo kwetu nasi tutakutajirisha”. Huyo mtu aliyeokoka aliposikia hayo, akatambua kosa lake, na mara hiyo akalikumbuka jina la Yesu Kristo. Kwa hiyo akayakemea yale majini nayo yakatoweka. Akamka akiwa anatetemeka. Kama asingelikumbuka uwezo wa jina la Yesu Kristo, angefanya nini? Naamini kama angepata msaada wa mahitaji yake toka kwa wakristo wenzake, asingebanwa na mtego huo. Wakristo naomba kuwakumbusha kusaidiana. Ni muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku. Ndiyo maana Mtume Paulo aliongozwa na Roho Mtakatifu kuandika hivi: “Kwa habari za kuwahudumia watakatifu (Wakristo) sina haja ya kuwaandikia. Maana najua utayari wenu, ninaojisifia kwa ajili yenu kwa Wamakedonia, kwamba Akaya ilikuwa tayari tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo wengi wao ……. Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu (Wakristo) riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu, kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote” (2Wakorintho 9:1,2,12 – 15) Ndiyo maana pia katika makanisa kuna mgawanyiko wa huduma. Kuna wengine kazi yao ni kuhubiri na kuwaambia watu waache dhambi kama, uasherati na wizi. Ni wajibu wa wale wanaoshughulika na mambo ya miradi ya maendeleo katika kanisa ni kusaidiana na wahubiri hao kuwaongoza watu waishije baada ya kuacha uasherati na wizi. Napenda kukuhimiza hata wewe unayeyasoma haya kuwa, ukiona mwenzako ni mhitaji wa kitu fulani ambacho unacho, usisite kumsaidia. Kumbuka huduma hii ina thawabu yake kama Mtume Paulo anavyosema. Hebu jibu swali hili; “Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?" (1Yohana 3:17) Mzee Yohana anatushauri anasema, “Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli” (1Yohana 3:18). Ni kweli Bwana Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani alikuwa maskini, lakini baada ya kufufuka alirudishiwa utajiri wake. Ndiyo maana Mtume Paulo anazungumzia juu ya “……… utajiri wake Kristo usiopimika” (Waefeso 3:8). Na katika Wafilipi 4:19 tunasoma hivi; “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu”. Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alichukua madhaifu yetu na magonjwa yetu yote, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona (Isaya 53:5; Mathayo 8:16, 17; 1Petro 2:24). Na kwa kujua hili kanisa linajihusisha na kuombea wagonjwa na kutoa huduma za afya kwa wagonjwa. Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alichukua dhambi zetu na akafanyika dhambi kwa ajili yetu, “Ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye” (2 Wakorintho 5:21). Na kwa kujua hili kanisa linahubiri habari za ondoleo la dhambi kwa ye yote atakayemwamini Kristo. Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alikuwa maskini, ingawa alikuwa tajiri, ili kwa umaskini wake sisi tupate kuwa matajiri (2Wakorintho 5:21). Na kwa kujua hili kanisa linajihusisha na miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili mtu aondokane na umaskini. Wakristo binafsi pia wanashauriwa kuwa na miradi isiyovunja maadili ya kikristo, ili waondokane na umaskini. |
![]() |
![]() |
![]() |
|
![]() |
Sura ya Nane SADAKA NA WOKOVU
“Palikuwa na mtu Kaisaria jina lake Kornelio,
akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na
nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu SADAKA NYINGI, na kumwomba Mungu
daima. Akaona katika maono waziwazi, kama
saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!
Akamtazama sana,
akaogopa akasema, kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na SADAKA ZAKO
zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. Sasa basi, peleka watu Yafa,
ukamwite Simoni, aitwaye Petro. Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simoni,
mtengenezaji wa ngozi, ambaye nyumba yake iko pwani; ATAKUAMBIA YAKUPASAYO
KUTENDA” (Matendo ya Mitume 10:1 – 6).
Tabia hii ya Kornelio ya kuwa mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba
yake yote, na pia tabia ya utoaji wa sadaka na kumwomba Mungu daima,
inaonyesha wazi kuwa Kornelio alimpenda Mungu sana na alikuwa anatafuta namna
yakukubalika mbele zake na namna ya kumpendeza Yeye.
Tungezungumza kwa lugha nyepesi zaidi, ni kwamba alitaka kwa MATENDO YAKE
aende mbinguni na kuurithi Uzima wa Milele baada ya kufa kwake . Kwa kifupi
alimtafuta Mungu kwa njia ya Matendo.
Hii ina maana ya kuwa Kornelio alitaka kuvuna baraka za Agano Jipya
katika damu Yesu, wa kutumia njia za kupendeza Mungu zilizomo katika Agano la
Kale.
Tena ingawa yeye hakuwa Myahudi kwa kuzaliwa, alitaka sana kuvuna baraka ambazo Mungu aliahidi
juu ya Wayahudi.
Mpaka hivi leo kuna watu wengi wanataka kuvuna baraka toka kwa Mungu bila
kutumia utaratibu aliouweka Mungu wa kuzipokea. Ni vigumu sana kupokea ahadi za Mungu nje ya mpango
wake.
Huwezi kupokea ahadi za agano la kale kwa kutumia mbini za agano la kale na
huku sasa hivi tumo katika kipindi cha agano jipya.
Baraka zote zilizomo katika agano la kale aliahidiwa Ibrahimu na uzao wake
MILELE. Soma mwenyewe Mwanzo sura ya 17 na 22. Kwa hiyo ukitaka kupokea
baraka za agano la kale lililofungwa kati ya Mungu na Ibrahimu, inabidi uwe
mzao au mtoto wa Ibrahim. - Kornelio hakufahamu hili; hata leo hii wengi
hawafahamu.
Baraka zote zilizomo katika agano jipya zimeahidiwa wale walio ndani ya
Kristo – waliotoa maisha yao kwa Yesu kama
vile Yesu Kristo alivyotoa maisha yake kwa ajili yao.
Ni vigumu kupokea baraka za ahadi za agano la kale na zile za agano jipya NJE
YA YESU KRISTO. Imeandikwa hivi katika Wagalatia 3:13,14,29;
“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, baraka ya Ibrahimu IWAFIKILIE MATAIFA KATIKA YESU KRISTO, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani…… Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi. "
Ndiyo maana Mungu alimtuma Malaika
wake ili amwambie Kornelio kuwa amwite Simon Petro ili awaeleze habari za
Yesu Kristo – ili baraka ya Ibrahimu iwafikie na wapate kupokea ahadi ya Roho
kwa njia ya imani – SIYO KWA MATENDO PEKE YAKE.
Jambo ambalo Mungu alitaka Kornelio ajue na sisi pia tujue ni kuwa matendo mema, maombi na SADAKA bila “kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani” yaani kuzaliwa mara ya pili kwa Roho au kuokoka – haitoshi kumpendeza Mungu, wala kukubalika mbele zake au kuhesabiwa haki. Ndiyo maana Yesu Kristo alimwambia Nikodemo, yule Farisayo kuwa “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu ….. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, HAMNA BUDI kuzaliwa mara ya pili”(Yohana 3:3,7).
Haya maneno “Hamna Budi” maana yake ni
“lazima” kwa hiyo Yesu Kristo alikuwa
anasema “…… LAZIMA kuzaliwa mara ya pili”.
Yesu Kristo alikuwa anasisitiza kwa Nikodemo, na hata kwetu sote tunaotaka
kuurithi ufalme wa Mungu, kuwa hakuna njia nyingine isipokuwa LAZIMA kuzaliwa
mara ya pili kwa Roho (au kwa maneno mengine) LAZIMA Kuokoka!
IMANI
NA MATENDO
Matendo peke yake hayatoshi kukupa ufalme wa Mungu. Kuna watu wengi sana ambao ni waaminifu sana katika kusali na kumtolea Mungu
sadaka, lakini hawakubaliani na jambo kuokoka. Wanaona kuwa wao tayari
wameokoka kwa sababu tu wanasali, wanatoa sadaka na kujitahidi kuishi katika
matendo mema. Hebu soma maneno ya mistari hii uone yanavyopingana
na msimamo huu;
“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; WALA SI KWA MATENDO, mtu awaye yote asije akajisifu” (Waefeso 2:8,9)
Tunaokoka kwa njia ya imani itendayo kazi katika Yesu Kristo, “Wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”.
Matendo yana faida zaidi kwa mtu baada ya kuokoka. Na pia imani bila matendo,
imani hiyo imekufa nafsini mwake. Biblia inasema hivi:
“Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya
kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! ile imani yaweza kumwokoa?….
Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. Lakini
mtu atasema, wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako
pasipo matendo, nami nitakuonyesha IMANI YANGU KWA NJIA YA MATENDO YANGU ……..
Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo
matendo imekufa” (Yakobo 2:14,17,18,26).
Jambo ambalo Yakobo alikuwa anasisitiza hapa ni kutaka kuwaonya watu kuwa
kusema wewe ni mkristo na huku matendo yako hayalingani na ushuhuda wa mdomo
wako ni bure. Wokovu uonekane katika maisha yetu kila siku – la sivyo imani
tuliyo nayo inakosa kuzaa matunda ya uzima wa milele. Ndiyo maana Yesu Kristo
aliwahi kuzungumza juu ya kukatwa kwa tawi (Mkristo) lisilo zaa, soma Yohana
15:1-8 ili upate picha zaidi juu ya jambo hili.
CHUKUA HATUA LEO
Malaika alimwambia Kornelio atume watu wakamwite Simoni aitwaye Petro ili
AMWAMBIE YAMPASAYO KUTENDA. Mungu kwa uweza wa Roho wake Mtakatifu amekuletea
maneno haya mkononi mwako ili UFAHAMU YAKUPASAYO KUTENDA.
Kama hujaokoka na unadhani unaweza kuokoka
kwa kutoa sadaka nyingi NAKUSHAURI KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI uombe
sala hii kwa sauti, ili utubu na kumpa Yesu Kristo maisha yako leo. HALAFU
endelea kutoa sadaka nyingi ukiwa ndani ya Yesu Kristo.
Omba sala hii kwa sauti; “Mungu Baba, unisamehe
dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu. Ninatubu kwako. Nitakase
kwa damu ya Yesu Kristo. Bwana Yesu Kristo nimefungua moyo wangu
nakukaribisha uingie ndani yangu, kwa uwezo wa Roho wako. Uwe Bwana na
Mwokozi wa maisha yangu – sasa na hata milele. Asante kwa kunisamehe dhambi na
kuniokoa. Amina”.
Ikiwa umeisema sala hii kwa uaminifu, basi umefanyika kiumbe kipya –
umezaliwa mara ya pili na Mungu hakumbuki dhambi zako tena. Soma 2Wakorintho
5:17, Waebrania 8:12. Karibu sana
katika ufalme wa Mungu kwa jina la Yesu Kristo!
Hili ndilo lililotokea kwa Kornelio na jamaa yake, Simoni Petro alipofika
kwao aliwaambia habari za Yesu Kristo – walisikia maneno hayo wakamwamini
Yesu na kujazwa na nguvu za Roho Mtakatifu wakati huo huo.
|
![]() |
Sura ya Tisa
NATOA LAKINI SIPOKEI –
NIFANYEJE?
Kuna wakati fulani, mtu mmoja alinifuata baada ya kipindi nilichokuwa
nafundisha Neno la Mungu juu ya utoaji, na akaniuliza hivi; “Kwa nini mimi
nimekuwa natoa zaka na sadaka nyingi lakini sipokei? Hata miradi niliyo nayo
haifanikiwi nilivyokusudia – ni kwa nini iwe hivyo.
Inawezekana na wewe unayesoma ujumbe huu sasa una maswali kama
haya. Hayo ni maswali ya msingi na ni muhimu tupate ufumbuzi wake. Hata
mkulima ambaye alipanda mbegu katika shamba, na asipate kitu au apate mavuno
machache, atajiuliza maswali kumetokea kitu gani.
Tukumbuke ya kuwa si mapenzi ya Mungu tuwe maskini – tuwe na hali ngumu
kimavazi, chakula na kiafya. Pia, tukumbuke ya kuwa ni tabia ya kiuungu mtu
kutoa na kutegemea kupokea. Ingawa si lazima upate toka kwa mtu huyo huyo
uliyempa, - maana Mungu anaweza kumgusa mtu mwingine akupe – lakini utaratibu
wa Mungu unabaki pale pale, ukitoa tegemea kupokea.
Ni kitu gani kinasababisha mtu asipokee na huku amekuwa akijitahidi kutoa?
Biblia inatuambia ya kuwa tukiwa waaminifu katika utoaji, Mungu atatumwagia
baraka, “hata isiwepo nafasi ya kutosha ya kuziweka” – Je! umewahi kumsikia
mkristo yo yote akisema amepata baraka nyingi mno hata amekosa mahali pa
kuziweka?
Sababu
zifuatazo zitatusaidia kujua ni kwa nini hatufanikiwi katika utoaji wetu – na
hata hatupokei kama tulivyotegemea na
kutarajia;
1. KUVUNJA
MIIKO AU UTARATIBU WA UTOAJIKila jambo lina utaratibu wake – usipoufuata usitegemee mavuno mazuri. Kilimo cha mahindi kina utaratibu wake wa upandaji na palizi tofauti na kilimo cha ngano au cha kabichi. Ndiyo maana wataalamu wa kilimo, walianzisha kampeni za kuwafundisha wakulima juu ya “kilimo cha kisasa” ili kiwasaidie wakulima kupata “mavuno” zaidi toka katika mashamba yao.
Hata katika “kupanda na kuvuna” au “kutoa na kupokea” katika mambo ya Mungu
kuna utaratibu wake. Ukienda kinyume na utaratibu huo, usitegemee mavuno ya
kuridhisha toka katika utoaji wako
Kwa mfano hebu soma na kutafakari maneno
haya yafuatayo:
“Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama ilivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu” (2Wakorintho 9:6,7).
“….wala si kama
kitu kitolewacho kwa unyimivu” (2Wakorintho 9:5).
Utaona katika mistari hiyo Mungu ametueleza kwa kiasi fulani utaratibu ambao
anataka ufuatwe mtu akitaka kuvuna katika utoaji wake. Je! unafuata utaratibu
huu katika utoaji wako?
Utaratibu huo ni huu; utoaji wako uwe si haba (au kidogo) bali uwe kwa
ukarimu. Ukitoa kidogo utapata kidogo – bali ukitoa vingi utapata vingi.
Ndiyo maana imeandikwa;
“Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha
kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu
watakachowapa vifuani mwenu. KWA KUWA KIPIMO KILE KILE MPIMACHO NDICHO
MTAKACHOPIMIWA” (Luka 6:38)
Kama unataka kutoa sadaka tu “ kama
ulivyokusudia moyoni mwako”. Kama ulikusudia
kutoa shilingi 100/= toa shilingi 100/=. Fanya hivi siku zote na utafanikiwa.
Tena, utoaji unatakiwa ufanyike “si kwa huzuni; wala si kwa lazima; maana
Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu “… na wala si kwa
unyimivu”.
Michango mingi iliyomo makanisani siku hizi wakati mwingine inafanyika
kwa kulazimishana. Mtu anatakiwa atoe kwa kupenda kwake toka moyoni mwake –
SI KWA LAZIMA. Kumlazimisha mtu kutoa ni kwenda kinyume cha utaratibu wa
utoaji.
Wakristo wengi wamekosa baraka au mafanikio katika utoaji kwa sababu wanatoa
huku WANAHUZUNIKA AU WANALALAMIKA! Wengi wanawanung’unikia viongozi wa
makanisa yao
kuwa wanatumia fedha au vitu vibaya. Kama
una wasiwasi na matumizi ya matoleo yako – yaombee kwa Mungu ayalinde
yatumike kwa utukufu wake kuliko kulalamika.
Wengine wanahuzunika na kulalamika kuwa michango imezidi. Je! umewahi
kumsikia mkulima akihuzunika au kulalamika kwa kuwa ameongezewa shamba la
kulima na kupanda? Hakuna. Mkulima halalamiki bali anafurahi kwa kuwa amepata
eneo kubwa zaidi la kupanda umeongezewa eneo la KUPANDA ili AVUNE ZAIDI. Ni
eneo la kukusaidia kutoa zaidi ili UPOKEE ZAIDI!
2. IBILISI
AMEZUIA BARAKA ZAKO;Kati ya baraka ambazo zinapatikana kutokana na mtu kuwa mwaminifu katika utoaji wa zaka (fungu la kumi) na dhabihu (matoleo mbalimbali) na kuzidiwa wakati wa matatizo, Mungu alisema hivi; “Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba ….” (Malaki 3:11). Ni wazi kuwa aliye nyuma ya kuharibika kwa mazao shambani au biashara ni yule ‘alaye’ ambaye ni Ibilisi. (Hii ni kama mkulima au mfanya biashara amefanya anachotakiwa kukifanya kilicho ndani ya uwezo wake). Kinyume cha jambo hili ni kwamba usipokuwa mwaminifu kutoa fungu la kumi toka katika mazao ya shamba lako, usitegemee Mungu akupiganie wakati mharibu anapoingilia mimea yako na kuiharibu. Vile vile usipokuwa mwaminifu kutoa fungu la kumi toka katika mapato ya biashara yako, usitegemee Mungu akusaidie wakati mharibu anapoingilia biashara yako na kuiharibu. Inawezekana unatoa sadaka, na huoni baraka zozote zinazotokana na kutoa kwako – hebu angalia na jichunguze kama umekuwa mwaminifu katika kutoa ZAKA KAMILI. Kwa mfano kama fungu la kumi la pato lako ni shilingi 2,000 – toa zaka kamili yaani shilingi 200/=. Usitoe pungufu ya hiyo maana haitakuwa zaka KAMILI. Ikiwa umekuwa mwaminifu katika kutoa Zaka kamili na dhabihu halafu huoni matokeo yake basi, tumia mamlaka ya Jina la Yesu Kristo – mfunge na kumkemea ibilisi ambaye ndiye mharibu wa mali yako aondoe mikono yake juu ya mali yako. Kumbuka Yesu Kristo alisema; “Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalofunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Mathayo 16:19).
Kuna mtumishi mmoja wa
Mungu ambaye anasimulia jinsi ambavyo mkulima mmoja wa pamba alivyosaidika na
uwezo wa jina la Yesu Kristo.
Huyo Mkulima alikuwa
mwaminifu katika kumtolea Mungu fungu la kumi la mapato ya shamba lake kila
mwaka, na alikuwa haelewi kwa nini pamba yake ilikuwa haifunguki ingawa muda
wa kufunguka na kuchanua ulikuwa umefika. Wataalamu wa kilimo cha pamba
walikuja kuliangalia shamba hilo lakini
hawakuweza kumsaidia mkulima huyo kutatua tatizo hilo.
Mtumishi wa Mungu huyo
alifika hapo, na alisikia habari ya mahangaiko ya mkulima huyo. Baada ya
kufahamu ya kuwa mkulima huyo alikuwa mwaminifu katika kutoa fungu la kumi –
alimwambia waende shambani ili waombe.
Huyo mtumishi wa Mungu
wakiwa shambani na mkulima huyo; - akimkumbusha Mungu juu ya ahadi yake ya
Malaki 3:7-11. Na mwishoni akamwamuru ibilisi aondoke kwenye pamba hiyo. Mara
tu baada ya kumaliza sala hiyo – pamba ilianza kufunguka na kuchanua! Bwana
asifiwe sana
kwa uwezo huu ulivyo wa ajabu.
Usibaki unalalamika na kuhangaika kama vile
mtu asiyejua ahadi za Mungu. Simamia haki zako ndani ya Kristo kwa kuwa
mtendaji wa neno na utafanikiwa.
3.
KUTOKUPANDA KATIKA UDONGO MZURIUtoaji ni sawasawa na upandaji. Mtu akipanda anategemea kuvuna pia. Kwa hiyo mtu akitoa anategemea kupokea.
Mkulima yo yote
akitaka mavuno mazuri toka shambani mwake kati ya vitu anavyoviangalia ni
aina ya mbegu na aina ya udongo. Siku zote atapanda kwenye udongo mzuri wenye
rutuba.
Mfanya biashara siku zote anataka aweke mtaji wake katika vitu vitakavyomletea faida kibiashara na siyo hasara. Lakini, inasikitisha kuona kuwa inapofika wakati wa utoaji – wakristo wanatoa tu bila kuangalia kwanza “udongo mzuri” ni upi ili utoaji wao uwaletee matokeo mazuri.
Biblia inatuambia
katika mfano wa mpanzi ya kuwa mbegu zingine“….
Zikaanguka penye udongo ulio mzuri, zikazaa matunda, zikimea na kukua, na
kuzaa, moja thelathini, moja sitini, na moja mia” (Mathayo 4:8).
Je, “udongo mzuri” unaoleta faida nzuri ni
upi? Sehemu za kutoa zenye matokeo au mavuno mazuri ni hizi zifuatazo;
(a)
Katika nyumba ya Mungu – kanisani ili kuendeleza kazi ya Mungu – soma
Malaki 3:10-11; na Kumbukumbu ya Torati 8:18.
(b)
Kuwasaidia watumishi wa Mungu na watakatifu wake kwa vitu/mali ulizo nazo.
Soma 1Wafalme 17:10-24 na 2Wakorintho 9:10-13.
(c)
Kuwasaidia maskini kwa vitu/mali ulizo nazo. Soma 2Wakorintho 9:8-9.
Angalia upandaji
wako katika utoaji – je! umepanda kwenye udongo ulio mzuri?
4.
KUKATA TAMAAWagalatia 6:9 inasema hivi; “Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho”. Tafsiri iliyo nyepesi inasema, “maana tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa”. Wakristo wengi wanatoa lakini hawana uvumilivu. Mkulima asipokuwa mvumilivu kusubiri mazao ya shamba lake yanayokuja kwa wakati wake – hawezi kuvuna alichopanda. Vile vile mtoaji asiyejifunza kumvumilia Mungu ili amletee matokeo ya utoaji huo kwa WAKATI WAKE – hawezi kuvuna alichopanda. Mungu si mwongo! Wala ahadi zake hazijui kusema uongo. Alichoahidi atatenda. Ukitoa utapokea KWA WAKATI WAKE USIPOKATA TAMAA. Usianze kutafuta njia za mkato ili ufanikiwe – uwe mvumilivu ulichopanda kwenye udongo mzuri utavuna. Mkumbuke Ibrahimu alivyovumilia. Biblia inasema hivi; “Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi” (Warumi 4:20-21). 5.KUTOA KWA MAJIVUNO NA KUTAFUTA KUSIFIWA NA WATU “Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili WATUKUZWE NA WATU. Amin, nawaambieni,wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na BABA YAKO AONAYE SIRINI ATAKUJAZI” (Mathayo 6:1- 4) |
![]() |
Sura ya Kumi
UFANYEJE KATIKA HALI
NGUMU YA UCHUMI?
Matatizo
ya ugumu wa uchumi katika dunia hii siyo mapya. Tangu baada ya mwanadamu
kuanguka katika dhambi – amekuwa mara kwa mara akisumbuliwa na matatizo ya
uchumi. Ukisoma habari za Isaka na za Yakobo utaona jinsi hali hii
ilivyojitokeza.
Lakini
biblia inaeleza wazi kuwa siku hizi ni mwisho. Katika siku hizi za mwisho,
biblia pia inasema wazi kabisa kuwa dunia itapita kwenye vipindi vigumu vya
uchumi
Kwa
Mfano: Katika Mathayo 24:7 na
Ufunuo wa Yohana 6:3-6 tunaona ya kuwa katika siku hizi za mwisho kutatokea
njaa – au upungufu wa chakula. Sababu ya kuja kwa njaa hiyo ni vita
vitakavyokuwa vinatokea katika nchi mbalimbali. Ni wazi kabisa kuwa palipo na
vita au palipo na ugomvi, panakuwa na matatizo ya ulimaji mashamba na usafiri
wa kuleta chakula toka sehemu zingine. Matokeo ni hilo eneo au nchi kukosa chakula, haya
mambo yaliyotabiriwa kutokea siku hizi za mwisho wa dunia.
Ukisoma
katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana sura za 17 na 18 utaona ya kuwa hali ngumu
ya kibiashara imetabiriwa kutokea katika siku hizi za mwisho. Kuuza au
kununua kutafanyika kwa vibali. Watu watapenda fedha sana kuliko kumpenda Mungu. Kutakuwa na
uhusiano mkubwa sana
kati ya utajiri na biashara na uasherati. Wafanya biashara wa siku hizi za
mwisho watakuwa na sehemu kubwa katika utawala wa miji au vijiji wanavyokaa –
hata wakati mwingine katika maongozi ya nchi au mataifa mbalimbali.
Matokeo
ya hali namna hii inawafanya watu watafute njia au mbinu za kuweza kuishi
katika vipindi vya namna hiyo. Lakini ni wazi kuwa si mbinu zote au njia zote
ambazo wanadamu wanazitumia katika kuishi wakati wa hali ngumu ya uchumi
zinampendeza Mungu.
Kunapotokea
hali ngumu ya uchumi, tabia za watu zinabadilika. Mara kwa mara mambo
yafuatayo hutokea;
Kubana matumizi Kununua vitu kwa wingi na kuvirundika Uchoyo –
kupunguza tabia ya utoaji na ukarimu Watu huacha kumtumikia Mungu na badala
yake mtu huitumikia mali Rushwa, wizi na dhuluma huwa ni vitu vya kawaida
Miradi ya kila namna huibuka kuanzia kwa watoto hadi watu wazima.
Jambo
linalowafanya watu wawe na tabia hizi, ni lile la kutaka kutafuta namna ya
kuishi katika kipindi kigumu cha uchumi. Je!mkristo afanye nini ili aishi
katika kipindi hiki kigumu cha uchumi bila kufanya mambo yatakayomkosea
Mungu?
Wakristo
wengine wamefika mahali pa kuhalalisha miradi ya kuwapatia fedha ambayo ni
kinyume na ushuhuda wa kikristo – Je! hii ni sawa?
Wengine
wamefika hata mahali pa kufunga nira na wasioamini (wasio wakristo) KWA JINSI
ISIYO SAWASAWA (yaani isiyokubalika) na neno la Mungu ili waweze kupata fedha
kutokana na mradi wanaofanya pamoja. IKO "jinsi iliyo sawasawa" na
utaifahamu ikiwa utakuwa mtendaji wa neno la Mungu.
Wakristo si wa ulimwengu huu
Ndugu
au Dada unayesoma sasa mambo haya – sikiliza! Sisi kama wakristo si wa
ulimwengu huu ingawa tunaishi hapa ulimwenguni. Fahamu na kumbuka hili kila
wakati. Yesu Kristo alisema hivi;
"Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao
si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Mimi siombi kwamba uwatoe
katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama mimi
nisivyo wa ulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Kama
vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao
ulimwenguni" (Yohana 17:14-18).
Je!
unafikiri Yesu Kristo anaweza kututuma hapa duniani bila kutuandaa kuishi
kiushindi katika majaribu yaliyomo ndani yake na hali ngumu ya uchumi?
Je!
unadhani Yesu Kristo anaweza kukuokoa halafu asikutunze kiuchumi katika
maisha mapya ya wokovu? Nafahamu kuna wakristo wengi walioanguka kiroho kwa
sababu ya kutafuta njia za kujisaidia kimaisha.
Biblia
inatuambia ya kuwa Yesu Kristo huwalisha na kuwatunza watu wake ili ajiletee
kanisa (wakristo) walio watakatifu. Soma Waefeso 5:25-33.
Katika
vipindi vyote vya matatizo ya uchumi, Mungu ameweza kuwalisha na kuwatunza
watu wake. Wamekula na kuvaa na kulala ndani ya mpango wake bila kumkosea.
Katika
siku hizi za mwisho, Kristo anazungumza na kulikumbusha kanisa (wakristo) juu
ya njia au mbinu za kuchukua wakati wa hali ngumu ya uchumi mahali walipo.
Mashauri muhimu ya kufanya
Fuata
maongozi ya Mungu na siyo ya dunia: Ni rahisi sana kusikia na kufuata ushauri wa wanadamu
kuliko ushauri wa Mungu hasa mtu anapobanwa na shida. Lakini kwa mkristo
nakushauri siku zote kuwe na shida au kusiwe na shida, fuata ushauri wa Mungu
kama vile anavyokuongoza kwa Roho Mtakatifu
katika neno lake. Tuangalie jinsi Isaka alivyofanya alipokumbwa na hali ya
njaa.
"Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza
iliyokuwa siku za Ibrahimu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti,
huko Gerari. Bwana akamtokea, akasema, usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi
nitakayokuambia …. Nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki …" (Mwanzo 25:1-3).
Njaa
ilipotokea huko Gerari, watu walianza kuondoka huko na kwenda Misri, ili
kutafuta chakula. Ni wazi ya kuwa hata Isaka alitaka kufanya hivyo. Bwana
akamzuia akamwambia asiondoke bali akae katika nchi aliyomwambia na katika
nchi hiyo atakuwa pamoja naye na kumbariki au kumfanikisha.
Nataka
kukukumbusha ya kuwa baraka za Mungu kwetu hazitegemei jinsi hali ya hewa na
uchumi wa dunia hii unavyokwenda bali zinategemea NENO LA KRISTO.
Isaka
akatii, hakuondoka bali alibaki katika nchi hiyo ambayo watu walikuwa
hawapati chakula wakilima.
"Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo
mia kwa kimoja, Bwana akambariki" (Mwanzo 26:12).
Siku
zote kaa na kufanya kazi mahali ambapo Mungu amekuongoza kukaa. Usihame
mahali au kuacha kazi, bila uongozi wa Mungu. Kufanikiwa kwako hakutegemei
mipango yako bali kunategemea mpango wa Mungu.
Ukiwa
ndani ya Kristo utafanikiwa mahali po pote pale ambapo Mungu atakapokuweka
hata kama mazingira yake kibinadamu si
mazuri kwa kufanikiwa. Ukiwa ndani ya Kristo, "Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani … utabarikiwa
uingiapo, utabarikiwa utokapo …. Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika
ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika
nchi akupayo Bwana, Mungu wako" (Kumbukumbu ya Torati 28:3,6,8).
Endelea kutoa hata wakati wa upungufu
Katika
hali ya kibinadamu upungufu unapotokea mahali watu wanabana matumizi – na
hali ya ukarimu na utoaji huwa inafifia sana
hata wakati mwingine kupokea kabisa. Wakristo wengi pia wamekumbwa na hali
hii – wanasema wamepunguza utoaji kwa kuwa wamepungukiwa na hali ya uchumi ni
ngumu. Je! hii ni sawa?
Wakati
wa ukame ulipotokea wakati wa maisha ya Nabii Eliya Mtishbi; Bwana alimwambia
Eliya, "Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa
Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe"
(1Wafalme 17:9).
Unakumbuka
jinsi yule mama alivyojitetea wakati Eliya alipofika kwake ili alishwe? Yule
mama alijitetea kama watu wengine
wanavyojitetea siku hizi wakitakiwa kutoa au kuchanga walivyo navyo kwa ajili
ya kazi ya Mungu. Naye yule Mjane akasema;
"Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga
katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili
niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tule tukafe" (1Wafalme 17:12).
Kwa
jinsi ya kibinadamu, Eliya angeweza kumwonea huruma yule mama, asile chakula
chake; na aondoke na aende kwa matajiri wa siku zile kupata chakula. Lakini
Eliya hakufanya hivyo- bali ALITII MAAGIZO YA MUNGU. Eliya akamwambia yule
mjane hivi;
"Usiogope;enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie KWANZA mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi
yako na mwanao" (1Wafalme 17:13).
Ndivyo
yule mama alivyofanya – alimpa KWANZA
MUNGU kwa kupitia mtumishi wake. Mungu akambariki yule mama kwa ukarimu
na utoaji wake wakati alipokuwa na upungufu. "Lile
pipa la unga HALIKUPUNGUKA, wala ile chupa ya mafuta HAIKUISHA sawasawa na NENO
LA BWANA alilolinena kwa kinywa cha Eliya" (1Wafalme 17:16).
Katika
hali ya upungufu ulionao, usiwe mchoyo bali endelea kumtolea Mungu, naye
atakubariki na kukufanikisha. Na hii itaonyesha ni kwa kiasi gani unamtegemea
Mungu wako na Neno lake.
Lazima
ufahamu ya kuwa Yesu Kristo anaangalia sana
jinsi tutoavyo. Siku moja akiangalia jinsi watu watoavyo fedha; "Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawambia,
Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la
Hazina; maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu
katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote
pia" (Marko 12:43-44). Soma na kuyatafakari tena maneno hayo
ya Yesu Kristo, halafu jiangalie jinsi utoavyo. Huyu mjane hakuwa na mali ya
kutosha alikuwa maskini, lakini bado aliendelea kumtolea Mungu! Je wewe una
la kujitetea katika kutomtolea Mungu wakati wa upungufu wako?
Weka hazina yako mbinguni
Yesu
Kristo alisema;"Msijiwekee hazina duniani,
nondo na kutu viharibupo,na wezi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina
mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wezi hawavunji wala
hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako"
(Mathayo 6:19 – 21).
Utoaji
wako utaonyesha kama moyo wako uko kwa Yesu
au unaitegemea dunia. Moyo wako ukimtegemea sana Yesu, utatoa zaidi kwa ajili ya kazi
ya Mungu kuliko mahali pengine. Mkristo anapopoa kiroho, utoaji wake HASA kwa
kazi ya kuhubiri injili nao unapungua. Hata hivyo Biblia inatuambia katika
siku za mwisho upendo wa wengi utapoa.
Mtolee
Mungu zaka na dhabihu (matoleo) bila kuchoka, nawe utakuwa umeweka hazina
yako mbinguni – mikononi mwa Mungu – ambamo wezi hawawezi kukuibia. Naye
Bwana atakurudishia mara nyingi zaidi. Mradi mzuri na wenye uhakika wa mavuno
kwa Mungu na kwako wakati wa hali ngumu ya uchumi ni mradi wa kuhubiri
injili. Kwa hiyo siku zote hakikisha umeweka kiasi fulani katika mradi wa
kuhubiri injili.
Dumu katika maombi
Hili ni
muhimu sana.
Kwa kuwa wakristo wengi wakiwa katika hali ya ugumu wa maisha na uchumi,
wanapoa katika maombi – na wanakumbwa na majaribu ambayo mara nyingi
yanachafua ushuhuda wao. Soma Luka 21:36, Mathayo 24:42 – 51 na Mathayo
26:41. Kwa hiyo dumu katika maombi, usikate tamaa, hata wakati wa hali ngumu
kiuchumi kwa upande wako – bado zidi kudumu katika maombi.
|
Subscribe to:
Posts (Atom)