Sunday, April 22, 2012

MAN UNITED YAVUTWA, MAN CITY YACHANJA MBUGA

TIME YA MANCHESTER UNITED LEO IMEVUTWA SHATI BAADA YA KULAZIMISHWA KUTOKA SARE YA 4 KWA 4 KATI YAKE NA EVERTON, MPINZANI WAKE KATIKA MBIO ZA UBINGWA MAN CITY IMEIBUGIZA WOLVE KWA JUMLA YA MAGOLI 2 kufuatia kazi nzuri ya nasri na aguelo sasa mahasimu hao wanapishana kwa point 3 tu ambapo mchezo unaofuata utawakutanisha wao wenyewe tarehe 30 april http://www.bbc.co.uk/sport/0/football/17718140 http://www.bbc.co.uk/sport/0/football/17718154

WEEKEND LEO "KIGAMBONI"

Wakati watanzania kote nchini wakiwa wamegubikwa na tetesi za kujiuzuru kwa mawaziri sita, shughuli za starehe katika jiji la Dar es salaam ziliendelea kama kawaida. hapa kamera yetu ilivinjari viwanja vya kigamboni katika maeneo mbalimbali

Friday, April 6, 2012

Sunday, April 1, 2012

CHADEMA YASHINDA UBUNGE ARUMERU

hot nuuuuuuz: CHADEMA YASHINDA KITI CHA UBUNGE ARUMERU MASHARIKI, MATOKEO YATANGAZWA ASUBUHI HII https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi58_eY5OBEEC45O7mX9dGMOuHoHYKtPWxUyp9mNTzJJCZ1VZXnbxGyJhnH2ow3e9eR1VnuwWNY-Ph9Mace56znZntrHNbMZS1PQOcQQnwYqTrOTAhgSkyylR1ExTn976UopVI4SAV_kTk/s640/jo.jpg Mbunge mteule wa Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nasari akiongea baada ya kutangazwa kuwa mshindi asubuhi hii huko Arumeru Matokeo ya kura za Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki yametangazwa sasa hivi na Msimamizi wa Uchaguzi na Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Bw Gracias Kagenzi amemtangaza mgombea wa CHADEMA Bw Joshua Nassari kuwa mshindi baada ya kupata kura 32,972 dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka CCM Bw Sioi Sumari aliyepata kura 26,757 Matokeo kwa Vyama vingine sita vilivyoshiriki ni kama ifuatavyo DP -77 NRA - 35 AFP - 139
UPDB - 18 TLP - 18 SAU - 22 Kwa mujibu wa Bw Kagenzi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na aliojitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696 ambapo kura halali zilikuwa 60,038 na zilizoharibika ni kura 661. Wakati huo huo, habari kutoka Mwanza zinasema CHADEMA kimeshinda katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kirumba mkoani Mwanza. Msimamizi wa uchaguzi huo, Bw. Aloyce Mkono, amemtangaza kuwa mshindi mgombea wa Chadema Mh Dany Kahungu kwa kura 2,938 dhidi ya mgombea wa CCM Mh Jackson Masamaki aaliyepata kura 2,131. Wagombea wengine walioshindwa vibaya katika uchaguzi ni pamoja na Mh Haji Issa wa CUF aliyepata kura 184, Mh Kasala Muhana wa UDP amepata kura 7 na Mh Athuman Jumanne wa NCCR Mageuzi aliyeambulia 0 katika uchaguzi huo . Msimamizi huyo alisema kuwa uchaguzi huo umefanyika katika hali ya amani na utulivu,na kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo na kuonyesha utulivu mkubwa wakati wa uchaguzi na zoezi la kutangazwa kwa matokeo. Kwa hisani ya Michuzi Blog